Tatizo kubwa la nchi za kiafrika ni kufanya mambo mengi kuwa siri

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,260
2,000
Tatizo kubwa la nchi za kiafrika ni kufanya mambo mengi kuwa siri!.Nyaraka nyingi zinazohusu nchi za kiafrika,zinaendelea kufanywa siri,matokeo yake waafrika hujadili na kuchambua mambo hata yanayowahusu kwa kuhisi hisi!.

Mfano leo ukitaka kuipitia zile nyaraka za makinikia za Prof Osoro na Prof Mruma,hutazipata popote,hata kwenye maktaba za vyuo vikuu,taasisi za utafiti,bungeni,kwenye vyombo vya habari huwezi kuzipata!.Zimebaki kuwa siri.

Leo mikataba yote ya madini imeendel...ea kuwa siri,huwezi kuiona popote,uende bungeni,maktaba ya Taifa,vyuo vikuu,kwenye taasisi za utafiti huwezi ona mikataba hiyo!.

Kwa sababu haya mambo yanawahusu watanzania,nadhani yangewekwa hata kwenye wovuti za wizara husika ili wanaotaka kuzisoma kwa undani wazisome kwa undani.

Ndiyo maana hata timu ya wataalamu wetu wanaokwenda kwenye mazungumzo na Accacia bado ni siri,hatujui ni akina nani wanakwenda pambana na mabeberu hawa kutoka Toronto!?

Tujenge utamaduni wa kuwafanya wananchi wayajue mambo yanayowahusu,nakumbuka siku Prof Osoro alipokuwa anasoma ripoti yake ,kama sikosei Mh Rais Magufuli alisema ripoti hizi zichaposhwe mpaka kwenye magazeti ili watanzania waone jinsi wanavyoibiwa,lakini leo nenda kwenye vyumba vya habari,hutakutana na ripoti hizo,nenda kwenye maktaba ya bunge hutakutana na ripoti hizo.

Kwa siku za usoni,ni vizuri mambo yanayowahusu watanzania yajulikane kwa watanzania!.haya mambo ya "Classified information" yamekuwa yanatukwamisha sana!.

Yote katika yote,Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania katika mazungumzo hayo,natumai mtaweka alama kwa vizazi vijavyo.!
 
Kingdavi.ii

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,181
2,000
Hii ni kweli kabisa, kwa sababu viongozi wengi wabapenda kupewa 10% au share kudogo ya project kama madini, ujenzi mkubwa na tenda za manunuzi ndiyo maana usiri ni mkubwa
Nashauri serikali iliyopo madarakani ipeleke bungeni mikataba yote ili wawakilishi wetu waijadili kwa maslai ya nchi, vinginevyo na wao watakuwa majizi kama watangulizi wao waliyza na ktaifisha mali za nchi kwa bei mbaya

Nb
Tuache kulindana tulinde mali za taifa letu
 
Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
23,314
2,000
Tatizo kubwa la nchi za kiafrika ni kufanya mambo mengi kuwa siri!.Nyaraka nyingi zinazohusu nchi za kiafrika,zinaendelea kufanywa siri,matokeo yake waafrika hujadili na kuchambua mambo hata yanayowahusu kwa kuhisi hisi!.

Mfano leo ukitaka kuipitia zile nyaraka za makinikia za Prof Osoro na Prof Mruma,hutazipata popote,hata kwenye maktaba za vyuo vikuu,taasisi za utafiti,bungeni,kwenye vyombo vya habari huwezi kuzipata!.Zimebaki kuwa siri.

Leo mikataba yote ya madini imeendel...ea kuwa siri,huwezi kuiona popote,uende bungeni,maktaba ya Taifa,vyuo vikuu,kwenye taasisi za utafiti huwezi ona mikataba hiyo!.

Kwa sababu haya mambo yanawahusu watanzania,nadhani yangewekwa hata kwenye wovuti za wizara husika ili wanaotaka kuzisoma kwa undani wazisome kwa undani.

Ndiyo maana hata timu ya wataalamu wetu wanaokwenda kwenye mazungumzo na Accacia bado ni siri,hatujui ni akina nani wanakwenda pambana na mabeberu hawa kutoka Toronto!?

Tujenge utamaduni wa kuwafanya wananchi wayajue mambo yanayowahusu,nakumbuka siku Prof Osoro alipokuwa anasoma ripoti yake ,kama sikosei Mh Rais Magufuli alisema ripoti hizi zichaposhwe mpaka kwenye magazeti ili watanzania waone jinsi wanavyoibiwa,lakini leo nenda kwenye vyumba vya habari,hutakutana na ripoti hizo,nenda kwenye maktaba ya bunge hutakutana na ripoti hizo.

Kwa siku za usoni,ni vizuri mambo yanayowahusu watanzania yajulikane kwa watanzania!.haya mambo ya "Classified information" yamekuwa yanatukwamisha sana!.

Yote katika yote,Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania katika mazungumzo hayo,natumai mtaweka alama kwa vizazi vijavyo.!
Pia kuna usiri mkubwa uliozunguka mkataba wa pango la Ufipa. Unafikiri vikao vya Trump vinafanywa mbele ya kadamnasi?
 
tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,388
2,000
Wazungu huwa wanasema tatizo la Africa ni kuwa huwa katika mambo mengi hatuko well organized.
 
Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
1,967
2,000
Tatizo kubwa la nchi za kiafrika ni kufanya mambo mengi kuwa siri!.Nyaraka nyingi zinazohusu nchi za kiafrika,zinaendelea kufanywa siri,matokeo yake waafrika hujadili na kuchambua mambo hata yanayowahusu kwa kuhisi hisi!.

Mfano leo ukitaka kuipitia zile nyaraka za makinikia za Prof Osoro na Prof Mruma,hutazipata popote,hata kwenye maktaba za vyuo vikuu,taasisi za utafiti,bungeni,kwenye vyombo vya habari huwezi kuzipata!.Zimebaki kuwa siri.

Leo mikataba yote ya madini imeendel...ea kuwa siri,huwezi kuiona popote,uende bungeni,maktaba ya Taifa,vyuo vikuu,kwenye taasisi za utafiti huwezi ona mikataba hiyo!.

Kwa sababu haya mambo yanawahusu watanzania,nadhani yangewekwa hata kwenye wovuti za wizara husika ili wanaotaka kuzisoma kwa undani wazisome kwa undani.

Ndiyo maana hata timu ya wataalamu wetu wanaokwenda kwenye mazungumzo na Accacia bado ni siri,hatujui ni akina nani wanakwenda pambana na mabeberu hawa kutoka Toronto!?

Tujenge utamaduni wa kuwafanya wananchi wayajue mambo yanayowahusu,nakumbuka siku Prof Osoro alipokuwa anasoma ripoti yake ,kama sikosei Mh Rais Magufuli alisema ripoti hizi zichaposhwe mpaka kwenye magazeti ili watanzania waone jinsi wanavyoibiwa,lakini leo nenda kwenye vyumba vya habari,hutakutana na ripoti hizo,nenda kwenye maktaba ya bunge hutakutana na ripoti hizo.

Kwa siku za usoni,ni vizuri mambo yanayowahusu watanzania yajulikane kwa watanzania!.haya mambo ya "Classified information" yamekuwa yanatukwamisha sana!.

Yote katika yote,Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania katika mazungumzo hayo,natumai mtaweka alama kwa vizazi vijavyo.!
Lazima ujue kutofautisha kati ya SIRI na Roho mbaya tatizo letu Africa ni ROHO MBAYA maana kuna vitu sio siri ni roho mbaya tu Kiafrika maana nchi yetu sote madini yetu sote iweje leo kundi fulani tu ndio wawe taarifa zote na kutuabumuria kila kitu juu maisha yetu bila hata kutushirikisha...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oh mara wazungu hawaji, mara sijui nini, na wakija mnaanza oh kwa nini hatushirikiswi. Unataka watanzania millioni hamsini wote waingie kwenye ukumbi wa majadiliano?
 
Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,207
2,000
Oh mara wazungu hawaji, mara sijui nini, na wakija mnaanza oh kwa nini hatushirikiswi. Unataka watanzania millioni hamsini wote waingie kwenye ukumbi wa majadiliano?

Mtandao wa Intaneti umeshaondoa tatizo unalolisema kwa asilimia kubwa tu. Kwani wakati Rais anapokea taarifa za Prof. Ossoro na Prof. Mruma wote tulijazana pale Ikulu?
 
Koplo prof

Senior Member
May 7, 2017
176
250
Tatizo kubwa la nchi za kiafrika ni kufanya mambo mengi kuwa siri!.Nyaraka nyingi zinazohusu nchi za kiafrika,zinaendelea kufanywa siri,matokeo yake waafrika hujadili na kuchambua mambo hata yanayowahusu kwa kuhisi hisi!.

Mfano leo ukitaka kuipitia zile nyaraka za makinikia za Prof Osoro na Prof Mruma,hutazipata popote,hata kwenye maktaba za vyuo vikuu,taasisi za utafiti,bungeni,kwenye vyombo vya habari huwezi kuzipata!.Zimebaki kuwa siri.

Leo mikataba yote ya madini imeendel...ea kuwa siri,huwezi kuiona popote,uende bungeni,maktaba ya Taifa,vyuo vikuu,kwenye taasisi za utafiti huwezi ona mikataba hiyo!.

Kwa sababu haya mambo yanawahusu watanzania,nadhani yangewekwa hata kwenye wovuti za wizara husika ili wanaotaka kuzisoma kwa undani wazisome kwa undani.

Ndiyo maana hata timu ya wataalamu wetu wanaokwenda kwenye mazungumzo na Accacia bado ni siri,hatujui ni akina nani wanakwenda pambana na mabeberu hawa kutoka Toronto!?

Tujenge utamaduni wa kuwafanya wananchi wayajue mambo yanayowahusu,nakumbuka siku Prof Osoro alipokuwa anasoma ripoti yake ,kama sikosei Mh Rais Magufuli alisema ripoti hizi zichaposhwe mpaka kwenye magazeti ili watanzania waone jinsi wanavyoibiwa,lakini leo nenda kwenye vyumba vya habari,hutakutana na ripoti hizo,nenda kwenye maktaba ya bunge hutakutana na ripoti hizo.

Kwa siku za usoni,ni vizuri mambo yanayowahusu watanzania yajulikane kwa watanzania!.haya mambo ya "Classified information" yamekuwa yanatukwamisha sana!.

Yote katika yote,Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania katika mazungumzo hayo,natumai mtaweka alama kwa vizazi vijavyo.!
Ndugu watawala tulio nao sasa hawakulelewa na kufundishwa kuwa wawazi. Toka ukoloni, TANU mpaka sisiem hakukuwa na mada ya uwazi iliyofundishwa kwenye vitabu vyao. Hakuna mentor aliyewahi kufanya hivi kwa warithi wake. Wao walichofundishwa wakafuzu ni kidumu chama chetu. Hata ile topic ya rushwa ni adui wa haki walianza pole pole kuiruka wakawa hawafundishani kabisa mwishowe wakaifuta kabisa wakai-replace na takrima.

Nachotaka ku-draw ni kuwa waasisi wa nchi walikuwa myopic kwenye baadhi ya mambo hasa hili la transparency hawakushughulika nalo kabisa. Sasa sijui hawakuliona na kuona madhara yake au waliliona ila na wao walikuwa wanalichukia wakaamua walichimbie kaburi walizike milele. Hawa wa sasa ni watoto wa wale wa mwanzo kabisa, warithi wa nchi hii toka kwa wakoloni, transparency wanaichukia toka moyoni na ukiidai watakuonyesha cha mtema kuni.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom