Tatizo hili la ulevi hasa wa pombe,Unga na Bangi linaanzaje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo hili la ulevi hasa wa pombe,Unga na Bangi linaanzaje

Discussion in 'JF Doctor' started by Maalim Jumar, Jan 3, 2011.

 1. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Wana JF!
  Heri ya mwaka wa Twenty Eleven.

  Hili jambo la ulevi haswa wa pombe na madawa ya kulevya n.k

  Nimeona kuanzia dini mbali mbali hata serikali wanalipiga vita kwa nguvu zote.

  Ajabu japo baadhi ya Nchi chache duniani wanaona ni jambo la kawaida tu.

  Sasa pamoja na kuona madhara yake...kwa walevi wa pombe..hutokea ikawa sababu ya kuharibika ndoa yake au kusambaratika familia yake..kwa madeni mbali mbali...hata kufukuzea kazi n.k.

  -Wavuta bangi kufanya mambo ya ajabu mitaani hata maofisini n.k

  -Hivi hadi muhusika akaingia katika hivi vishawishi hua analazimishwa na jamaa zake? Au kuna nguvu ziada humzidi?

  - Kuna kijana mmoja kwao wanao uwezo wa mali...ambazo angeweza kusima hadi Phd kwa pesa za kwao...ajabu ni kua ameingia kwenye utumiaji wa Unga...hata form four matokeo si mazuri..akapelekwa akasome japo (IT) na huko imeshindikana...sasa ni nini mambo haya?

  HITIMISHO:
  Tunawasaidiaje waathirika na wale
  E wapo njiani kuingia humu katika utumiaji wa viharibu akili na mambo mengine?
  Au kuna faida ambazo wanazipata kwenye hayo matumizi yz madawa ?

  Nawasilisha nisaidiwe kujua.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hapa ni malezi tu! peer group influence!
   
 3. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo hakuna wakumlaumu?
   
 4. N

  Nonda JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Vijana wengi huanza hayo uliyoyataja kutokana na kupenda kuiga. Kwa mfano wanapotizama filamu za action, za kimafia na kuona matumizi ya vileo na wale watumiaji wanavyoonekana wajanja.

  Pia vigenge,vikundi vya marafiki wanaokuzunguka au unaowahusudu kuwa ni mfano mzuri kwako(peer group influence)

  Pia kwa wakubwa huingia huko kutokana na frustration za maisha ili kupoteza mawazo(kutaka kusahau kwa muda shida walizonazo)
  Wengine ndio huwa wana hela na husema wanataka kustarehe, nao huelekea huko vilabuni kukamata chupa na gilasi.
  Tatizo ni kuwa watu wanapoanza huanza kama utani hivi, wakisahau kuwa vileo huendana na (addiction) Vileo vina kawaida ya kuwa ving'anganizi.Unapovichokoza vinakuganda na inakupa kufanya kazi ya ziada kuvibandua kutoka katika fikra(hamu) na kutoka katika damu yako.
  Vileo vinakujengea utegemezi, kwamba lazima uvipate ndio akili itulie....in the long run vinakuathiri hiyo akili na kukupopotoa, una-loose control ya utashi wako, na vileo huwa vinakuamrisha ukavitafute kokote kule.

  Nani wa kumlaumu? hili ni suali gumu kulijibu
  lakini lawama zianzie kwa mtumiaji mwenyewe, pili wale wanaofanikisha kupatika kwa vileo hivyo.....huenda nitarudi tena kuchangia jinsi ya kugawa lawama ... lakini la msingi ni kuwa kinga ni bora kuliko kutibu! na lawama hazisaidii sana tatizo likishakuwepo.
   
 5. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hakuna njia zozote za kuwasaidia waliokwisha zamia katika ulevi?
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Zipo.
  Mara nyingi njia inayotumika ni kwa wale walikubuhu ni kuwaingiza katika rehabilitation program. Kuwekwa katika jengo, kama gereza-hospitali, ili wanaomsaidia wawe wanamwangalia kwa karibu ,lakini pia ni kumuondolea yale mazingira ya kupata vileo kirahisi.

  Huko anaweza kupewa kileo chake lakini dose inapunguzwa kidogo kidogo hadi anaacha kabisa. Pia huwa anapata ushauri nasaha.
  wengine wanahitaji medication na ushauri nasaha. kwa hiyo inategemea na ukubwa wa tatizo alilonalo huyo mtumiaji.

  Viko vitengo vya kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya. Na huwa na mafaniko hasa mtumiaji anapoamua yeye mwenyewe kutafuta msaada ili aweze kuacha kuliko yule atakayeshurutishwa na jamaa zake.
   
 7. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Huku uswazi hiyo huduma inaweza kuwafikia hawa jamaa?
  Wameathirika kila kitu...uhakika wa kula hawana...matokeo yake wanakaba wenzao...na ndio hao hao utawakuta wakishiriki hivyo vileo!
  Au umasikini wa hizi familia zetu inachangia?
   
Loading...