Tatizo CCM ni kushindwa kujibu hoja jinsi zinavyotolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo CCM ni kushindwa kujibu hoja jinsi zinavyotolewa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Mar 5, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  WajaJF:

  Nadhani sasa wengi wetu tumeshaelewa sababu za kuweweseka kwa viongozi wa CCM hadi kutaka kufanya mambo ya ajabu.

  Tatizo ni kushindwa kwa viongozi wao kujibu hoja zionazotolewa na CDM, moja baada ya nyingine, tena kwa ufasaha bila kuuma maneno. Ni dhahiri hawana la kujibu kwani ni hoja ngumu. Kwa mfano umeme, inakuwaje serikali hii ya JK inashindwa kusimamia kikamilifu upatikanaji wa nishati hii kwa miaka mitano sasa.

  Sasa JK anataka tukubali kwamba suala hili limemshinda – maana kasema mwenyewe kwamba hawezi kutimiza yote kwani hata waliomtangulia walishindwa kutimiza yote. Mtu wake mmoja Chiligati naye kasema eti JK si Mungu wa kuweza kufanikisha kila kitu.

  Majibu hayo ni ya hovyo – kwani ni kweli JK hawezi kuwqatimizia Watz kila kitu – lakini yako ya msingi, na ambayo wenzake huko nyuma walifanikiwa kwa viwangi vikubwa tu. Hawakuwa Miungu.

  Waliotangulia walifanikisha uendeshwaji unaoridhisha wa reli ya kati, shirika la ndege, etc. sasa huivi mfano uwanja wa ndege wa Tabora umefungwa kwa sababu njia yake ya kurukia (runway) ndiyo mapitio ya ng’ombe. Hii imetokea kwa utawala wa Jk na usimamizi wake mmbovu kwa watendaji wake.

  Halafu kama JK anasema hawezi kutimiza kila kitu, basi ina maana akubali kwamba ahadi zake 200+ katika kampeni mwaka jana zilikuwa za laghai tu, maana tayari amekiri kwamba hawezi!

  Hoja zinazotolewa na viongozi wa CDM ni za msingi kabisa na wala hazina element yoyote ya kutishia amani kwani wanaojibu, angalau basi wawe wanapangua hoja moja baada ya nyingine kwa hoja pia kwamba, kwa mfano:

  * Bei ya sukari siyo 1,700/- kwa kilo na wala haikupanda sana, kwani 2005 ilikuwa 450/- tu!

  * Ukosefu wa umeme hauleti shida yoyote kwa wananchi kwani wanaotumia ni asilimia 5 tu – kelele za nini? Viwanda vilivyosimamisha shughuli wanatumia jenereta zao, na wamiliki wa biashara ndogondogo zinazotegemea umeme tumewaarifu wachukuwe likizo fupi.

  * Ukosefu wa kazi si tatizo kabisa na hili tulishalifanyia kazi – kwamba tangu 2005, ajira 1.3 million zimetengenezwa! Tatizi la wengi wa hao waajiriwa – yaani wamachinga – hawataki kukaa kwenye vibanda – sasa serikali ifanyeje?

  * Ufisadi unashughulikiwa – ziko kesi za vigogo mahakamani na mchoto wa Kagoda umesharudishwa, kelele za nini? Kama mnataka risiti za marejesho tutawapeni……etc… etc


  Angalau basi CCM wawe wanajibu hizo hoja za akina Mbowe ili wananchi waelewe, wapime ni nani kati ya CDM na CCM wanadanganya umma, waache kukimbilia kuwatisha wanaozitoa kwamba watashughulikiwa na vyombo vya dola.

  Hoja iliyojibiwa na Mbunge Lema kumjibu Spika kuhusu Pinda imefunikwa na Spika. Hakika majibu ya Lema hayawezi kujibika kwa hoja.

  CCM iache kutumia ma-stooge wake kuwatetea kama vile Mrema na Cheyo. Wote hao wawili wasingepata uwenyeviti wa kamati hizo nyeti za Bunge bila mbinu ya CCM – na wameambiwa lazima walipe fadhila za CCM. Hili kila mmoja analiona.

  Isitoshe hata hao wawili wameshindwa kujibu hoja za akina Mbowe moja baada ya nyingine, na badala yake wanazungumzia juu juu kwamba CDM wanatishia amani. Wanatishia kwa kauli gani hasa? Ziorodheshwe ni kauli hizi (a), (b), (c)….etc.

  Majibu ya kiujumlka jumla yanaonyesha udhaifu wa CCM katika kujibu hoja.
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Hivi unataka wajibiwe vipi hizo hoja?

  Au husikii, au huoni?
   
 3. oba

  oba JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tatizo la CCM na wanasiasa wao ni kukaba mtu badala ya kukaba mpira, washangiliaji- wananchi tunaona waziwazi kuwa wanacheza faulo badala ya kucheza mpira- hoja. Badala ya kujibu hoja wanakimbilia kuwavaa watoa hoja- mwisho wao umefika refarii na mashabiki tunauona mchezo vilivyo
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawajibu chochote isipo kutishia tu kwachukulia hatua wanaozitoa. Eleza wamejibu hoja zipi, ngapi na kwa maelezo yapi.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama wlishindwa kutangazwa kwa majibu ya Lema -- Mbunge mmoja tu, wataweza kweli kuwajibu ki-hoja, wale makamanda wakuu? CCM wake up, jibuni, ama sivyo you are losing the grip of leadership? Msikalie tu oh mnataka kutung'oa kama Misri etc etc. Jibuni hoja jamani! Aceni mambo ya kiutoto, nyie ni watu wazima.

  Hakuna haja ya kuwa-enlist akina Mrema kuwasemea -- twajua tayari mmemnunua -- hata mtoto mdogo anajua hivyo.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Mkuu Zak - hii imetulia kabisa. Badala ya akina Mrema kwani hawana wasomi waliobobea, wenye uwezo wa kuchanganua masuala ili wawajibu hao CDM? Yuko wapi Pro Bana? na wengine? Au CCM imekimbiwa na wasomi kutoka katika safu zake?
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawana muda wa kufikiri na kupanga majibu ya ufasaha kwa akina Mbowe -- kwani wamezama kwenye namna ya kupanga ufisadi wa kuwaibia Watanzania.
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Msomi gani anaitaka CCM? Labda wa kununuliwa!
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni usaliti mkubwa CCM wanawafanyia Watz. Wanashindwa hoja halafu wanakimbilia vyombo vya dola viwasaidie! Wakifanya hivyo hapo ndiyo watafahamu kwamba kamwe maharage siyo mboga -- ni dawa ya tumbo!
   
Loading...