Tatizo la meno kufa ganzi na chanzo chake

Heshima wakuu,
Mimi ninatatizo la jino moja tu la mbele kupata ganzi ninapokunywa maji
ya baridi au ninapo vuta upepo. Please naomba mwenye ushauri hapa
jamvini anisaidie.

Tumia sensodyne toothpaste apply 2 to 4 times daily.baada ya wiki utapata jibu. EPUKA kunywa vinywaji baridi.
 
Wandugu awali sikua na tatizo hilo lakini kwa sasa kwa mfano nikila kipande kidogo tu cha nanasi basi meno yanashikwa ganzi sana. Nisaidieni wandugu dawa ya kutibu tatizo hili. Nimejaribu dawa ya meno sensodyne lakini hakuna mafanikio.!
 
Habari wakuu.? poleni na majanga na adha ya mvua hapa mjini dar. ni wiki 2 sasa zimepita tangu ning'oe jino 'gego' baada ya kupona ufizi limeenza kujitokeza tatizo la meno kuuma , yanakufa ganzi na kuuma..sasa sijui tatizo ni sindano za ganzi nilizopigwa maaana nilipigwa kama 4-5 ivi.. naombeeni msaada wadau!
 
Huu ni mwezi na nusu sasa na hili tatizo kwa vile nilikuwa safarini nilishindwa kwenda hospital, yalianza meno ya nyuma, wiki hii gafla ya mbele yameanza.Hili tatizo linatokana na nini haswa na lina tiba ?

Nitashukuru saana kupata ushauriwa wakati najianda kesho kwenda kwa dk.
 
Saitoti nikweli sasa wewe kama mtaalamu unatushauri je hili tatizo la kutoka kwa leya ya juu kunaweza kutibika au ndio kuishi kwa mashart.
 
Habari zenu wanajamvi,mnamo mwanzoni mwa mwaka jana nilianza kusumbuliwa na meno na hali ya kuwa na ukakasi kama mtu aliyekula ndizi mbichi au limao mdomoni,yaani kuna wakati nakuta kinywa ni kikavu hata nashindwa kuongea vizuri.Tena siwezi kukaa eneo lenye kelele nahisi meno yanakela kama mtu anaposugua kitu chenye kelele mfano wa bati kwenye sakafu.Naomba nisaidiwe ni nini hii jamani?
 
Dah, pole sana bro.
Nayajua maumivu ya meno, pole tena. Maana yakianza kuuma, unaweza vua hata Nguo ukijua ni nzito.
Nilitibiwa kwa dawa ya kienyeji, dawa ya meno lkn ilipitia sikioni!!!! Siku 2 nilipona kabisa.
Nenda Hospital mapema upate Tiba
 
Nina tatizo kama lako na bado sijapona. Epuka kutumia nguvu wakati unapiga mswaki au epuka kupiga mswaki kwa muda mrefu. Wanagoogle wanasema ukiona umeanza kuhisi ganzi ktk meno ujue kuna layer ya juu kwenye meno umeiondoa, layer ya chini inayobaki ni very sensitive-ndo maana unapata ganzi. Hii sio suluhisho la tatizo, lakin itasaidia kuepuka matatizo zaidi.

Ukipata matibabu nifahamishe inbox.
 
Hata mimi nasumbuliwa meno kufa ganzi, ya kwangu hayajatoboka wala kuoza.

Nimetumia dawa ya meno niliyoambiwa na daktari kwa muda mrefu sasa hamna kitu sijapona.

Nimepakwa floride kwenye meno lakini bado hali ni tete...

Anayejua dawa jamani tusaidieni.
 
Habari zenu wanajamvi,mnamo mwanzoni mwa mwaka jana nilianza kusumbuliwa na meno na hali ya kuwa na ukakasi kama mtu aliyekula ndizi mbichi au limao mdomoni,yaani kuna wakati nakuta kinywa ni kikavu hata nashindwa kuongea vizuri.Tena siwezi kukaa eneo lenye kelele nahisi meno yanakela kama mtu anaposugua kitu chenye kelele mfano wa bati kwenye sakafu.Naomba nisaidiwe ni nini hii jamani?
Acha kutumia Whitedent, tumia Colgate utapona
 
nipigie nkupe formula ya kutengeneza dawa ya kienyeji
Dah, pole sana bro.
Nayajua maumivu ya meno, pole tena. Maana yakianza kuuma, unaweza vua hata Nguo ukijua ni nzito.
Nilitibiwa kwa dawa ya kienyeji, dawa ya meno lkn ilipitia sikioni!!!! Siku 2 nilipona kabisa.
Nenda Hospital mapema upate Tiba
Ni ipi hiyo dawa,iweke hapa isaidie wengi ndugu.
 
Back
Top Bottom