Tatizo la ajira Tanzania sio kubwa ila wanohusika na wizara ndio wanalifanya lionekane kubwa

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau!

Nimewaza sana baada ya kutangazwa zile ajira elfu tisa na za walimu na kada ya afya huku waliotuma maombi ni zaidi ya 80,000 inatia kinyaa sana kuona ajira elfu tisa tu zinajadiliwa mpaka bungeni.

Nilikuwa na mapendekezo kwamba ili tatizo la ajira linachagizwa na mambo mengi ambayo moja kwa moja wizara inahusika. Kama wataamua kufuata mapendekezo haya basi vilio vitapungua.

1. Kuwepo ukweli na uwazi katika mfumo wa kuajiri, wakurugenzi wanaingilia sana hii mifumo yetu kwa kutumia madaraka waliyonayo vibaya kila ajira zinapotangazwa hawa ndio watu ambao wakidhibitiwa wasilete undugu au rushwa kwenye mchakato wa kuajiri tatizo litapungua (hapa watoto wa mjini tunaita connection).

Maana wapo wanao apply online lakini wapo wanaopeleka barua kwa mkono kwa sababu mahususi lakini huku kwenye barua za mkono ndio kwenye loop hole.

2. Watu wa TEHAMA wa wizara wanatakiwa kuwa wabunifu katika kutengemeza mifumo ya mtandao ambayo mizuri na bora, haiwezekani mtu ana apply kazi online siku tatu haujakamilisha mfumo unakataa ku appload au ku change taarifa.Kwenye mfumo naomba niende mbali niseme kwamba wanatakiwa kuwa na mfumo ambao mtu atafanya application kwa urahisi bila shuluba pia mfumo ambao utakuwa na uwezo wa kufanya screening na kutambua watu wenye vigezo na wasio na vigezo.

3. Lazima kuwe na data base ya wahitimu wa kila mwaka ambao hawana kazi ambao watafanyia pymetric test na system na interview na taarifa zao kutunzwa inapofika swala la ajira mpya serikali inaingia kwenye data base tu na kuchagua.

4. Wale waliohitimu miaka mingi wapewe vipaumbele selection ifanye kwa kutumia data base ya wahitimu walioanya pymetric test na interview.

5. Serikali iangalie hawa wanaojiita recruitment agents ikae nao waangalie njia gani bora ya kufanya nao kazi na kuwaondoa wale agents wababaishaji wanafanya swal la ajira liwe gumu sana.

6. Serikali iweke sera nzuri ya internship program waweke masharti kwa viwanda na makampuni kila mwaka wawe wanafanya recruitment kupitia intern pia sera inatakiwa kufanyiwa ufuatiliaji wale wasiotekeleza wawe wanachukuliwa hatua.

7. Utaratibu huu wa kujitolea una mapungufu mengi pia ni kichaka cha rushwa na rushwa ya ngono, mabadiliko yafanyike wizara inatakiwa ndio iwe inatoa barua na kupangia watu nafasi za kujitolea kama bodi ya wahandisi kwenye ile program yake ya SEAP inavyofanya yaani mtu apangiwe na wizara shule ya kwenda kujitolea harafu akimaliza aajiriwe sio huu utaratibu wa sasa ni wa hovyo sana unaongeza tu rushwa na malalamiko.

8. Lazima wizara ishirikiane na uhamiaji kuangalia wale wageni walioajiriwa kinyume na sheria za nchi na wasio na vibali vya kufanya kazi, lazima tulinde watu wetu lasivyo yanaweza kutikea kama yale ya SA maana vijana ni jeshi kubwa hivyo tusijidanganye kwamba uvumilivu wao utaendelea kuwa hivi hivi miaka yote.
 
Kweli hzo hoja zinaweza kusaidia angalao wawe na longterm plan na short term plan lakusadia wahanga wa ss na wanakuja mtaan baada ya kumaliza.

Serikali wanayo internship program inayotolewa na taesa ila haijulikani na watu. Wala yenyew sijue hata inaendeshwa kwakujuana viongozi sijue n hawana mawazo mapya.
 
kweli hzo hoja zinaweza kusaidia angalao wawe na longterm plan na short term plan lakusadia wahanga wa ss na wanakuja mtaan baada ya kumaliza.
serikali wanayo internship program inayotolewa na taesa ila haijulikani na watu. wala yenyew sijue hata inaendeshwa kwakujuana viongozi sijue n hawana mawazo mapya.
Tamisemi nao wanatakiwa kuwa nayo maana ni taasisi inayojitegemea kwenye kuajiri.
 
Back
Top Bottom