Tatizo hili si Francis Ndulane pekee, hata hawa waliwahi kubabaika sana kuapa mbele ya Rais Magufuli. Ndulane apewe nafasi tena aape vizuri!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,126
Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli mimi najua wewe ni jembe kwelikweli na hutaki mchezo katika masuala ya kazi.

Nakuomba Mkuu najua nafasi hizi Mungu ndiye hupanga.

Angalia tena wakati unamwapisha Ndugu Martin Shigela kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, pamoja na Shigela kuwa na Masters ya sheria (LLM) alishindwa kabisa kusoma kiapo. Ni mtendaji mzuri na anachapa kazi kwelikweli!

Mwingine aliyewahi kubabaika sana mbele yako ni Eng. Stella Manyanya wakati akiapa kuwa Naibu Waziri .

Mkuu nakuomba ebu tumia hekima yako Mungu aliyokujalia pamoja na vyombo vyako katika jambo hili.

Kama ulivyosita kutia saini kunyonga wale wafungwa basi ebu sita tena katika maamuzi yako kuhusu Mhe. Francis Ndulane.

Mimi binafsi simjui huyu ndugu Francis Ndulane ila imeniuma sana pale nilipojaribu kuvaa viatu vyake!

Sina ninaloweza kumsaidia zaidi ya kuandika hapa kwenye huu ukurasa basi.

Najua Mwenyezi Mungu hufanya kazi kwa namna ya ajabu pengine huu ujumbe waweza kukufikia. Ahsante.
 
It was fairly short, he could have memorised and sang it from rot. Hata maneno Jamhu Jamhu jamuhuri ya muungano wa Tanzania yalimtatiza. Of course kuna kupanic, tusimhukumu outright but he was given a second chance hado hakuweza. Simpo: aulizwe mwalimu wake wa mwisho IFM
 
Naunga mkono hoja. Endapo itampendeza mh. Rais ajaribu tena kumfikiria huyu mtu kilichokuwa kikimsumbua muda ule sisi sote hatujui ila yeye pekee na Mungu wake.
 
Mikataba inahitaji kutulizana. Hata hivyo, uchunguzi wa sayansi ya saikolojia inabidi kufanywa kujua hasa nini kilimpata ndugu yetu huyu.
 
Kwa nini huo utoto wote ? Uraisi wa JMTZ ni Taasisi na siyo utoto wa cheke chea, Watanzania tunaheshimu Uraisi hatuogoipi mtu aliyekalia kiti cha Uraisi na kuna tofauti hapo, Raisi Magufuli ajitafakari sana aache kudhalilisha watu bila ya sababu tena kwa makusudi kabisa kwani anajua wazi kwamba yuko live na kila mtu anaona na kusikia hiyo ni abuse, mambo mengine anapaswa kuongea na hao wateule wake wakiuwa wao wenyewe.

Say no to abuse, na haijalishi ni Baba yako, Mama yako, Mke wako, Mume wako, usikubali abuse, ...
 
Duuuh huyu ni wewe?
 
Kapiga igizo la nguvu Jiwe, baada ya kuona kachemka kumteua mla rushwa fisadi aliyefukuzwa ukurugenzi na waziri mkuu morogoro ndio akaona aje kumtoa kwa staili hiyo.
 
Back
Top Bottom