Tatizo CHADEMA ni Uenyekiti: Kweli Humweka Mtu Huru!

Mwenye kauli katika chadema ni mmoja tu. Godfather Mtei, wengine wote wanatumwa tu.

Labda Ndesamburo kidooogo anaweza kusikilizwa lakini nae anamuogopa Mtei asije akatengwa, kwani Mtei ana mtandao mkubwa zaidi.

chadema inamilikiwa na "organized family gang" kama zilivyo koo za kisisili (Sicily). Mpaka ije koo nyingine yenye nguvu zaidi ya hii ya sasa au afe Godfather, hamtaona mabadiliko. Ya Chacha Wangwe mmesha yasahau?
 
Mkuu, kwa kuwa muaminifu, nimetumia muda mwingi na njia mbali mbali kulipata kosa la Zitto ka kusema kweli mpaka sasa sijaliona.Ninachokiona ni shutuma zinazoanzia hewani hewani.Wanaozianzisha nimejaribu bara kadhaa kuwaomba watoe vielelezo vya kuaminika vya kuthibitisha shutuma hizo mpaka leo hakuna alietoa zaidi yakuendelea kusisitiza "mnafiki", "anaringa" "msaliti" "anapenda sifa" "ana dharau" "amepewa hela na CCM" "KALALA HOTELINI" N.K. naomba kwama wewe unajua kosa lake objectively na una ushahidi wa kitaalam unaothibitika, basi uliweke hapa na tutamsinikiza objectively, aombe msamaha.
Umemtaka Mbowe aombe radhi kwa kosa gani?
Umemtaka Kileo aombe radhi kwa kosa gani? Yeye alichofanya ni kuweka waraka kwenye blog yake , sasa hilo ni kosa? Mbona Jf uliwekwa ? Huwa ambo wagombea radhi? Au ndio double standards ?
Zitto, alisema ataenda mahakamani kuwashitaki waliomchafua , mbona haja ends mpaka leo? Akajisafishe kaa alichafuliwa na sio kama unavyotaka wewe mkuu..
 
Umemtaka Mbowe aombe radhi kwa kosa gani?
Mbowe ndie mwenyekiti wa chama,mbowe anaona viongozi mbali mbali wakimtukana na kumchafua zitto hadharani na hajachukuwa hatua yeyote
Umemtaka Kileo aombe radhi kwa kosa gani? Yeye alichofanya ni kuweka waraka kwenye blog yake , sasa hilo ni kosa?
Mkuu, ikiwe ulipewa habari inayomchafua mtu kutoa chanzo fulani, ukaamini kwamba ni ya ukweli ukaitoa kwenye media yako, baadae ukagundua habari ilikuwa ni yauongo na aliekupa kakudaganya, ni busara kumuomba radhi yule ambaye umerusha raarifa yake na sasa umegundua haikuwa sawa.Akiona kama pendekezo langu hajalielewa nibora akauliza yeye mwenyewe.

Zitto, alisema ataenda mahakamani kuwashitaki waliomchafua , mbona haja ends mpaka leo?
Mkuu, tunaamini kwamba hatuwezi kutumia busara mpaka kwa nguvu za mahakama? kwa mfano kutukana ni kosa la jinai.Hivi kwa mfano wewe kwa busara zako ikitokea ukigundua umetukana mtu, huombi radhi mpaka itoke amri ya mahakama? fiki mara mbili ndugu.
Akajisafishe kaa alichafuliwa na sio kama unavyotaka wewe mkuu..
Kwa hiyo wewe unapendekeza ni bora tuwe tunafanya siasa za kuchafuana na kujisafisha! badala ya kufanya siasa za kuonesha watanzania njia nzuri na yenye manufaa?
 
mbowe anaroho mbaya sana kamwandama zitto mpaka basi wakati anadai demokrasia ndani ya chama.
 
Kwa mnaodhani CHADEMA itayumba eti kisa ZZK katimuliwa, hamko seriazi.
Mkuu kwa hili tunachoangalia sana sana hapa si matokeo.Tunachoangalia ni sababu.Matokeo yeyote yanayokuja kutokana na mchakato usio wa kiadilifu ni tatizo kubwa sana kwa kweli.Ni sawa na ni kuambie tuue mtu mmoja maana kwa kufanya hivyo tutapata mafanikio makubwa sana. Je! utaniunga mkono?
Jamaa ataondolewa,
ni sawa na mtu analalamika hana kosa wewe unasisitiza atapigwa tu lazma! anaweza akapigwa kweli lakini kupigwa huko hakumaanishi kwamba sasa ndio haki na uadilifu itakuwa imefanyika
watapika propaganda kama wafanyavyo sasa kuhusu matamko n.k.
mkuu, miongoni mwa msingi mkubwa kabisa wa propaganda ambao ni universaly applied, nimtu kufanya jambo na kumsingizia mwezake ndio kafanya.Kuna watu wanatukana wenzao wakimaliza wanadai wao ndio wametukanwa n.k. uzuri ni kwamba jamii inaona kwa hiyo kwa mwenye busara ni bora akafikiri mara mbili.

Bado CHADEMA itakuwa imara zaidi na zaidi.
ni kweli ila hii haisababishi sehemu zenye makosa kuachwa hivyo hivyo, au kueleleza makosa kwa hoja kuwa chama ni imara.

Propaganda hazitaishinda kweli.
Propaganda zikifanywa kwa umahiri mkubwa na kwa umakini zinawezakuuficha ukweli hasa kwa jamii ya watu wasiotafakari mambo kwa kina kabla la kuamua.
 
Mbowe ndie mwenyekiti wa chama,mbowe anaona viongozi mbali mbali wakimtukana na kumchafua zitto hadharani na hajachukuwa hatua yeyote
Mkuu, ikiwe ulipewa habari inayomchafua mtu kutoa chanzo fulani, ukaamini kwamba ni ya ukweli ukaitoa kwenye media yako, baadae ukagundua habari ilikuwa ni yauongo na aliekupa kakudaganya, ni busara kumuomba radhi yule ambaye umerusha raarifa yake na sasa umegundua haikuwa sawa.Akiona kama pendekezo langu hajalielewa nibora akauliza yeye mwenyewe.

Mkuu, tunaamini kwamba hatuwezi kutumia busara mpaka kwa nguvu za mahakama? kwa mfano kutukana ni kosa la jinai.Hivi kwa mfano wewe kwa busara zako ikitokea ukigundua umetukana mtu, huombi radhi mpaka itoke amri ya mahakama? fiki mara mbili ndugu.Kwa hiyo wewe unapendekeza ni bora tuwe tunafanya siasa za kuchafuana na kujisafisha! badala ya kufanya siasa za kuonesha watanzania njia nzuri na yenye manufaa?

Kama unamtaka Mbowe aombe radhi kwa sababu tu ameona watu wanachafuana kwenye mitandao, na yeye hakuchukua hatua, nafikiri humtendei haki , na nikuulize swali hivi ni viongozi wangapi wa Chadema wamekuwa wakichafuliwa kwenye mitandao , mbona haujawahi kuchukua hatua hii unayochukua leo?

Kuhusu Zitto na mahakama , yeye ndio alimwandikia barua katibu mkuu wake kuwa anataka kuchukua hatua za kisheria kwa kuchafuliwa , haja chukua hatua , hivi unalisemeaje jambo hili?
 
Huyu mwanzisha mada nilikuwa nafatilia taratibu kila hatua ya thread na post zake.Nimepata picha kamili.
 
Kwa atakaye kuwa na swali lolote aniulize .safari hii nitamjibu hapa hapa na kwa uwazi kabisa.Kwa hali ilivyo kwa sasa, hii ndio itakuwa njia bora kabisa!

Ndugu zangu,kwanza nawasalimu sana!

Kwa kipindi sasa nimekuwa nikijaribu kusisitiza kuridhiana na kurudisha uhusiano mwema miongoni mwa wanachadema kwa kukwepa kueleza wazi wazi kile kinachotokea dhani ya chama nikiamini kwamba wahusika wangenielewa na kuchukua hatua za haraka kwa kuwa wanaelewa vizuri kile wanachokifanya. Kwa bahati mbaya ni kwamba inaonekana jitihada hizo zimekwama na bado baadhi ya viongozi wa chama wanaendelea kuzunguka huku na kule wakifitinisha wanachama wenzao na wananchi. Hali hii ya uchonganishi naona sasa imefikia hatua mbaya kiasi kwamba naona hamna haja ya kuendelea kufichaficha mambo!.

Kwa mfano, Kufuatia hotuba aliyoitoa Mchungaji Msigwa huko Arusha 04/12/2013, ilikuwa kwa kiwango kikubwa imejaa uchonganishi na uchochezi miongoni mwa wanachama kufikia kiasi cha msikilizaji mmoja ndugu Exaud Mamuya kusema “ kutokana na speech ya Mh Msigwa, Zitto angetokea bahati mbaya angegombaniwa na kuraluliwa kama Simba aonavyo kitoweo.” Katika mazingira haya naomba sasa niwe muwazi zaidi kidogo.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,

Tatizo la msingi kwa sasa ndani ya CHADEMA, ni "u-mwenyekiti".Hizi mbio tunazoziona mitaani kwa sasa, na kurushiwa maneno kwa ndugu Zitto,ni matokeo tu lakini suala la msingi ni "u-mwenyekiti "ndugu zangu.Tatizo la msingi ni Zitto kuonekana anaonesha dalili za kugombea uenyekiti na kuonekana ana ushawishi ndani na nje ya chama hivyo asipochafuliwa na kufitinishwa haraka, anaweza akashinda uenyekiti kweli.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,

Imeonekana kwamba kutokana na umaarufu wa Zitto kutokana na mambo aliyokifanyia Chama na taifa kwa ujumla ukichanganya na uwezo wake binafsi, si rahisi kwa mtu mmoja kumchafua na akachafuka bali hilo linaweza kufanyika kwa ufanisi kwa kuunda kundi kubwa na ikiwezekana kuishawishi kamati kuu kufanya mchezo huo wa hatari, wakufedhehesha, na kukatisha tamaa kabisa; mchezo ambao ni dhambi kumbwa sana.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,

Kitu kinachofanyika kwa sasa, licha ya kwamba ni dhambi na udhalimu mkuu, kinasababisha wananchi kugawanyika makundi makundi bila sababu ya msingi. Kadhalika kunasababisha wote tuonekane kama watu ambao tunalenga kupigania vyeo na maslahi tu na tusio kuwa na maono wala uadilifu wa kiuongozi hali hiyo hutufanya tuonekane tuko radhi hata kumtoa mtu muhanga kwa dhuluma ili tufikie lengo..Hali hiyo haiwezi kuwa na manufaa kwetu binafsi, kwa chama wala kwa taifa letu.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,
Hatuwezi kuwa vionzi bora wala hatuwezi kupewa madaraka ya kuongoza nchi hii kwa kufanyiana hila, uzushi, fitna majungu na kuchonganishana wenyewe kwa wenyewe.

Ndugu wana CHADEMA, wenzangu,

Wakati wote tumekuwa tukimlaumu na kumkemea Naibu Katibu mkuu wa CCM, ndugu Mwigulu Nchemba kwa kufanya siasa chafu za fitna na kugombanisha watu. Sasa na sisi tunafanya nini sasa? Tunafanya nini sasa?tunafanya nini ndugu zangu!

MSIMAMO WANGU.

Mimi tangu nilipopata akili, nilijiapiza na nikamuomba mungu anisaidie kwenye mambo kadhaa!.

1.Nilijiapiza kujiepusha kwa uwezo na maarifa yangu yote kumdhulumu mtu yeyote kwa sababu yeyote na nikamuomba mungu anisaidie!.

2. Nilijiapiza kujiepusha kushirikiana na mtu yeyote kumuhujumu mtu yeyote kwa dhuluma na nikamuomba mungu anisaidie!.

3. Nilijiapiza kumkosoa mtu yeyote kwa njia ya hekma na busara na kumshauri ajirekebishe ikiwa anamdhulumu mwenzake kwa kutokujua au kwa makusudi na nikamuomba mungu anisaidie!.

Kwa sababu yeyote ile, sitakuwa tayari kuihalifu misingi yangu hii kwa sababu yeyote ile ,kwani kufanya kinyume na hapo, itakuwa ni kuchagua njia mbaya miongoni mwa njia mbaya kabisa !.

KWA SASA KILICHOBAKIA NI HIKI;

1. Mh. Mbowe! Muombe radhi Mh.Zitto kwani wewe unajua umemfanyia nini na unaujua vizuri mkakati unaoendelea. Mwenyekiti muombe radhi mwenzako yaishe tujenge chama na taifa letu!

2. Mh. Lema, umemkosea Zitto na wewe unaelewa hilo, muombe radhi tusoonge mbele tafadhali!,

3.Kilewo, Umefanya jambo ambalo si jema sana kwa kusambaza waraka wa kumchafua zito bila kujua au kwa kujua, muombe radhi Zitto yaishe tujenge chama na nchi yetu!.

4.Mchungaji Msigwa! Wewe ni mchungaji, tumia busara za kichungaji muombe zitto msamaha! Wewe umemchafua na unaendelea kuuchafua zitto kwa makusudi na hali unajua. Ni bora ukaomba radhi yakaisha.! hauwezi kupungukiwa na kitu Msigwa!

5.Yericko nyerere na wenzako wewe tumekuwa tukiungana mkono katika mambo mengi na wewe unalijua hilo, ila katika hili mimi nafsi yangu inakataa!.Tumia uaminifu wetu kumuomba Zitto radhi kwani wewe unajua umemfanyia nini!.Yericko naomba kwa hili tuwe waaminifu na busara itawale.Naamini mungu atakuongoza vyema.

Nawasihi sana wale mnaoendelea kuzunguka mitaani. Tafadhalini sana wekezeni nguvu zenu katika kushughulikia matatizo ya watu badala ya kuwachonganisha wanachama ikiwa kweli ninyi ni waadilifu, wenye nia njema na chama pamoja na nchi hii. Hatuwezi kuwa na mapenzi mema kwa jamii kwa kuchonganishana ,kufitinishana na kuchafuana!

Ni matumaini yangu kwamba jambo hili la kuendelea kuzunguka watu wakichafuana litakoma na atakayeliendeleza wananchi watamuelewa vyema!.

Maneno ya busara sana, lakini walengwa hawaambiliki.
 
Mkuu, kwa kuwa muaminifu, nimetumia muda mwingi na njia mbali mbali kulipata kosa la Zitto ka kusema kweli mpaka sasa sijaliona.Ninachokiona ni shutuma zinazoanzia hewani hewani.Wanaozianzisha nimejaribu bara kadhaa kuwaomba watoe vielelezo vya kuaminika vya kuthibitisha shutuma hizo mpaka leo hakuna alietoa zaidi yakuendelea kusisitiza "mnafiki", "anaringa" "msaliti" "anapenda sifa" "ana dharau" "amepewa hela na CCM" "KALALA HOTELINI" N.K. naomba kwama wewe unajua kosa lake objectively na una ushahidi wa kitaalam unaothibitika, basi uliweke hapa na tutamsinikiza objectively, aombe msamaha.

Mkuu betlehem, huwa nafuatilia sana mabandiko yako mengi hapa jukwaani na nimekuwa nikikuchukulia kama mtu mwenye uelewa mkubwa sana wa mambo haya ya kisiasa na nimekuwa nikiheshimu sana michango yako hapa. Najua ulikuwa tofauti sana na CDM mwanzoni lakini baadae ulisema umeamua kuwa upande wao.

Tatizo kubwa ninaloliona kwenye uzi wako huu ni kwamba umeamua kuchagua upande tayari na kwa maana hiyo umejitosa kuutetea kwa nguvu zako zote. Sitaki kuamini kabisa kwamba hata mtu wa aina yako anaweza kusimama na kutaka watu walete ushahidi juu ya mengi yanayosemwa dhidi ya huyo uliyejitosa kumtetea. Kuna mambo ambayo hayahitaji hata kuomba ushahidi ili kujua kwamba ni tatizo kwa huyu unayemtetea. Kwa mtazamo wangu mimi binafsi, sihitaji mtu yeyote kuniletea ushahidi ili eti nijiridhishe kwamba huyo unayemtetea ni mtu mwenye ubinafsi sana kwa maana ya yeye kwanza halafu taasisi (CDM) baadaye. Hili wala halihitaji ushahidi kutoka kokote isipokuwa ni wewe tu kufumbua macho na masikio yako ili uuone na kuusikia ukweli! Hivi unataka kuniambia unahitaji ushahidi gani ili kujua kwamba ZZK alikaidi makubaliano na wabunge wenzake wa CDM ya kugomea hotuba ya Rais wakati wa uzinduzi wa Bunge hili la sasa? Mtu ambaye anaenda kinyume na maamuzi ya pamoja ya taasisi wewe binafsi unamchukuliaje?

Kikubwa ambacho naona umekosea hapa ni kwamba ushauri wako si kwa ajili ya kumaliza mgogoro bali ni kwa ajili ya kuukuza. Nasema hivyo kwa sababu una upande tayari katika mgogoro husika na aina ya utetezi unaoutoa hapa ni sawa kabisa na ule ambao umekuwa na unaendelea kutolewa na watu ambao wako tofauti na CDM (rejea ushauri unaotolewa na watu wa CCM juu ya sakata hili). Kama ZZK anahujumiwa kisiasa, kwa nini isiwezekane na yeye akawa anahujumu wengine kisiasa? Ni kweli kwamba ndani ya CDM ni ZZK tu ndo mwenye uwezo wa kugombea na kuupata huo uenyekiti? Kama hivyo sivyo, kwa nini sasa huongelei wengine isipokuwa huyo tu?

Mkuu, kwa mtazamo wangu suala hili halitakwisha kwa hao uliowasema kuomba msamaha kwa ZZK bali ni kwa ZZK mwenyewe aidha kubadili mienendo yake na kukiri makosa yake ili kutokuacha maswali mengi au ajiondoe kwenye taasisi ambayo yeye (na wewe pia) anaamini haina demokrasia na kwenda kule ambako anaona kuna demokrasia. Hata kama hao uliowasema wamemzidi kete kisiasa ZZK, bado nadhani kwa kiasi kikubwa itakuwa ni kwa sababu yeye kawapa nafasi ya wao kufanya hivyo kutokana na makosa ya wazi kabisa ambayo huwa anayafanya!
 
Last edited by a moderator:
Kama unamtaka Mbowe aombe radhi kwa sababu tu ameona watu wanachafuana kwenye mitandao, na yeye hakuchukua hatua, nafikiri humtendei haki , na nikuulize swali hivi ni viongozi wangapi wa Chadema wamekuwa wakichafuliwa kwenye mitandao , mbona haujawahi kuchukua hatua hii unayochukua leo?
Mkuu, msimamo wangu ni huu toka zisu zote.Fuatilia nyuzi zangu toka mwanzo. Mimi toka wakati niko CCM,nimekuwa nikiwaambia akina Nape na wenzake waombe radhi pale ambapo walikuwa wakiwachafua viongozi wa chadema kwa makusudi.Uzuri jf historia haifutiki

Kuhusu Zitto na mahakama , yeye ndio alimwandikia barua katibu mkuu wake kuwa anataka kuchukua hatua za kisheria kwa kuchafuliwa , haja chukua hatua , hivi unalisemeaje jambo hili?
CHADEMA ikichafuliwa au kiongozi wajuu akichafuliwa, haipiti masaa nane wasemaji wachama hawajatoa ufafanuzi. unajua ni kwa nini waraka ule wa kumchafua zitto ulikaa humu zaidi ya wiki mbili bila chama kutoa ufafanuzi wowote kinyume chake viongozi wakawa wanaulike licha ya kujua ni wakutunga? unadhani kwa nini licha ya kuwa zitto bado alikuwa kiongozi wakati huo aliachwa achafuliwe tu mpaka kufikia hatua ya kuandika barua? kama chadema tunataka kujenga utamaduni wa kutojisahihisha mpaka kwa amri ya mahakama haya bwana. mimi sina la kusema.
 
Huyu mwanzisha mada nilikuwa nafatilia taratibu kila hatua ya thread na post zake.Nimepata picha kamili.
na mimi nilikuwa naenda taratibu ili kuzingatia kanuni za kimaadili na busara na nitazidi kwenda taratibu kuhakikisha tunafikia lengo zuri.
 
Nimeamua kuungana na watetezi wa nchi hii "Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kutetea rasilimali za nchi, uongozi bora, uadilifu na katika kusimamia masuala mbalimbali yanayohusu uongozi kwa ujumla.

Nimefikia hatua hiyo baada ya kuona Chama changu (CCM) ambacho kwa hakika nilikipenda kimepoteza muelekeo kwa kiwango kikubwa na baada ya kupima nimegundua hakiwezi kurejea kwenye njia tena.Nimefikia uamuzi huu baada ya kuona chama nilichokuwa kimegeuka kuwa adui wa watu badala ya kuwa rafiki wa wananchi,kuwa wanyonyaji wa wananchi badala ya kuwa watetezi wa wananchi, kuwa watu wasiowajibika, wasioshaurika, wasiojishugulisha, wasiojirekebisha, wasiosikiliza wanachoambiwa na wananchi na wanaotumia mamlaka waliyopewa kujinufaisha kwa njia za hila.

Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikiitetea CCM kwa dhahiri na kwa siri kutokana na mapenzi niliyo kuwa nayo kwa chama hicho licha ya udhaifu uliokuwa unaonekana ndani ya chama cha CCM kwa ku amini kwamba wangejirekebisha pengine, lakini naona uziwi na upofu umekuwa ukizidi siku hadi siku hata kuamini yale waliyosema wahenga kwamba "mtu anapokaribia kufa hawezi kuona wala kusikia tena mambo ya ulimwengu huu".

Nimejipatia kadi yangu ya CHADEMA jana Tarehe 13/03/2013 na nina nia ya dhati kushirikiana na wanachadema katika harakati za kutetea ujenzi wa taifa imara, adilifu, na lenye uongozi imara na unaowajibika.Nawasihi na wenzangu wenye mapenzi mema na nchi hii wajiunge na CHADEMA ili kulinda haiba, utu, heshima na taaluma zao kuliko kuendelea kuitetea CCM Huku viongozi wake wakiendelea kuhujumu nchi kwa hila.

Mwisho nawasihi watanzania wote tuchangie harakati za CHADEMA kwa hali na mali ili tuweze kufikia ukombozi wa kweli ili akili ndogo zisiendelee kutawala akili kubwa.

Wenu katika ujenzi wa taifa,
Betlehem,

wa JF.
 
"Nimejipatia kadi yangu ya CHADEMA jana Tarehe 13/03/2013 na nina nia ya dhati kushirikiana na wanachadema katika harakati za kutetea ujenzi wa taifa imara, adilifu, na lenye uongozi imara na unaowajibika" by betlehem

Bora Fisadi kuliko mnafiki wa siasa.
 
Last edited by a moderator:
Kwa atakaye kuwa na swali lolote aniulize .safari hii nitamjibu hapa hapa na kwa uwazi kabisa.Kwa hali ilivyo kwa sasa, hii ndio itakuwa njia bora kabisa!

Ndugu zangu,kwanza nawasalimu sana!

Kwa kipindi sasa nimekuwa nikijaribu kusisitiza kuridhiana na kurudisha uhusiano mwema miongoni mwa wanachadema kwa kukwepa kueleza wazi wazi kile kinachotokea dhani ya chama nikiamini kwamba wahusika wangenielewa na kuchukua hatua za haraka kwa kuwa wanaelewa vizuri kile wanachokifanya. Kwa bahati mbaya ni kwamba inaonekana jitihada hizo zimekwama na bado baadhi ya viongozi wa chama wanaendelea kuzunguka huku na kule wakifitinisha wanachama wenzao na wananchi. Hali hii ya uchonganishi naona sasa imefikia hatua mbaya kiasi kwamba naona hamna haja ya kuendelea kufichaficha mambo!.

Kwa mfano, Kufuatia hotuba aliyoitoa Mchungaji Msigwa huko Arusha 04/12/2013, ilikuwa kwa kiwango kikubwa imejaa uchonganishi na uchochezi miongoni mwa wanachama kufikia kiasi cha msikilizaji mmoja ndugu Exaud Mamuya kusema “ kutokana na speech ya Mh Msigwa, Zitto angetokea bahati mbaya angegombaniwa na kuraluliwa kama Simba aonavyo kitoweo.” Katika mazingira haya naomba sasa niwe muwazi zaidi kidogo.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,

Tatizo la msingi kwa sasa ndani ya CHADEMA, ni "u-mwenyekiti".Hizi mbio tunazoziona mitaani kwa sasa, na kurushiwa maneno kwa ndugu Zitto,ni matokeo tu lakini suala la msingi ni "u-mwenyekiti "ndugu zangu.Tatizo la msingi ni Zitto kuonekana anaonesha dalili za kugombea uenyekiti na kuonekana ana ushawishi ndani na nje ya chama hivyo asipochafuliwa na kufitinishwa haraka, anaweza akashinda uenyekiti kweli.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,

Imeonekana kwamba kutokana na umaarufu wa Zitto kutokana na mambo aliyokifanyia Chama na taifa kwa ujumla ukichanganya na uwezo wake binafsi, si rahisi kwa mtu mmoja kumchafua na akachafuka bali hilo linaweza kufanyika kwa ufanisi kwa kuunda kundi kubwa na ikiwezekana kuishawishi kamati kuu kufanya mchezo huo wa hatari, wakufedhehesha, na kukatisha tamaa kabisa; mchezo ambao ni dhambi kumbwa sana.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,

Kitu kinachofanyika kwa sasa, licha ya kwamba ni dhambi na udhalimu mkuu, kinasababisha wananchi kugawanyika makundi makundi bila sababu ya msingi. Kadhalika kunasababisha wote tuonekane kama watu ambao tunalenga kupigania vyeo na maslahi tu na tusio kuwa na maono wala uadilifu wa kiuongozi hali hiyo hutufanya tuonekane tuko radhi hata kumtoa mtu muhanga kwa dhuluma ili tufikie lengo..Hali hiyo haiwezi kuwa na manufaa kwetu binafsi, kwa chama wala kwa taifa letu.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,
Hatuwezi kuwa vionzi bora wala hatuwezi kupewa madaraka ya kuongoza nchi hii kwa kufanyiana hila, uzushi, fitna majungu na kuchonganishana wenyewe kwa wenyewe.

Ndugu wana CHADEMA, wenzangu,

Wakati wote tumekuwa tukimlaumu na kumkemea Naibu Katibu mkuu wa CCM, ndugu Mwigulu Nchemba kwa kufanya siasa chafu za fitna na kugombanisha watu. Sasa na sisi tunafanya nini sasa? Tunafanya nini sasa?tunafanya nini ndugu zangu!

MSIMAMO WANGU.

Mimi tangu nilipopata akili, nilijiapiza na nikamuomba mungu anisaidie kwenye mambo kadhaa!.

1.Nilijiapiza kujiepusha kwa uwezo na maarifa yangu yote kumdhulumu mtu yeyote kwa sababu yeyote na nikamuomba mungu anisaidie!.

2. Nilijiapiza kujiepusha kushirikiana na mtu yeyote kumuhujumu mtu yeyote kwa dhuluma na nikamuomba mungu anisaidie!.

3. Nilijiapiza kumkosoa mtu yeyote kwa njia ya hekma na busara na kumshauri ajirekebishe ikiwa anamdhulumu mwenzake kwa kutokujua au kwa makusudi na nikamuomba mungu anisaidie!.

Kwa sababu yeyote ile, sitakuwa tayari kuihalifu misingi yangu hii kwa sababu yeyote ile ,kwani kufanya kinyume na hapo, itakuwa ni kuchagua njia mbaya miongoni mwa njia mbaya kabisa !.

KWA SASA KILICHOBAKIA NI HIKI;

1. Mh. Mbowe! Muombe radhi Mh.Zitto kwani wewe unajua umemfanyia nini na unaujua vizuri mkakati unaoendelea. Mwenyekiti muombe radhi mwenzako yaishe tujenge chama na taifa letu!

2. Mh. Lema, umemkosea Zitto na wewe unaelewa hilo, muombe radhi tusoonge mbele tafadhali!,

3.Kilewo, Umefanya jambo ambalo si jema sana kwa kusambaza waraka wa kumchafua zito bila kujua au kwa kujua, muombe radhi Zitto yaishe tujenge chama na nchi yetu!.

4.Mchungaji Msigwa! Wewe ni mchungaji, tumia busara za kichungaji muombe zitto msamaha! Wewe umemchafua na unaendelea kuuchafua zitto kwa makusudi na hali unajua. Ni bora ukaomba radhi yakaisha.! hauwezi kupungukiwa na kitu Msigwa!

5.Yericko nyerere na wenzako wewe tumekuwa tukiungana mkono katika mambo mengi na wewe unalijua hilo, ila katika hili mimi nafsi yangu inakataa!.Tumia uaminifu wetu kumuomba Zitto radhi kwani wewe unajua umemfanyia nini!.Yericko naomba kwa hili tuwe waaminifu na busara itawale.Naamini mungu atakuongoza vyema.

Nawasihi sana wale mnaoendelea kuzunguka mitaani. Tafadhalini sana wekezeni nguvu zenu katika kushughulikia matatizo ya watu badala ya kuwachonganisha wanachama ikiwa kweli ninyi ni waadilifu, wenye nia njema na chama pamoja na nchi hii. Hatuwezi kuwa na mapenzi mema kwa jamii kwa kuchonganishana ,kufitinishana na kuchafuana!

Ni matumaini yangu kwamba jambo hili la kuendelea kuzunguka watu wakichafuana litakoma na atakayeliendeleza wananchi watamuelewa vyema!.

wenye vyama nawashauri msiongozwe na mawazo yaliyojaa ubinafsi. subirini maamuzi, Zitto kapewa muda wa kujieleza, muda wake haujaisha, akishajieleza, utetezi wake utalinganishwa na ushahidi uliopo. tatizo lenu nn mbona mmejaa mihemuko na mnahangaika kama kuku wa kinyeji anataka kutaga mayai? mm niwaulize hivi ikitokea zzk amekufa ghafla leo hii, cdm yenu haitaendelea? hamtaendelea katika cdm yenu, iweni wa kweli.

mm ninahisi wengi wenu hamjakomaa kisiasa, mngekuwa wakomavu mngesubiri uamuzi wa vyombo vyote ndani ya CDM na mngesoma sababu za kufikia uamuzi wowote watakaoufikia kisha baada ya hapo ndipo mngetoa uamuzi/ misimamo yenu na sio vinginevyo.

ndiyo maana kuna usemi kufa kwa kungwi sio mwisho wa kazi? kufa kwa mchungaji sio mwisho wa ibada
 
na mimi nilikuwa naenda taratibu ili kuzingatia kanuni za kimaadili na busara na nitazidi kwenda taratibu kuhakikisha tunafikia lengo zuri.

Badala ya kupangua tuhuma 11 zilizotolewa na Kamati kuu wewe unaanza kujiundia tuhuma? Wewe bado unadamu halisi ya ukoo wa panya huko CCM.
 
1452339_558673044208406_2063836110_n.jpg
 
Mkuu betlehem, huwa nafuatilia sana mabandiko yako mengi hapa jukwaani na nimekuwa nikikuchukulia kama mtu mwenye uelewa mkubwa sana wa mambo haya ya kisiasa na nimekuwa nikiheshimu sana michango yako hapa. Najua ulikuwa tofauti sana na CDM mwanzoni lakini baadae ulisema umeamua kuwa upande wao.

Tatizo kubwa ninaloliona kwenye uzi wako huu ni kwamba umeamua kuchagua upande tayari

ndugu wikolo , iko hivi: kwa mfano unapoona watu wawili wanapiga, ukadhani ipo haja ya kuwasuluhisha na kuwapatanisha kwa kuwa umegundua kwamba wote ni kaka zako,ukawaambia waache kupigana wakae chini waongee (na hasa baada ya kugundua kwamba msingi wa ugomvi wao ni nini), halafu pamoja na kuwaambia hivyo, unaona mmoja anaendelea kumshushia ngumi mwenzake, nadhani hapo uamuzi wa busara ni kujaribu kumshika yule anayeendelea kurusha ngumi (Ijapokuwa katika kumshika huko, na wewe msuluhishi unaweza kushushiwa kipigo vile vile).Katika hali ya kawaida, utakapojaribu kumshika yule anayeendelea kurusha ngumi, uliemshika anaweza kukutafsiri kwamba upo upande wa ambaye hujamshika lakini kumbe ishu ni kwamba uliemshika yeye anaendelea kurusha ngumi wakati mwenzake katulia.Katika mazingira hayo hakuna ujanja. katika kusuluhisha migogoro, hiyo inaitwa "Dilema of udesirable ends"

Ndugu, wikolo , tusiwe wepesi wa kusahau.Ni juzi tu hapo Rais Kikwete kamshauri Rais Kagame azungumze na waasi wa DRC ili kupata amani DRC.Bila shaka Rais Kikwete alijiridhisha kwamba Kagame ana nafasi kubwa katika kuuchochea au kuuzima mgogoro wa DRC. Hata hivyo kwa macho yetu tulishuhudia Rais Kikwete akinyeshewa na mvua ya mawe kutoka kwa Kagame.

Ndugu wikolo , haya mambo ni magumu kidogo na sirahisi kama mtu anavyoweza kudhani kwa harakaharaka.
 
Ndio nazidi kukuona pimbi, nini maana ya katiba? nini maana ya vikao vya maamuzi? Issue ya Kagame ina lipi la kufanana na issue za Zitto?

Huu mlango unaotaka kutokea ndio wa kuingilia hautoki ndugu hata kwa kuruka ukuta!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom