Tatizo la Corona: Wa kulaumiwa ni Serikali kwa asilimia 100%

Kama tungekubaliana wote tungeiweka kwenye karantini mikoa yote yenye maambukizi. Hakuna mtu kutoka wala kuingia. Kama ni suala la uchumi tutalijadili baadaye baada ya kumpiga na kumshinda adui. Hivi anakosekana mwenye maamuzi wa kuwaza kama mimi?
Mkuu jana sijui juzi tu wametangaziwa kuwa wa Dar wabaki Dar leo asubuhi Ubungo Terminal hapakanyagiki...….Ndicho kilichotokea kwenye jimbo moja la Italy...……..Watu walikimbilia jimbo lingine wakidhani watakuwa salama kumbe ndio wamepeleka maambukizi..(Hawa wetu wanakimbilia mikoani - pengine vijijini ambako wazee na wale wenye magonjwwa yasiyotibika wameshindikana na kurejeshwa vijijini ndio wapo...………) hatuombei ila tusikilizie tu
 
Mkuu jana sijui juzi tu wametangaziwa kuwa wa Dar wabaki Dar leo asubuhi Ubungo Terminal hapakanyagiki...….Ndicho kilichotokea kwenye jimbo moja la Italy...……..Watu walikimbilia jimbo lingine wakidhani watakuwa salama kumbe ndio wamepeleka maambukizi..(Hawa wetu wanakimbilia mikoani - pengine vijijini ambako wazee na wale wenye magonjwwa yasiyotibika wameshindikana na kurejeshwa vijijini ndio wapo...………) hatuombei ila tusikilizie tu
Pendekezo langu siyo hilo la kukimbilia mikoani bali la kuzuia kuingia wala kutoka angalau kwa siku 14
 
  • Thanks
Reactions: Mj1
Pendekezo langu siyo hilo la kukimbilia mikoani bali la kuzuia kuingia wala kutoka angalau kwa siku 14
Nimekuelew mkuu………… Nilikuwa natoa tu angalizo kwa kuzingatia hali ya sasa……..uko sahihi kabisa.
 
Tatizo la Corona wa kulaumiwa ni serikali kwa asilimia 100% nitawalaani mpaka kaburini

Nina sababu ya kusema serikali ndo ya kulaumiwa kwa sababu zifuatazo

KWANZA kabisa kipindi mwezi wa pili na wa tatu Corona ilivyoanza kuwa serious ninyi mliendelea kuwapokea watalii na wachina tena bila kificho mkisema kuwa hamtaki kupoteza mapato na watalii kwa sababu ya Corona

PILI ni kwamba mliendelea kuruhusu wageni na safari zikiendelea bila kujali watu wetu watakaoambukizwa mkijimwambafai kwamba mmejizatiti kwa kuwapima watu Airports

TATU mlikua mnaidharau Corona Rais na Makonda walikua wakidharau Corona wakiita kuwa ni kaugonjwa kadogo tu hako na kasiwatishe watanzania huku mkisema ni kaugonjwa kadogo mngekua basi hata mmejiandaa kufanya tafiti ya dawa za asili na kuandaa mazingira ya kukabiliana na Corona. Halafu sasa hivi mnasema tuombe my dear government maombi hayatosaidia chochote mungu hadhihakiwi na wala hapendi unafiki!

NNE hamkufunga mipaka hata mpaka sasa sidhani kama mmefunga sijui mnataka tufe wote?

TANO mliwapa wanasiasa nafasi mkaingiza siasa kwenye ugonjwa mara polepole aite wapinzani Corona mara makonda atoe matamko ya hovyo hovyo sasa hivi mambo yamekua magumu mnasema tuombe maombi hayatosaidia chochote kile nawaambia maana mlikufuru mkasema korona ni kaugonjwa kadogo sana.Mmesahau suala la bashite kumtangaza mtoto wa mbowe kuwa ana Corona na kwamba ni mungu kaleta Corona kwa familia ya Mbowe

SITA hili ni kosa kubwa sana mlificha data za ugonjwa wa Corona sijui mlikua mnamaanisha nini mfano tu mdogo kulipotiwa Corona Zanzibar na mgonjwa mkabisha lakini baadae ikaja kuonekana ni kweli,mlificha sana na sasa mmeona hali ni mbaya hadi waziri anakiri alikua anaficha ficha lakini sasa ameamua kuwa muwazi mmepika data na mnaendelea kuficha maana watu wanakufa wengine ni ndugu zetu kabisa na tena wanakufa kwa Corona mnawazika lakini cha ajabu hairipotiwi

Sasa hivi mmeona hali ni mbaya Mloganzila imejaa ndio mnakumbuka shuka kumekucha watu wameathirika wengi mnoo Corona inatembea mtaani kama nzi mmekumbuka shuka kumekucha watanzania wengi wanaenda kupoteza maisha kwasababu ya uzembe wenu

Wa kulaumiwa ni serikali ya awamu ya tano kwa asilimia 100 na nitawalaani mpaka kaburini
Kwani jamaa wa kaugonjwa kadogo amerudi mjini au bado yuko chattle😍😍😃😂🐃
 
Badala ya sisi wananchi kuona ni namna gani tuweze kujikinga mmoja mmoja na kuzingatia maelekezo ya wataalamu, ndo kwanza tunaanza kulaumu serkali kanakwamba serikali ndo walio uleta ugonjwa ,na pia hata hiyo lockdown unayoitaka wewe au unayotaka kuiga kutoka kwa wenzetu jarbu kuangalia na mazingira yao na yetu ulinganishe sio kila kitu successful kwao na uku kitakuwa successful hali ya uchumi mbaya wananchi maskini asilimia kubwa ya watu wanategemea kipato cha kila siku kuilisha familiya na serikali haina pesa yakusema kuwalisha watu kama ikiamua lockdown afu na lockdown yenyewe ni hadi lini ?? Na huku hata dawa haijulikani itapakina lini ??
Watu watakaa lockdown hadi lini ?? Marekani walipitisha bajeti ya dollar tirrioni we una hiyo pesa ?? Mi nadhani watu wangezingatia haya

Kwanza ,kuvaa mask kwa kila MTU kila wakati pamoja na gloves.

Pili,Kuwa na sanitizers ya kujisafisha kila Mara.

Tatu,Kuepuka misongamano isiyo na lazima mfano huna haja ya kuenda k.koo kama bidhaa huska unaweza ipata mtaani kwako.

Nne,Kuripoti mapema kituo cha afya pale unapohisi joto kupanda na dalili kama mafua.

Tano,Kuepuka kuzurura mitaani bila sababu ya msingi.

Sita,Kujiziba pale tunapo piga chafya.

Saba,Kujitahidi kukaaa mbali na watu wengine kwa mita kadhaa.

Nane,Kuzingatia na Kuepuka kujishika maeneo ya mdomoni,puani na machoni kabla ya kunawa

Mwisho ,Watu mnalaumu serikali na huku hata kujikinga wenyewe mnapuuzia,afu asilimia kubwa ya wanaotaka lockdown ni watumishi wa serikali maana mnajua mshahara wenu upo pale pale ,vipi kama mkiambiwa mkatwe nusu ya mishahara kwaajili ya lockdown mtakubali ili hiyo pesa isaidie wale wasiojiweza ?

Nobody.
Hivi unajua kwanini kuna Serikali? Sio kwamba inatakiwa ifanye kila kitu lakini unaelewa wajibu wake hasa katika masuala kama haya
 
ahahahhaa nasikia covid-19 ikonjiani inaitafuta CHATO
Ahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.......unajua watu wanasikilizia siku moja wasikie imemfikia. Nakwambia mtaani itakuwa sherehe. Hili jambo la chuki kwa huyu ndugu limefikia kiwango kikubwa sana hadi binafsi naogopa kwa sababu Mungu anatuhimiza kupendana na kutakiana mema. tatizo ni pale anayetakiwa kupendwa na kuungwa mkono anapokuwa wa kwanza kuumiza wenzake. Ni shida kweli kweli, ikizingatiwa kuwa hakuna kukimbizwa India wala wapi, ni humuhumu tunabanana kwenye vitanda vyetu vya Kibasila wing
 
Wewe ndio watoa taarifa ya uzushi. Hospitali zilizoteuliwa mkoani Dsm ni kwa ajili ya vipimo vya awali vya COVID-19 ili kuongeza uwezo wa upimaji. Mgonjwa akithibitishwa anapelekwa Mloganzira kwa matibabu.

Tumeumbwa na uelewa tofauti hapa duniani, na kila Mungu amekuwa na kusudi naye. Wengine amewaleta awe anajifurahisha anapowatazama (kama vile tu sisi binadamu tunavyoangalia 'comedy')
 
Kumbuka tu kwamba uhai wako uko mikononi mwako unapofanya maamuzi na kuyatekeleza. Uliingia duniani peke yako na utataitoka mwenyewe tu.

Hujui ni kwa nini kuna "Serikali" kila nchi duniani!!! Binadamu angekuwa na uwezo wa kufanya maamuzi mwenyewe, kwa namna unayodhani wewe, nini sasa sababu ya kuweka Serikali itunge sheria na kuweka utaratibu. Kuna kitu wanaita "market failure", huu ndiyo msingi wa uwepo wa "Serikali"! Mashuleni huwa mnaenda kufanya nini!????
 
Serikali ilaumiwa imetengeneza COVID-19, kinga familia yako acheni ni tabia za kulaumu kwa kila kitu, tunpoteza muda mwingi kulaumiani badala ya kutatua tatizo. Ghana ilifunga Mipaka lakini baada ya siku 21 imefungua ila gonjwa bado lipo, ili kuokoa maisha ya watu wake.
 
JPM - Hatuombei ila watanzania wakianza kufa kwa mafungu wanaweza kukugeukia usiamini...

Ushauri: Funga mikoa yote fasta...ruhusu vyakula tu ku move.

Tupo vitani....
 
Hujui ni kwa nini kuna "Serikali" kila nchi duniani!!! Binadamu angekuwa na uwezo wa kufanya maamuzi mwenyewe, kwa namna unayodhani wewe, nini sasa sababu ya kuweka Serikali itunge sheria na kuweka utaratibu. Kuna kitu wanaita "market failure", huu ndiyo msingi wa uwepo wa "Serikali"! Mashuleni huwa mnaenda kufanya nini!????
Kwa hoja yako hiyo pasingekuwepo Bunge na Mahakama katika nchi. Naamini hujanielewa na kamwe hutaniekewa kwa kuwa ni mmoja wa watu ambao huitegemea Serikali kwa kila kitu.

Ebu jiulilize kwa mifano michache ifuatayo: Mbona unaishi kwenye nyumba yenye milango na madirisha? Kwa nini unavaa nguo? Nani anakupangia aina ya chakula na wakati wa kula?
 
Kwa hoja yako hiyo pasingekuwepo Bunge na Mahakama katika nchi. Naamini hujanielewa na kamwe hutaniekewa kwa kuwa ni mmoja wa watu ambao huitegemea Serikali kwa kila kitu.

Ebu jiulilize kwa mifano michache ifuatayo: Mbona unaishi kwenye nyumba yenye milango na madirisha? Kwa nini unavaa nguo? Nani anakupangia aina ya chakula na wakati wa kula?

Nimefahamu kinachotufanya mimi na wewe tusielewane, na maswali yako yana akisi hivyo. Maswali yako yanarudi kwenye hoja yangu, lakini hutoelewa hata ukae ufikirie mwaka mzima (kuna jambo la msingi sana linalotufanya mimi na wewe tusielewane).
 
Well According to My very credible source !!!! Raisi Magufuli akizungumza kwa Video conference kutoka Chato !!! Amepewa Ushauri na Kamati kuu Ya Covid19 Nchini Tanzania , inayoongozwa na Waziri mkuu Majaliwa kuwa the only Thing can save Tanzania Right now ni Herd immunity !!!! sorry kwa typo kwenye picture it’s Herd immunity “
.
.

Kwa Mapendekezo yao !!! Wanatumia Trick walioifanya Wingereza ikafail , ila wao wakkiamini Tanzania haita fail sababu wako na Jua la kutosha na Alternative medicine!!! .
.
.

Walichopendekeza Wataalamu wao since Hospital ziko out of Control , Wagonjwa wamejaa , Mochwari ndo usiseme !!!! basi Mgonjwa asiyeonesha Symptoms asiwekwe hospital !!! Warudishwe nyumbani miili yao ijitibishe yenyewe uku wakifata Ushauri wa kukaa juani na kujitibisha kwa Mitishamba !!!! .
.
.

Pia kuhusu risk ya wagonjwa hao kusambaza , Wamesema ni vizuri wagonjwa hao wasambaze huu Ugonjwa ili watu waupate , wapone na ugonjwa ukijirudia basi hauta kuwa na madhara , Antibodies zitakuwa strong !!! .
.
.

Kwa makadilio yao , Atleast watu 500,000 wanaweza fariki sababu ya Underlying medical Conditions !!! Na Taifa litabaki na watu Milion 50 strong !!! .
.
.

According to them in 3 months Tanzania Itakuwa na wagonjwa zaidi ya Milion 20 !!! But watakao kufa ni kama laki 5 tu !!! Hivyo kuachia Taifa la watu wenye Afya
.
.
Targeted Group la watu wanaoweza Kufariki ni HIV+ , Asthma , Diabetic, Cancer , Hight Blood Pressure , Wenye Magonjwa ya Moyo , Sikocell etc !!!!!!! .
.
.

So Hakuna Plan ya Kulock down !!! Plan ni Kuambukizana, ili wenye strong Immune system wasurvive !!!!! .
.
.

I rest my case !!!! Who are we decide wakukufa na Kupona ili kusave Economy Kwanini tusitumie Nguvu kubwa kusave watu wote ??? Kwanini tusitengeneze Ventilator zetu ??? Kwanini tusishone PPE za kutosha??? Kwanini tusiwatoe hofu na kuwapa training ya kutosha wahudumu wa Afya
.
.
Anyway with that said Hao watu Mnaozika Moshi kila siku , Dar , Tanga , Zanzibar , Mara , TABORA , Mwanza etc !!!! Ndo kwanza Safari Imeanza !!!!! Am so down right now Na hao 500,000 watakao fariki , mtatangaziwa ni watu 50 wamefariki !!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Horrific. Muda wa kuwa zuia hawa watu.

Wazalendo bila kujali vyama mko wapi haya yakiendelea?

Wapinzani na hata CCM mko wapi kikundi hiki kidogo kikiendeleza ubazazi huu?

Bungeni mnafanya nini huko ubazazi huu ukiendelea?

Jamii tumekosa mwelekeo kiasi hiki?
 
Back
Top Bottom