Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Tatizo kubwa la nchi za kiafrika ni kufanya mambo mengi kuwa siri!.Nyaraka nyingi zinazohusu nchi za kiafrika,zinaendelea kufanywa siri,matokeo yake waafrika hujadili na kuchambua mambo hata yanayowahusu kwa kuhisi hisi!.
Mfano leo ukitaka kuipitia zile nyaraka za makinikia za Prof Osoro na Prof Mruma,hutazipata popote,hata kwenye maktaba za vyuo vikuu,taasisi za utafiti,bungeni,kwenye vyombo vya habari huwezi kuzipata!.Zimebaki kuwa siri.
Leo mikataba yote ya madini imeendel...ea kuwa siri,huwezi kuiona popote,uende bungeni,maktaba ya Taifa,vyuo vikuu,kwenye taasisi za utafiti huwezi ona mikataba hiyo!.
Kwa sababu haya mambo yanawahusu watanzania,nadhani yangewekwa hata kwenye wovuti za wizara husika ili wanaotaka kuzisoma kwa undani wazisome kwa undani.
Ndiyo maana hata timu ya wataalamu wetu wanaokwenda kwenye mazungumzo na Accacia bado ni siri,hatujui ni akina nani wanakwenda pambana na mabeberu hawa kutoka Toronto!?
Tujenge utamaduni wa kuwafanya wananchi wayajue mambo yanayowahusu,nakumbuka siku Prof Osoro alipokuwa anasoma ripoti yake ,kama sikosei Mh Rais Magufuli alisema ripoti hizi zichaposhwe mpaka kwenye magazeti ili watanzania waone jinsi wanavyoibiwa,lakini leo nenda kwenye vyumba vya habari,hutakutana na ripoti hizo,nenda kwenye maktaba ya bunge hutakutana na ripoti hizo.
Kwa siku za usoni,ni vizuri mambo yanayowahusu watanzania yajulikane kwa watanzania!.haya mambo ya "Classified information" yamekuwa yanatukwamisha sana!.
Yote katika yote,Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania katika mazungumzo hayo,natumai mtaweka alama kwa vizazi vijavyo.!