Tatizo la choo kurudisha harufu ndani

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,366
2,397
Harufu inatoka kwenye yale mashimo ya nje (septik) inarudi ndani ya nyumba (chooni).

Inakera sana, choo kinatoa harufu mbaya hata kama hakijatumika kabisa.

Hali hii inasababishwa na nini na je naweza kuizibiti vipi?
 
Pole sana hili tatizo in dogo sana na linatibika, inawezekana sinki likiwekwa vibaya Yale maji yanayozuia harufu kurudi ndani hayatuami vizuri au na pia inatakiwa kuwekwa bomba kwenye chemba ya nje lipande had I usawa was bati kusaidia kupunhuza harufu kutudi ndani

Tafuta Fundi bomba mzuri akague atakushauri cha kufanya mkuu
 
Hizi nyumba za kujenga kimasikini, unajikuta unatumia mafundi wenye uwezo wa kukaririshwa tu, matokeo yake ni gharama mara mbili.

Nyumba mbili nilizowahi kuishi(kupanga) zilisumbua sana kwa hilo tatizo, weka mabomba kila shimo na kwenye vijichemba lakini haikusaidia, maji yanayopaswa kutuama kwenye zile trap, yapo. Nikahama, nikahama na sasa nina shida hiyo tena.
 
1600713323459.png
1600713516068.png


1600713576490.png



Choo kina kitu kinaitwa s-trap, ambayo inakuwa na maji 24/7 ili kuzuia harufu yoyote kuja ndani. Angalia kwa nje kama fundi wako aliweka vent pipe ambayo inazuia maji kwisha kwenye s-trap.
 
View attachment 1576572View attachment 1576585

View attachment 1576588


Choo kina kitu kinaitwa s-trap, ambayo inakuwa na maji 24/7 ili kuzuia harufu yoyote kuja ndani. Angalia kwa nje kama fundi wako aliweka vent pipe ambayo inazuia maji kwisha kwenye s-trap.
Pole sana hili tatizo in dogo sana na linatibika, inawezekana sinki likiwekwa vibaya Yale maji yanayozuia harufu kurudi ndani hayatuami vizuri au na pia inatakiwa kuwekwa bomba kwenye chemba ya nje lipande had I usawa was bati kusaidia kupunhuza harufu kutudi ndani

Tafuta Fundi bomba mzuri akague atakushauri cha kufanya mkuu
Je bomba la nje halijaziba? Je maji kwenye choo yanabaki na kuzuia harufu toga kwenye shimo?
Asante kwa ushauri wakuu. Nilikuwa sijui kumbe yale maji pale chini ndo yanazuia harufu kuja ndani duuh? Baasi inaelekea hiyo sehemu ya kuweka hayo maji ndo kuna shida
 
Angalia maji kwenye choo kama yanakaa.

Angalia bomba la kutolea hewa nje kama lipo.

Solution ya muda mfupi ila hatari kwa watoto, fungua chemba ndogo moja hewa iwe inatokea huko na uifunike na mesh wire while you are looking for a permanent solution.
 
Angalia maji kwenye choo kama yanakaa.
Angalia bomba la kutolea hewa nje kama lipo.
Solution ya muda mfupi ila hatari kwa watoto, fungua chemba ndogo moja hewa iwe inatokea huko na uifunike na mesh wire while you are looking for a permanent solution.
Pamoja mkuu
 
Ni cha kuflash mkuu

System ya choo na maji ya kuongea, maji ya msuaki na maji ya kuoshea vyombo jikoni umechanganya pamoja. Yaani umechimba shimo 1 ambalo linapokea maji ya kuflash choo, maji ya kuongea, maji ya msuaki na maji ya kuoshea vyombo jikon.
 
System ya choo na maji ya kuongea, maji ya msuaki na maji ya kuoshea vyombo jikoni umechanganya pamoja. Yaani umechimba shimo 1 ambalo linapokea maji ya kuflash choo, maji ya kuongea, maji ya msuaki na maji ya kuoshea vyombo jikon.
Ni kweli mkuu, kuna shida kuchanganya?
 
Ni kweli mkuu, kuna shida kuchanganya?
Kuna shida kubwa hapo wataalum wanasema unapounganisha kwa pamoja hiyo system ya maji unafanya Karo libakuwe na kutoa harufu kali. Ni Sawa Sawa na mtu anayebakuwa Kuna gesi anatoa.

MI nipo kwenye ujenzi Fundi wangu alinishauri kutenganisha na akanipa hiyo sababu.

Maji ya msuaki na maji ya kuoshea vyombo na maji ya kunawa pale dinner yanakwenda kwenye Karo lake unachimba shimo alfu unajaza mawe mpaka juu bomba zinaingia kule unatandika viroba juu unaweka na zenge hata maji ya Mvua kama una sehemu ya kuyatoa nje yanaingia humo na huwa alijai kwa sababu kule chini na ukutani haujenge.

Karo la 2 maji yanayoingia Ni maji ya Chooni kuflash na maji ya kuongea. Maji ya kuongea Kuna kifaa inabidi uweke kunisaidia kurudisha harufu
 
Muwe mnatumia wataalamu wa ujenzi kwenye kazi zenu,cheap is expensive,pili muwe mnauliza mashimo 2 ni ya kazi gani na ni maji yapi yaingie shimo dogo na yapi shimo kubwa,technically shimo dogo ni kwa ajili ya choo tu na maji mengine yote ni shimo kubwa na kila moja Lina utaratibu wake wa kuyajenga.
 
Choo chako kimekosa kitu kidogo ila muhimu sana, TRAP. Mwambie fundi akuwekee trap.
 
Naona karibu WOTE wanazungumzia suala "maji hayakai"!!

Mimi sio fundi lakini I doubt kama chemba inanyonya maji, na matokeo yake isije ikawa imejaa machafu yenye harufu ya hovyo na kufanya harufu ile kurudi kwenye chanzo!!!

Suala la maji kutokaa sioni kama ni hoja ya msingi kwa sababu choo ninachotumia ni cha kuchuchumaa na ukingia HUKUTI mjai hata tone kutokana na elevation ambayo fundi aliweka!

Narudia, HUKUTI maji hata tone na ni zaidi ya miaka 7 sasa; ukikuta harufu basi kuna mhuni haja-flash sawasawa!!!

The only problem ya staili hii ni pale mnapokuwa na watu wachafu kwa sababu, ukiweza kulenga, unaweza kusukuma uchafu hata kwa maji yaliyojaa kwenye kikombe cha chai!!

Sasa kwa hapa juu utaamini uchafu umefika mbali lakini kwavile maji yaliyotumika ni kidogo sana, there's no way uchafu huo utaweza kufika mbali kama unavyodhani... kitakachokuwa kimetokea ni kwamba uchafu umesukumwa nje ya upeo wa macho yako but it's still there!!

Na hapo sasa ndipo linakuja suala la harufu!
 
Hizi nyumba za kujenga kimasikini, unajikuta unatumia mafundi wenye uwezo wa kukaririshwa tu, matokeo yake ni gharama mara mbili.

Nyumba mbili nilizowahi kuishi(kupanga) zilisumbua sana kwa hilo tatizo, weka mabomba kila shimo na kwenye vijichemba lakini haikusaidia, maji yanayopaswa kutuama kwenye zile trap, yapo. Nikahama, nikahama na sasa nina shida hiyo tena
Wasiweke zile chemba za nje zile ndo zinahalibu mambo, mbona magorofa hayana hizo chemba, waswahili mmefundishwa na nani kuweka chemba nje kila choo, mimi ziliwekwa bomba kutoka chooni zikaenda kwenye septic moja kwa moja, na hakuna yale mabomba mnayoweka kwenye kila choo yale yanapanda hadi juu ya bati, yale pia yanaleta hewa chafu tu kila kona ya nyumba, bomba la hivyo lipo kwenye septic tank tu, ndo shio linapumulia huko, sijawahi sikia harufu mbaya ndani.
 
Zingatia sana matumizi ya GULLY TRAP kila katika ufungaji wa mabomba kakika nyumba yako iwe kwenye sinki la kunawia, sinki la vyoo, bafuni maji ya kuoga ma katika choo, usipo weka GULLY TRAP utageuza nyumba yako dampo.
1603530069130.png
 

Attachments

  • traps-300x225.jpg
    traps-300x225.jpg
    16.6 KB · Views: 78
Kitaalamu kinyesi huwa kinakua digested na bacteria waliomo kwenye kinyesi chenyew, digestion hii huwa za aina mbili anaerobic na aerobic!Kinachofanya harufu kwenye choo ni baada ya bacteria kuvunja kinyesi bila oxygen(anaerobic) hvyo kufanya uzalishaji wa hewa ya Hydrogen sulphide, hii ndo hewa chafu sasa.

Unapomwaga maji kwenye kinyesi unasaidia kuongeza oxygen kwenye kinyesi hvyo kufanya wale bacteria kuvunja kinyesi (aerobic), hapa hakuna uzalishaji wa hewa chafu.

ukiona harufu kwenye choo chako jua kuna ukosefu wa maji kwenye kinyesi.

Njia za kurekebisha
1.Mwaga maji mengi kila unapotumia choo chako
2.Kipindi cha ujenzi wa pipe za chooni hakikisha slope ya bomba inakua sio kali wala sio ndogo iwe moderate, slope kali ya bomba inafanya maji yaende kwenye shimo kwa haraka huku kukiacha kinyesi kikibaki kwenye bomba,
3.Weka vent pipe kwenye septic tank mana kwenye hili shimo ndo kunapozalishwa hii harufu, hvyo ukieka bomba litasaidia kupeleka harufu hewani,
Kwa msaada wowote unaweza nitafuta Dm tuje tufanye hyo kazi.
Civil engineer
 
Back
Top Bottom