Tatizo kubwa la ukosefu wa ARVs na reagents za kupimia wagonjwa wa UKIMWI: Kulikoni?

kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,021
365
taarifa za uhakika kutoka ndani ya Medical Store Department (MSD), wataalamu wa madawa (wafamasia wa mikoa, wilaya na hospitali) pamoja wale wa maabara inabainisha ukosefu mkubwa wa dawa mbalimbali za ARVs (za kurefusha maisha kwa wagonjwa wa UKIMWI) mfano atripla, nevirapine, pamoja na reagents za kupimia HIV na CD4. mfano ni mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza na Mara, Kagera... ruvuma, Lindi, mtwara, Morogoro
maswali:

  1. Je wizara ya afya imeenda likizo sababu ya uchaguzi
  2. Je fedha za kununulia vitu hivyo imepelekwa uchaguzini?
  3. Je tunakubali ndugu zetu wateseke kwa ajili ya uzembe wa wachache?
Mwisho naomba taasisi inayosimamia masuala ya ukimwi (nadhani NACP na TACAIDS) pamoja Stoo ya kitaifa ya madawa (MSD) na vitengo vingine vya Wizara ya Afya vichukue hatua.. Katibu mkuu wizara ya afya yupo au na yeye yupo kwenye kampeni? Wakurenzi wizara ya afya mpo au na nyie mnagombea ubunge? Jamani tuokoeni....

tujadili
 
taarifa za uhakika kutoka ndani ya Medical Store Department (MSD), wataalamu wa madawa (wafamasia wa mikoa, wilaya na hospitali) pamoja wale wa maabara inabainisha ukosefu mkubwa wa dawa mbalimbali za ARVs (za kurefusha maisha kwa wagonjwa wa UKIMWI) mfano atripla, nevirapine, pamoja na reagents za kupimia HIV na CD4. mfano ni mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza na Mara, Kagera...
maswali:

  1. Je wizara ya afya imeenda likizo sababu ya uchaguzi
  2. Je fedha za kununulia vitu hivyo imepelekwa uchaguzini?
  3. Je tunakubali ndugu zetu wateseke kwa ajili ya uzembe wa wachache?
Mwisho naomba taasisi inayosimamia masuala ya ukimwi (nadhani NACP na TACAIDS) pamoja Stoo ya kitaifa ya madawa (MSD) na vitengo vingine vya Wizara ya Afya vichukue hatua.. Katibu mkuu wizara ya afya yupo au na yeye yupo kwenye kampeni? Wakurenzi wizara ya afya mpo au na nyie mnagombea ubunge? Jamani tuokoeni....

tujadili

Kanyagio,

Je hii haitokani na serikari ya marekani kupunguza misaada ya hizo ARVs? Nasikia tangia Obama aingie serikari ya marekani imepunguza misaada ya hizo dawa hasa afrika,kwa sababu ilielekea ukimwi unachukua resources nyingi huku magonjwa mengine yanayoua zaidi yanasaulika.
 
Tatizo linaweza kuwa sera za obama1
Mkuu usirahisishe mambo hivyo kwani utafanya wanahusika kutokua sirias

Tatizo si pesa, bali tatizo ni watu... na kuna habari zinasema kwamba kuna dawa zilichakachuliwa

naskia hata yale madawa yaliyooza yanatumika na wafanyakazi wa msd kuiba dawa, wanareplace na dawa nzuri kutuzuga, mkuu wao kalala fofofo anafuatilia mademu, na wameunda genge baya sana la kuhuju wagonjwa wa ukimwi
 
Back
Top Bottom