Tatizo CHADEMA ni Uenyekiti: Kweli Humweka Mtu Huru!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,427
Kwa atakaye kuwa na swali lolote aniulize .safari hii nitamjibu hapa hapa na kwa uwazi kabisa.Kwa hali ilivyo kwa sasa, hii ndio itakuwa njia bora kabisa!

Ndugu zangu, kwanza nawasalimu sana!

Kwa kipindi sasa nimekuwa nikijaribu kusisitiza kuridhiana na kurudisha uhusiano mwema miongoni mwa wanachadema kwa kukwepa kueleza wazi wazi kile kinachotokea dhani ya chama nikiamini kwamba wahusika wangenielewa na kuchukua hatua za haraka kwa kuwa wanaelewa vizuri kile wanachokifanya. Kwa bahati mbaya ni kwamba inaonekana jitihada hizo zimekwama na bado baadhi ya viongozi wa chama wanaendelea kuzunguka huku na kule wakifitinisha wanachama wenzao na wananchi. Hali hii ya uchonganishi naona sasa imefikia hatua mbaya kiasi kwamba naona hamna haja ya kuendelea kufichaficha mambo!.

Kwa mfano, Kufuatia hotuba aliyoitoa Mchungaji Msigwa huko Arusha 04/12/2013, ilikuwa kwa kiwango kikubwa imejaa uchonganishi na uchochezi miongoni mwa wanachama kufikia kiasi cha msikilizaji mmoja ndugu Exaud Mamuya kusema " kutokana na speech ya Mh Msigwa, Zitto angetokea bahati mbaya angegombaniwa na kuraluliwa kama Simba aonavyo kitoweo." Katika mazingira haya naomba sasa niwe muwazi zaidi kidogo.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,
Tatizo la msingi kwa sasa ndani ya CHADEMA, ni "u-mwenyekiti".Hizi mbio tunazoziona mitaani kwa sasa, na kurushiwa maneno kwa ndugu Zitto,ni matokeo tu lakini suala la msingi ni "u-mwenyekiti "ndugu zangu.Tatizo la msingi ni Zitto kuonekana anaonesha dalili za kugombea uenyekiti na kuonekana ana ushawishi ndani na nje ya chama hivyo asipochafuliwa na kufitinishwa haraka, anaweza akashinda uenyekiti kweli.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,
Imeonekana kwamba kutokana na umaarufu wa Zitto kutokana na mambo aliyokifanyia Chama na taifa kwa ujumla ukichanganya na uwezo wake binafsi, si rahisi kwa mtu mmoja kumchafua na akachafuka bali hilo linaweza kufanyika kwa ufanisi kwa kuunda kundi kubwa na ikiwezekana kuishawishi kamati kuu kufanya mchezo huo wa hatari, wakufedhehesha, na kukatisha tamaa kabisa; mchezo ambao ni dhambi kumbwa sana.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,
Kitu kinachofanyika kwa sasa, licha ya kwamba ni dhambi na udhalimu mkuu, kinasababisha wananchi kugawanyika makundi makundi bila sababu ya msingi. Kadhalika kunasababisha wote tuonekane kama watu ambao tunalenga kupigania vyeo na maslahi tu na tusio kuwa na maono wala uadilifu wa kiuongozi hali hiyo hutufanya tuonekane tuko radhi hata kumtoa mtu muhanga kwa dhuluma ili tufikie lengo..Hali hiyo haiwezi kuwa na manufaa kwetu binafsi, kwa chama wala kwa taifa letu.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,
Hatuwezi kuwa vionzi bora wala hatuwezi kupewa madaraka ya kuongoza nchi hii kwa kufanyiana hila, uzushi, fitna majungu na kuchonganishana wenyewe kwa wenyewe.

Ndugu wana CHADEMA, wenzangu,
Wakati wote tumekuwa tukimlaumu na kumkemea Naibu Katibu mkuu wa CCM, ndugu Mwigulu Nchemba kwa kufanya siasa chafu za fitna na kugombanisha watu. Sasa na sisi tunafanya nini sasa? Tunafanya nini sasa?tunafanya nini ndugu zangu!

MSIMAMO WANGU.

Mimi tangu nilipopata akili, nilijiapiza na nikamuomba mungu anisaidie kwenye mambo kadhaa!.

1.Nilijiapiza kujiepusha kwa uwezo na maarifa yangu yote kumdhulumu mtu yeyote kwa sababu yeyote na nikamuomba mungu anisaidie!.

2. Nilijiapiza kujiepusha kushirikiana na mtu yeyote kumuhujumu mtu yeyote kwa dhuluma na nikamuomba mungu anisaidie!.

3. Nilijiapiza kumkosoa mtu yeyote kwa njia ya hekma na busara na kumshauri ajirekebishe ikiwa anamdhulumu mwenzake kwa kutokujua au kwa makusudi na nikamuomba mungu anisaidie!.

Kwa sababu yeyote ile, sitakuwa tayari kuihalifu misingi yangu hii kwa sababu yeyote ile ,kwani kufanya kinyume na hapo, itakuwa ni kuchagua njia mbaya miongoni mwa njia mbaya kabisa !.

KWA SASA KILICHOBAKIA NI HIKI;

1. Mh. Mbowe! Muombe radhi Mh.Zitto kwani wewe unajua umemfanyia nini na unaujua vizuri mkakati unaoendelea. Mwenyekiti muombe radhi mwenzako yaishe tujenge chama na taifa letu!

2. Mh. Lema, umemkosea Zitto na wewe unaelewa hilo, muombe radhi tusoonge mbele tafadhali!,

3. Kilewo, Umefanya jambo ambalo si jema sana kwa kusambaza waraka wa kumchafua Zitto bila kujua au kwa kujua, muombe radhi Zitto yaishe tujenge chama na nchi yetu!.

4. Mchungaji Msigwa! Wewe ni mchungaji, tumia busara za kichungaji muombe zitto msamaha! Wewe umemchafua na unaendelea kuuchafua zitto kwa makusudi na hali unajua. Ni bora ukaomba radhi yakaisha.! hauwezi kupungukiwa na kitu Msigwa!

5. Yericko Nyerere na wenzako wewe tumekuwa tukiungana mkono katika mambo mengi na wewe unalijua hilo, ila katika hili mimi nafsi yangu inakataa!.Tumia uaminifu wetu kumuomba Zitto radhi kwani wewe unajua umemfanyia nini!.Yericko naomba kwa hili tuwe waaminifu na busara itawale.Naamini mungu atakuongoza vyema.

Nawasihi sana wale mnaoendelea kuzunguka mitaani. Tafadhalini sana wekezeni nguvu zenu katika kushughulikia matatizo ya watu badala ya kuwachonganisha wanachama ikiwa kweli ninyi ni waadilifu, wenye nia njema na chama pamoja na nchi hii. Hatuwezi kuwa na mapenzi mema kwa jamii kwa kuchonganishana ,kufitinishana na kuchafuana!

Ni matumaini yangu kwamba jambo hili la kuendelea kuzunguka watu wakichafuana litakoma na atakayeliendeleza wananchi watamuelewa vyema!.
 
Mbowe ana mipango hatari sana na vijana wake ,alishawahi hadi panga plot ya kumuwekea sumu zzk
 
Mkuu uwa nathamini sana michango yako lakini niliposoma hapo chini( SIJASOMA HEKAYA NZIMA) nimekuona mtu wa OVYO SANA

1. Mh. Mbowe! Muombe radhi Mh.Zitto kwani wewe unajua umemfanyia nini na unaujua vizuri mkakati unaoendelea. Mwenyekiti muombe radhi mwenzako yaishe tujenge chama na taifa letu!

2. Mh. Lema, umemkosea Zitto na wewe unaelewa hilo, muombe radhi tusoonge mbele tafadhali!,
 
Kwa mnaodhani CHADEMA itayumba eti kisa ZZK katimuliwa, hamko seriazi.

Jamaa ataondolewa, then watapika propaganda kama wafanyavyo sasa kuhusu matamko n.k.

Bado CHADEMA itakuwa imara zaidi na zaidi.

Propaganda hazitaishinda kweli.
 
wewe acha hizi story za abunuasi na kufundisha watu nidham ya uoga mbona hutaki kuona waraka wa kipuuzi wa zito....siasa ni game na zitto kashajifunga utabadilishaje matokeo
 
Mkuu uwa nathamini sana michango yako lakini niliposoma hapo chini( SIJASOMA HEKAYA NZIMA) nimekuona mtu wa OVYO SANA

1. Mh. Mbowe! Muombe radhi Mh.Zitto kwani wewe unajua umemfanyia nini na unaujua vizuri mkakati unaoendelea. Mwenyekiti muombe radhi mwenzako yaishe tujenge chama na taifa letu!

2. Mh. Lema, umemkosea Zitto na wewe unaelewa hilo, muombe radhi tusoonge mbele tafadhali!,
Kitu pekee ninachokumbuka kwa huyu jamaa ni kuwa ametokea ccm hivi majuzi. Akili zake humu jamvini zilikuwa ni za akina ze makopolo et al.
 
wewe ndio mnafiki mkubwa na ukawaombe msamaha viongozi na wanachama wa CHADEMA kwa kuandika upuuzi kama huu. Nina mashaka na uwezo wako wa kufikiria. Maelezo mengi lakini pumba tupu
 
Unawapotezea watu muda kwa kuongea mambo ya ajabu .Mwacheni Zitto na Uongozi wa Chadema wanaongea watayamaliza .JF hakuna msaada kwa Chadema au Zitto zaidi ya hisia zenu na majungu .
Mkuu ungeonesha uajabu wa nilichokisema ungeonekana kwamba una roho safi kuliko kunikemea tu bila kuibua wala kujibu hoja.
 
wewe ndio mnafiki mkubwa na ukawaombe msamaha viongozi na wanachama wa CHADEMA kwa kuandika upuuzi kama huu. Nina mashaka na uwezo wako wa kufikiria. Maelezo mengi lakini pumba tupu
Ungejibu hoja, kuuliza shwali au kuonesha udhaifu wa hoja angalau moja, nadhani ungekuwa umeongea jambo zuri zaidi.
 
Ungejibu hoja, kuuliza shwali au kuonesha udhaifu wa hoja angalau moja, nadhani ungekuwa umeongea jambo zuri zaidi.

sasa kuna hoja gani hapo ya kujibu zaidi zaidi ni kudhoofisha uwezo wangu wa kufikiria. Nenda kajipange next time uje post zenye akili
 
Zitto hapaswi naye kuomba radhi? Kama uko objective .......
Mkuu, kwa kuwa muaminifu, nimetumia muda mwingi na njia mbali mbali kulipata kosa la Zitto ka kusema kweli mpaka sasa sijaliona.Ninachokiona ni shutuma zinazoanzia hewani hewani.Wanaozianzisha nimejaribu bara kadhaa kuwaomba watoe vielelezo vya kuaminika vya kuthibitisha shutuma hizo mpaka leo hakuna alietoa zaidi yakuendelea kusisitiza "mnafiki", "anaringa" "msaliti" "anapenda sifa" "ana dharau" "amepewa hela na CCM" "KALALA HOTELINI" N.K. naomba kwama wewe unajua kosa lake objectively na una ushahidi wa kitaalam unaothibitika, basi uliweke hapa na tutamsinikiza objectively, aombe msamaha.
 
Narudia kwa mara nyingine kuwa wewe Bethlhem ni gamba na ulikuja cdm majuzi kwa special mission na sasa imebuma
Usitupotezee muda wetu kuc wewe,eti wote hao wamwombe radhi ZZK!
Yeye amewaomba radhi aliowahujumu ùbunge?
Mfarijini mwenzenu mâana si mwenzetu huyo kwa muda mrefu
 
Aliyesoma yote naomba summary.
nafahamu ni kwa nini hukusoma.Ila haina shida wewe endelea kucomment bila kusoma tu hivyo hivyo halafu kwa njia hiyo hiyo ndio tutaweza kusimamia haki na kuleta maendeleo kwenye nchi hii.
 
wewe acha hizi story za abunuasi na kufundisha watu nidham ya uoga mbona hutaki kuona waraka wa kipuuzi wa zito....siasa ni game na zitto kashajifunga utabadilishaje matokeo
Mkuu kuna waraka mwengine au ni ule ambao CHADEMA wamesema si wao na hawajui ulikotoka?
 
Mkuu uwa nathamini sana michango yako lakini niliposoma hapo chini( SIJASOMA HEKAYA NZIMA) nimekuona mtu wa OVYO SANA

1. Mh. Mbowe! Muombe radhi Mh.Zitto kwani wewe unajua umemfanyia nini na unaujua vizuri mkakati unaoendelea. Mwenyekiti muombe radhi mwenzako yaishe tujenge chama na taifa letu!

2. Mh. Lema, umemkosea Zitto na wewe unaelewa hilo, muombe radhi tusoonge mbele tafadhali!,
Mkuu huwa sifanyi mambo kumfurahisha mtu au kumuudhi mtu.Nafanya kile ninachoamini ni sahihi.Kufanya kitu kumfurahisha mtu hata kama hayuko sawa kwenye jambo, ni kumpoteza.Ulitakiwa uniulize kwanini nadhani Lema anatakiwa amuombe radhi zitto.
 
Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom