Tatizo hili linanikatisha tamaa ya kuishi.. Nisaidieni wana jf wenzangu.

Pretty R.

JF-Expert Member
Apr 14, 2012
200
31
Habari zenu madokta wa jf? Mm nina tatizo la ngozi ambalo linanifanya nikose hamu ya kuishi kwa sababu kila dokta ninayemwendea ananiambia tatizo lake, mwingine ananiambia allerg ya sulphur, mwingine naungua na mionzi ya jua na wengine wananiambia allerg ya vipodozi na sijawahi kutumia cream. Tatizo hili lilinianza nikiwa form six uso ukaanza kuwa mweusi na baadaye ukasambaa mpaka kwenye mikono na shingoni ila sehemu zingine zipo kawaida. Ni mwaka wa 3 sasa nahangaika kwenda hospital bila matokeo yoyote mazuri. I'm frustrated kama kuna mtu anaweza kunisaidia humu jf anisaidie jamani nateseka sn. Asanteni nasubiri michango yenu.
 
pole sana, usifikie kusema umekata tamaa ya kuishi,
soma hiyo link hapo juu unaweza pata msaada.
 
Kuna ugonjwa flani hivi mtu anababuka anakua na ngozi nyeupe ya mabakamabaka ila wewe badala ya kua nyeupe inakua nyeusi,hyo ni allergy(mzio) waone ma-spesholisti watakusaidia! Kwanin ujiue wakati wewe ni Pretty?
 
...Pole sana kwa matatizo yako ya ngozi ila usikate tamaa na kukatisha maisha yako. Jitahidi tu katika kutafuta tiba labda utampata daktari ambaye ataweza kukusaidia.
 
Mimi ushauri wangu naomba uende hospital za rufaa hasa kcmc na hakika tatizo lako litapata ufumbuzi.Pole sana na usikate tamaa
 
Asanteni ndugu zangu kwa ushauri wenu, kwa kweli mnanitia moyo sn, Mungu aendelee kuwabariki. Kwa aliyeuliza naishi wapi nipo dar, kwa aliyenishauri niende KCMC nilishaenda kitengo cha ngozi ila sijapona wala kupata nafuu. Asanteni tupo pamoja.
 
ndugu pole sana kwa matatizo, nakushauri usichoke kuwaona madaktari na pia tafuta tiba za asili maana zingine ni effective kuliko za hospitali halafu uwe unafanya research kutoka kwenye mtandao kuhusu ugonjwa wako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom