Tatizo kubwa la CCM sio upinzania ni sensa! (Watanzania)

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Magufuli ana nia nzuri ya kuweka nchi vizuri lakini tatizo kubwa la viongozi wetu ni kwamba pamoja na kuwa wasomi na kujigamba ya madegree ambayo hayafanyiwi kazi ni ukweli kwamba hawajui kutumia takwimu kujua nchi inaenda wapi na inataka nini. Kama mnakumbuka wakati Magufuli alipoingia madarakani walishangaa jinsi watoto walivyo ongezeka shule sasa tujiulize je walikuwa hawajui sensa na kujua kuna watoto wangapi hawako shule?? nianze na kutoa data za TZ. Namba za makisio kutoka CIA factbook

0-14 years: 43.74% (male 11,921,393/female 11,678,536)

15-24 years: 19.86% (male 5,361,747/female 5,351,794)

25-54 years: 29.88% (male 8,098,183/female 8,020,289)

55-64 years: 3.51% (male 836,313/female 1,055,347)

65 years and over: 3.02% (male 687,118/female 940,215) (2017 est.)

Idadi ya watu ni 54M na walio chini ya miaka 24 ni 34M


63.9% ya Watanzania wapo miaka 24 au chini. Hawa vijana na watoto wamekulia mazingira tofauti sana na nchi yetu inavyoendeshwa. Kwa ufupi watu zaidi ya 63.9% ya Watanzania wamezaliwa kuanzia 1993. Wamezaliwa na mitandao, teknologia, wanajua wenzao nchi nyingine wanafanya nini na pamoja na umasikini wao wanajua shida ni viongozi. Kwa misingi hiyo huwezi kuzuia vyombo vya habari na kufanikiwa au kukataza watu kuongea kwasababu hawa watoto wamezaliwa na kujua kutumia vyombo vya habari na kutumia mitandao huwezi kuwabadilisha maana ndiyo walivyo. Huwezi kulazimisha watu kuwa wengine hivyo jitihada za CCM ya Magufuli ya kufunga vyombo vya habari au kupeleka watu mahakamani kwa kuongea sio tu ni kitu cha ajabu kwa hawa watoto bali hata hawaelewi ina maana gani. Pili hawa vijana wanajali maendeleo sio Chama hivyo CCM inawakati mgumu kwani mfumo wa serikali bado ni wa kizamani sana

Lakini ukiangalia vizuri vijana wengi wanakuja mijini na mijini kutaendelea kuwa kwa upinzani si kwasababu wana solution zaidi bali kwasababu wameweka watu ambao wanafananafanana nao. Ukiangalia miji mingi wabunge wengi ni wadogo, Mayor vijana na hawa wanasikilizwa kuliko Magufuli. Vilevile CCM wameishiwa idea mfano hakuna mabadiliko ya mifumo ya kuomba kazi, hakuna ukuwaji wa kazi za private sector, na hakuna mazingira mazuri ya ufanyaji wa biashara ndogondogo. Hii imeleta maneneo kama "Tanzania bahati mbaya"... hivyo CCM inaweza kuendelea kutawala kwa nguvu lakini wananchi hawatakuwa upande wao mpaka wabadilike kufanana na wakati. Mfano angalia Mayor wa Arusha ambayo analeta maendeleo haraka haraka kwasababu hata .... milolongo ..
 
Back
Top Bottom