Tatizo la ardhi Tanzania litatuleta mfarakano baadaye

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,619
2,567
Ndugu wanaJF, nionavyo mimi tatizo la ardhi litatuletea mfarakano hapa nchini hapo baadaye. Ingawa viongozi wetu wanasema “hakuna nchi iliyoendea bila wawekezaji” lakini nchi zilizoendelea zina sheria nzuri kuhusu ardhi yao. Kama hizo nchi nazo zingegawa ardhi kama viongozi wetu wanvyofanya hapa Tz wasingefikia maendeleo waliyonayo leo hii. Vingozi wetu wanatafuta wawekezaji wa kuja kuwaondoa wananchi kwenye ardhi yao kwa kisingizio cha uwekezaji. Lakini watoto na wajukuu wetu watakapotaka kulima baadaye watapata wapi ardhi? Nahisi watakapokosa ardhi wataanza kuidai kwa nguvu na hapo ndipo matatizo yatakapoanza. Nchi ambazo zimewekeza kwenye kilimo zina utaratibu tofauti na tulio nao sisi. Mfano, katika hizo nchi wawekezaji wachache wamewekeza kwenye kilimo kwa kulisha nchi nzima na hata kusafirisha ziada nje. Lakini utaratibu unaotumika ni tofauti na huu unaotumika hapa kwetu maana huko husikii wananchi wanalalamikia kuondolewa kwenye ardhi yao kwa nguvu bila fidia nzuri au kupewa sehemu nyingine ya kuishi au kulima. Hapa kwetu Tz mwananchi anaondolewa au anazuiwa kuendeleza ardhi yake bila fidia na hivyo kutojua afanye nini. Mpaka aje afidiwe unakuta thamani ya ardhi imeshabadilika. Kweli hali hii ndiyo itakayotuletea maendeleo na ndio aina ya uwezekezaji unaotakiwa ili tuendelee?
 
Magobe,
Hakuna nchi yeyote iliyoendelea kwa kukaribisha wageni kuwalimia. That is a fact. Tungejikita zaidi kuwakaribisha wawekezaji kutusaidia kuanzisha/kufufua viwanda vyetu. Hivi sasa sisi ni wanunuzi tu na hatuna bidhaa tunazouza nje. Dhahabu nayo tumewagawia wawekezaji, inawanufaisha wao zaidi ya inavyoingiza fedha nchini. Hizi sera ni za watu waliofilisika kimawazo kwamba mzungu atakuja akulimie. Huyu atakuja ajilimie, auze mazao yake nje na faida aiweke kwao.
 
Tungejikita zaidi kuwakaribisha wawekezaji kutusaidia kuanzisha/kufufua viwanda vyetu.
Kwa nini hamuwezi kuvianzisha wenyewe?

Na nani aliwaanzishia vile vilivyokuwepo?


Na kwa nini mliua mlivyokuwa navyo?

Na mnatuhakikishiaje sasa hivi mkianzishiwa vingine hamtaviua?

Na unajuaje mkianzishiwa na "mwekezaji" viwanda hivyo vitakuwa vya kwenu?
 
Magobe na Jasusi... tuanze wenyewe kama alivyosema Anheuser!!!I c

an tell you kwamba mimi nimeanza, na in just one year my span has exploded (exponential expansion)... tatizo letu ni kuogopa kuchukua risk.... i am on 300% turn over in just 10 months and this is not a joke

Tuamke na bahati nzuri humu JF kuna wataalam hasa wa ardhi, kilimo na makazi, na wana uzoefu wa ukweli na si nadharia

akina bakhresa wameonyesha kwamba it can be done
 
Hapa wanacho kiandaa ni zaidi ya zimbabwe, jamani hawa viongozi hawa kusoma historia? Viongozi watafakari maana ya uhuru uliopiganiwa!
 
Kwa nini hamuwezi kuvianzisha wenyewe?

Na nani aliwaanzishia vile vilivyokuwepo?


Na kwa nini mliua mlivyokuwa navyo?

Na mnatuhakikishiaje sasa hivi mkianzishiwa vingine hamtaviua?

Na unajuaje mkianzishiwa na "mwekezaji" viwanda hivyo vitakuwa vya kwenu?

Nyerere alikuwa na wazo zuri sana la kuanzisha viwanda. Tulikuwa na viwanda vya nguo, tulikuwa na viwanda vya ngozi. etc. etc. Lakini tulizembea sana katika management. Sasa kwa sababu tumejikita katika siasa za kuamini kuwa wawekezaji ndio wakombozi afadhali basi tuwashirikishe katika ufufuaji wa viwanda , si kwamba tuwaachie wao ndio waamue kama ilivyo sasa kwa mujibu wa sera za CCM.
 
Nyerere alikuwa na wazo zuri sana la kuanzisha viwanda. Tulikuwa na viwanda vya nguo, tulikuwa na viwanda vya ngozi. etc. etc. Lakini tulizembea sana katika management. Sasa kwa sababu tumejikita katika siasa za kuamini kuwa wawekezaji ndio wakombozi afadhali basi tuwashirikishe katika ufufuaji wa viwanda , si kwamba tuwaachie wao ndio waamue kama ilivyo sasa kwa mujibu wa sera za CCM.
Bro, Nyerere alifelishwa, Zimbabwe walifanya tunachofanya sisi sana, tunakaa na kuangalia wazungu wanweka planta, havesta, pipes za irrigation, solar systems, one man managed warehouse system with trade mills, movers and ultra modern in-premise logistics system.. do you know how many people may needed in 200 acres??? 4, to be fair... later tunalalama na kula vibua na mapanki

I want a rather proactive and explosive approach like Kenya.... we grab it ourselves, we unite and farm kwa kutumia hizi exemptions za kodi za vifaa vya kilimo na mikopo... wahindi wanaramba tu ardhi in the name of kilimo kwanza

Take it kwamba una unakopa 10M na mkiwa watatu naweza kulipa hadi eka 200, na ukipanga vizuri unapata returns na pia continuity

It is absurd tunawapokea wageni pale TIC kwa kujipendekeza wakati wengine kwao hata boksi hawawezi kupiga (ni viazi) ila akija m'bongo tunamuangalia juu hadi chini)

as a solution to attitude, we need to have agencies, yes local agencies to run that business and represent locals in investment plans so that we only do what we do
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom