Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Serikali ya Nigeria imewaondoa wafanyakazi hewa 23846 kutoka kwenye orodha ya wafanyakazi wote wanaotambuliwa kisheria. Nigeria inao wafanyakazi wa serikali ambao ni milioni 1.2, inasemekana kuwa asilimia 7.6 ya idadi ya waajiriwa wote wa serikali wana uhusiano na ajira hewa, kwa maana ya majina ya marehemu kutumika, pamoja na majina ya bandia kutumiwa na baadhi ya wafanyakazi wenye vyeo vya juu wasiokuwa waaminifu.
Jana rais wetu kasema kuwa mpaka sasa wameshagunduliwa wafanyakazi 1681 na ukaguzi wa kina bado unaendelea. Hapa tunaziongelea nchi mbili tu za Afrika, yaani Nigeria na Tanzania, hatujaongelea madudu mengine mengi tu katika nchi zote za Afrika.
Tatizo la Afrika haliwezi kuwa ardhini, chini ya huu udongo tunaokunyaga kila siku, kuna mali nyingi sana tena zenye thamani kubwa sana. Kuna gesi ambayo haijaguswa, kuna madini ambayo hayajachimbwa bado.
Ukiangalia jinsi ambavyo mashirika mengi tuliyokuwa nayo yalivyokufa na ukatazama jinsi ambavyo mashirika kama hayo yetu ya nchi nyingine za Afrika yanavyokufa, huwezi kuona tofauti kubwa.
Ardhini Mungu alitujaalia neema nyingi sana, lakini vichwani....Mmmmh