Tatizo kubwa linaloturudisha nyuma sio kukosa akili bali UJASIRI

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Ukweli ni kwamba raia wengi ni waoga mno karibia kwenye kutenda kila kitu.
• Madereva ni waoga (uzoefu wangu barabarani unaonyesha wengi wakimuona traffic police wanafunga breki hata kama hawana kosa,wanaogopa kujieleza,wanaogopa korti)

• Vijana wengi kwenye usaili ni waoga mnoo ( nimebahatika kuwa ktk 8 job interview panels haki ya nani wasailiwa naweza sema 90% huwa ni waoga mnoo na wanatetemeka na kutweta mno hata pale wanapojua ingawa wana qualifications nzuri tu.)

• Umahiri wa lugha ya Taifa... ukifuatilia kwa kina utagundua vijana wengi hawawezi kujieleza sawasawa kwa lugha fasaha kutokana na uoga na si kutoelewa....wengi hushindwa hata kutofautisha herufi 'r' na 'l' sio kwa sababu hawajui hasha! bali uoga...aidha lugha ya kigeni wengi hushindwa kwa sababu ya uoga...mbona wengi huandika vizuri tu kizungu.

• Malezi yamechangia....watanzania wengi tumelelewa ktk familia za kawaida (humble life) na kwa sababu ya influence ya wanasiasa na siasa kwamba wanatuamulia mambo mengi huko vijijini wazazi wetu wamekuwa wakifahamu kutii tu na kuhoji kidogo sana,desturi ambayo imejenga mazoea na hatimae kuwa uoga,ambao umeambukizwa kwa vizazi.

• Kuiga sana tamaduni za nje...kumetuondolea ujasiri na kudhani kila kizuri hutoka nje...ndio sababu kuna code mixing sana kwenye uzungumzaji wa vijana walopata kaelimu kidogo...kijana asipofanya kama wa nje hajioni mkamilifu,matokeo yake anapofeli ujasiri humuondoka.

• Siasa...imeathiri uwezo wa maamuzi binafsi hatimae kukosa ujasiri.

• Kukosa elimu. Elimu inasaidia kuongeza kiwango cha ujasiri lakini ikiwa aliefunzwa kaipata vema formal na informal yaani ile ya kuishi na ya shule.

• Usafi na unadhifu....kwa kweli watanzania wengi wanaitwa 'wavuja jasho' sawa! Lakini bado hata pale wasipovuja jasho wengi elimu ya usafi binafsi bado ni changamoto....mathalani usafi wa kinywa ni tatizo kubwa kwa vijana wengi....huwezi kuzungumza nae usigeuze sura maana harufu inayotoka hapo ni CO2 plus monoxide...kutokuwa msafi huondoa ujasiri matokeo yake mtu hushindwa kujamiiana na matokeo yake ni ujasiri wake kushuka na kushuka na kushuka.

Suluhu yake ni kinyume cha hayo...

Happy new year 2019 mwana JF.

Endelea kuongeza mdau ili hili suala lishuke tujenge jamii inayojiamini hapa inchini Tanzania...



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye usafi ni balaa,.vijana wengi midomo yao michafu kuanzia maneno hadi harufu,.na kama mdomo unanuka bila shaka sehemu zingine zitakuwa zinanuka pia,.
 
Back
Top Bottom