Tatizo La Ardhi: Wawekezaji Wanaipeleka Hii Nchi Kubaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo La Ardhi: Wawekezaji Wanaipeleka Hii Nchi Kubaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Oct 31, 2011.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Majuzi tu, mtoto wa mkulima, Waziri Mkuu mizengo Pinda alielekea Marekani na kusaini mkataba wa kuwapa wawekezaji mamillioni ya hekari. Leo hii tunaanza kuyaona matatizo ya hawa wawekezaji. Hawa watu wanatuchafulia nchi yetu. Punde tu tutawafukuza wote. soma hii ujionee wawekezaji wanavyojichukulia sheria mikononi mwao na kuanza kukodisha ardhi waliyouziwa.....Kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu

  Serikali yatakiwa kuondoa wawekezaji [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Friday, 28 October 2011 19:38 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Chanzo MWANANCHI

  Esther Mwimbula, Kilosa
  SERIKALI imeombwa kuwakamata na kuwaondoa wawekezaji waliovamia mashamba mbalimbali wilayani Kilosa, mkoani Morogoro, ambao wamebadili matumizi na kukodishia wananchi wengine ambao siyo wakazi wa wilaya hiyo. OfisaTarafa ya Magole, Conradi Mzwalandili, alimweleza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, alipotembelea tarafa hiyo kuwa wilaya hiyo ina mashamba makubwa yenye ardhi yenye rutuba kwa kilimo cha mazao mbalimbali. Hata hivyo, Mzwalandili alisema wawekezaji hao wamewakodishia watu wengine na kuwafanya wakazi wa wilaya hiyo kukosa eneo la kuishi, hali inayowafanya kukumbwa na njaa mara kwa mara.

  Mzwalandili alisema wilaya hiyo ina maeneo yenye rutuba, lakini wakazi wake wana tatizo la ukosefu wa ardhi kwa ajili ya kuendesha kilimo baada ya maeneo makubwa kupewa watu wachache wanaojidai wawekezaji, ambao hawaitumii kama kulingana na walivyoomba. Alisema imefikia wakati wakulima na wafugaji kutengewa maeneo yao ili kuzuia migogoro isiyo ya lazima wilayani humo.Alisema licha ya wakulima kulima maeneo yao, ruzuku ya pembejeo haziwafikii wakulima kwa wakati hivyo kusababisha kuchelewesha maandalizi ya mashamba. Mzwalandili aliendelea kuwa kiasi ambacho wamepangiwa wakulima kutoa ili wapate ruzuku za pembejeo, ni kubwa tofauti na kipato cha wakulima hao.Hivyo aliomba Serikali kupunguza kiwango cha ruzuku za pembejeo na kuwaondoa wawekezaji waliovamia mashamba kwa maslahi binafsi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  serikali ya washenzi unategemea nini?
   
 3. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  I hate CCM...kila chenye mwanzo hakikosi mwisho,time will tell.
   
 4. M

  Moses msisia Member

  #4
  Oct 31, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wengi tunaichukia sana lakini wajinga wanaendelea kuichagua tutafanyaje?
   
 5. M

  Mawazo metusela Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  too bad, but nachoamini Liberation is at the door.........
   
Loading...