Tatizo la Ajira kwa Wazawa na alichokisema NW Makongoro Mahanga.

Ryaro wa Ryaro

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
2,661
Points
1,225

Ryaro wa Ryaro

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2010
2,661 1,225
Naibu Waziri Makongoro Mahanga ametoa majibu kisiasa Zaidi kuhusu swala nyeti la ajira kwa Wazawa, alichojibu bungeni leo asubuhi siyo uhalisia wa swala la ajira za wazawa zinazofanywa na wageni.

Tatizo hili ni Sugu na serikali yetu ni vema ikiri kushindwa kulinda ajira kwa wazawa; Yalikuwa ni maswali magumu toka kwa yule mbuge na majibu yake yamekuwa mepesi/mepesi na rahisi/ rahisi kama alivyolisema naibu waziri ( Mahanga).


Wageni ( expriates) wengi wanaokuja nchini siyo tu hawana ujuzi wa kazi wanazozikuta TZ bali pia wengi utoka makwao hawajui watakuja kufanya kazi gani.
Wageni Wengine wanaingia nchini kwa ujanja ujanja wakijifanya watalii, na siku zao zikiisha wanajichimbia kwenye migodi na kwenye makampuni ya uchimbaji mafuta na gesi wakisubiria mtanzania atimuliwe kwa fitina ili wao washike nafasi hizo.


Tunajua wageni wengi (inpersonal) hawaendi kuomba vibari vya kuishi wala kufanya kazi nchini bali wanawatumia watumishi wa mamlaka husika kuwapatia vibari hivyo, Pesa zao wanasema ndio kibari cha kazi. Wengine hawajawahi hata kufika ofisi za mamlaka husika. wanachokifanya wageni ni kutoa mshiko na watanzania wenye njaa wanafanya kazi.


Succession plan aliyoisema naibu waziri ni usanii mtupu na hakuna effort yoyote ya kuimplement kitu hicho, Hakuna mentoring wanayowafanyia kwa wazawa kwani wengi wa wageni hawawezi kazi; na badala yake ni kuwafrastrate wazawa ili wao ( wageni) waendelee kuzikalia nafasi ambazo hakuna umuhimu wa wao kuzifanya.


Mfano mzuri ni kuona mgeni anapewa kazi ya Kuendesha fire track au gari la kuzoa taka/ sewage track eti anajinasibu ni expart na analipwa madola kibao.

Unaona eti mgeni anafanya kazi za ulizi na kuwasearch wazawa magetini???; wageni wegine kufanya kazi (shell) zajaza mafuta kwenye magari, wengine kugawa chakula kwenye mess za makampuni husika.


La ajabu ni kwamba mgeni awa hawafanyi idara maalum (hawako specific & professional), kwamfano Kaburu toka SA anakuja idara fulani let say engineering lakini ndani ya miezi miwili umeamia Jikoni ( mgawa chakula) na baada ya muda yupo IT hivyo hivyo mwisho wa siku yupo idara ya ulinzi.

Hizi zote ni dalili kwamba wageni wengi wanakuja kufanya kazi wasizokuwa nazo utaalam, ni waganga njaa kwa lugha rahisi, na TZ imekubali kuwahifadhi kwa ajiri rangi zao nyeupe.

Makanjanja hawa wa kigeni ni wengi sana Migodini na mara nyingine wanafanya kazi nyakati za usiku ili kujificha kukwepa mkono wa mamlaka husika.
Je mikataba yao toka huko makwao waliambiwa baada ya kuingia TZ watafanya kazi kila idara???; Mkataba kwa kawaida lazima unaonyesha toka mwazo kazi ambazo mgeni anakuja kuzifanya nchi ya ugenini.

Ushauri: Serikali sikivu ya CCM kupitia wizara ya Kazi na ajira/ Idara ya uhamiaji wakishirikiana na Police na Usalama wa Taifa ni vema ukafanya uhakiki wa wageni wanaofanya kazi hasa kwenye Makampuni ya nishati na madini ili kuokoa ajira za Wazawa ( na huu ndio uzalendo).

Kila Mgeni anayefanya kazi hapa nchini aonyeshe aliingia lini na kama ana Zaidi ya miaka miwili aeleze nini amekifanya kwenye succession plan ambayo ni sehemu ya mkataba wake; na kama akufanya mentoring kwa ajiri ya succession plan kwa nini asiondoke kwa kosa la kukiuka mkataba.


Mwisho: Serikali ya CCM itamke na isimamie kwa vitendo, kwamba mgeni aruhusiwe kufanyakazi nchini Iwapo tu Hakuna Mzawa anayeweza kuifanya kazi hiyo; Na kama itatokea mgeni amefanya kazi serikali impe muda maalumu let say 6-12 months yaku m-mentor Mzawa kwa ajiri ya Kuifanya kazi hiyo na yeye (mgeni) aondoke mara moja.

Uzalendo ni Kulinda ajira kwa Wazawa: Ni aibu wageni kufanya kazi za kugawa chakula, kunywesha magari mafuta na hata kazi za Kiulinzi; tukiwa kama taifa huru lenye umri wa miaka Zaidi ya hamsini lazima Tujitambue.

Asanteni.
 

Emma Lukosi

Verified Member
Joined
Jul 22, 2009
Messages
929
Points
195

Emma Lukosi

Verified Member
Joined Jul 22, 2009
929 195
Tukiachana na kutokua na ujuzi Wengi wao ni local criminals na CIA spies...

Ma Expert walio wengi hawezi ku prefer kuja kwenye nchi za ulimwengu wa tatu kama tz..
 

Forum statistics

Threads 1,390,917
Members 528,291
Posts 34,066,493
Top