Tatizo la choo katika Ofisi za Forodha zilizopo Mpaka wa Tunduma

wainga

Member
Mar 30, 2017
73
66
Hali ya vyoo katika ofisi za forodha kwa wageni imekuwa tatizo kubwa sana tangu kituo hiki cha pamoja kati ya Tanzania na Zambia kilipofunguliwa.

Imekuwa ni kawaida kufungwa kila mara kwa sababu zisizojulikana hali ambayo inasababisha wageni wanaongia kutoka nchni za Kusini mwa Afrika kupata taabu wanapokuwa wanahitaji huduma hii.

Mpaka sasa choo hiki kimefungwa tangu Marais walipokuja kukifungua tarehe 5/10/2019 mpaka sasa. Tunaomba mamlaka zinazohusika washughulikie hili tatizo haraka iwezekanavyo ili kulinda hadhi ya nchi yetu.

Ni aibu sana mlango mkuu wa nchi kukosa huduma muhimu ya choo.
 
Back
Top Bottom