Tatizo kubwa sio anakozipata, bali anakozipeleka Bil 240 RA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo kubwa sio anakozipata, bali anakozipeleka Bil 240 RA

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Tuko, Apr 21, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Alishawahi kusema mwenyewe na jana Dr Slaa kakumbushia kuwa RA ana kipato cha zaidi ya Tsh Billion 240 kwa mwaka!Hii ina maana kuwa RA anaingiza faida ya zaidi wa Tsh million 657 kwa siku!

  Naomba kuuliza hizi fedha anazipeleka wapi? RA na mabilionea wengine hata Tanzania, fedha zao wanapeleka wapi? Sijawahi kusikia RA kafadhili kitu chochote kikubwa katika jamii ya Watanzania. Ukiacha vimichango vidogo kama million 3 alizowahi kumpa Mtikila, na kwingineko, RA anapeleka wapi fedha zake? RA ana charity fund/foundation yoyote Tanzania?. Tunasikia mabilionea wa nchi nyingine wanachangia kujenga mahospitali, wanatoa mahela mengi kwenye taasisi za utafiti n.k. (eg Bill and Melinda Gates foundation). Mabilionea wa Kitanzania kama RA, hela zao zinaenda wapi?

  Tukisema kuwa zinafadhili ugaidi duniani, au zinafadhili vita sehemu fulani, au zinaendesha serikali kandamizi sehemu fulani, au ziantumika hapa hapa kufadhili makundi, njama na mipango hatarishi kwa maslahi ya watu fulani, tutakuwa tunakosea? Hivi si kuna FBI na sheria ya ugaidi ilishapitishwa Tz? Kama vyombo vyetu vya usalama haviwezi kufuatilia mambo kama haya, kwa nini hivi vya kimataifa visiingilie na kuhakikisha fedha hizi hazihatarishi usalama wa dunia?
   
 2. U

  Uswe JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tuanze na heading yako mkuu, anakozipata ni TATIZO KUBWA anakozipeleka ni TATIZO KUBWA ZAIDI!

  Pesa zinazopatikana kifisadi zitatumika kulinda maslahi na usalama wa fisadi, kama asipotumia pesa hizo kujilinda sasa hivi angekua segerea. Huwezi kumuongelea Bill gates na Rostam katika sentensi moja, RA ni fisadi mkubwa, Bill Gates ni mfanyabiashara mkubwa hatutegemei watumie pesa yao kwa namna zinazoshahabiana
   
 3. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,948
  Likes Received: 1,501
  Trophy Points: 280
  Na pamoja na kuwa RA amekuwa tajiri kwa muda mrefu lakini hasa ameanza kuvuna mapesa kuanzia mukulu alipokamata dola ,ndipo jamaa kajitanua kwelikweli biashara zake zimesambaa hadi nje ya nchi
   
 4. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ni kweli Mkuu. Nadhani unajua kuwa kwa taratibu za kibenki siku hizi (sina uhakika kama ni sheria), zikiingizwa fedha nyingi (sijui kuanzia tsh ngapi, but najua hata tsh 50,000,000) kwenye akaunti yako kutoka nje, huruhusiwi kuzichukua hadi ueleze zimetoka kwa nani na za nini.

  Sidhani kama fedha zote za RA zinatumika kumlinda kwa ufisadi wake. Bil 240 ni nyingi, lazima kuna sehemu nyingine zinaenda. Hata hivyo sawa, kama zinatumika kumlinda, huoni kama hapo ndipo starting point ya kuangalia ufisadi wake anafanya na analindwa na akina nani?
   
 5. U

  Uswe JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kulinda ufisadi ni gharama kubwa, kumbuka ni kitu kinaendelea na unatakiwa uwe na vyanzo vya mapato, kwa hiyo wakati nyingine zinatumika kumlinda nyingine lazima zitumike kuendeleza biashara zake.

  Ili awe salama lazima anunue vyombo vya habari, vile anavyomiliki moja kwa moja na vile asivyomiliki, lazima awe na watu wa kumpa taarifa na kufanya umafia (rejea ile story ya mwanahalisi kwamba walitaka kum-eliminate mwakyembe, slaa na wengine) ku arrange umafia kama ule ni gharama kubwa, kumbuka hii si one time issue, ni kitu kinaendelea, kwenye maisha yake yote kuna watu wanafanya kazi ya kusaka wabaya wake na kuwaondosha, this is no something cheap! RA anaendesha nchi kwa remote, anaweka anaowataka na kuondoa asiowapenda, rejea zile bilioni nane za kumsafisha EL, na hizi ni zile zinavuja kwetu bado kuna mambo mengi ambayo si hatuyajui, yote haya yanahitaji pesa nyingi

  Lazima pia atakua na pesa nyingi benki ndani na nje.
   
Loading...