Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
Hello Wajasiriamali,
Jamani kuna utapeli unaoendelea kwa siku ya pili sasa. kuna jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Professor Alexander Moses kutoka marekani ana kampuni inayoitwa Angel Investors for Africa na website ni www.investorsforafrica.com
Jamaa huyu alitoa tangazo kupitia clouds radio wiki iliyopita kwamba wajasiriamali wafike Jengo la LAPF kijitonyama ili kufanyiwa usahili na kupatikana wajasirimali 100 ambao watapelekwa chuo cha Havard Marekani, kupata mafunzo na kukutanishwa na wawekezaji.
Wajasiriamali zaidi ya 300 walipata fursa ya kuhudhuria na baada ya hapo wakapewa namna ya ku apply nafasi hizo. Baada ya kuapply jamaa huyu anawatumia ujumbe anawataka wajasiriamali wampe dola 200 kama visa application fee kupitia account yake personal na malipo hayo yafanyike haraka iwezekanavyo kabla ya jumanne jambo ambalo limewashangaza wengi. Ila cha kushangaza zaidi kijana aliyekuwa anaendesha usajili huo alijitambulisha kama marketing Manager katoka kampuni ya Clouds FM. Awali alitoa namba ya simu ambayo wajasiriamali waliwasiliana nae na kupata maelekezo ya namna ya kufika kwenye usahili ila kwa sasa namba hiyo haipatikani tena.
Clouds Media group walikuwepo na walichukua video mbalimbali siku ya jumamosi katika udahili huo.
Kutokana na kuwa na maswali mengi yanayokosa majibu sahihi hasa kwenye ulipwaji wa hizo hela dola 200 tunatoa tahadhari kwa mjasiriamali yeyote asije kutuma idea yake au hela kupitia mtandao huo hadi utakapojiridhisha.