Tatitizo la CCM ni ufisadi na sio makundi katika mbio za urais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatitizo la CCM ni ufisadi na sio makundi katika mbio za urais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Nov 27, 2011.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wanajamii tusikubari usanii wa CCM(MAFISADI)Kututoa katika hoja ya msingi UFISADI.Katika siku za karibuni kumekua na mbinu za makusudi za CCM kutuondoa katika hoja ya msingi ufisadi uliokithiri katika chama hicho,baada ya kushindwa kujivua magamba-kitu ambacho hakiwezekani kwani asilimia 99 viongozi wake CCM na serikali pamoja na JK mwenyewe ndio MAFISADI-Wameanza kupotosha ya kwamba tatizo la CCM ni vita ya makundi ndani ya chama kuelekea uchaguzi wa Rais mwaka 2015!Huu ni uongo mkubwa na upotoshaji!Hivi kweli uozo mkubwa wa ufisadi,rushwa ukosefu wa maadili miongoni mwa viongozi wake uliokitawala chama na serikali ni sababu ya mbio za urais 2015?!swala la ufisadi wizara ya nishati na madini,maliasili na wizara nyingine na taasisi za serikali ni mbio za urais 2015?!
  Mfano mdogo ni swala la Jairo ambalo limetupa sura kamili kukithiri kwa rushwa na ufisadi,rushwa,kulindana na ukosefu wa maadili katika wizara nyingi za serikali na taasisi zake,ambapo kwa Rais makini swala la kuwatimua wahusika wa sakata hilo akiwemo waziri wa nishati walikua wanapashwa kutimulia dakika chache baada ya kuawakilishwa kwa taarifa ya kamati je na hilo ni sababu ya mio za urais 2015?!TUSIPOTOSHWE MALIZENI KWANZA SWALA LA KUJIVUA GAMBA KABLA YA KUANZISHA KAULI MBIU NYINGINE "MAKUNDI KUELEKEA MBIO ZA URAIS 2015"TATIZO LA CCM NI UFISADI ULIOKITHIRI MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Naunga hoja kwa mikono yote miwili,wache hao magamba wawe kama mbuni aliyeficha kichwa chake kwenye mchanga asionekana ilihali mwili wake wote mkubwa uko wazi,waache ajifanye hamnazo,hii ni nafasi nzuri kwa Chadema katika uchaguzi ujao,kwa sasa Chadema wanachakusema,EL katwambia yale yaliyojificha,hata mama Sophia Simba aliwahi kusema hakuna aliye msafi CCM hii inamaanisha pamoja na hao akina Ben,Mwinyi,Sumaye,Warioba SAS yaani woote hao wana vimhogo vyao.Kwa msingi huo naona Chadema njia ni nyeupe
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  na lazima wang'oke hiyo 2015
   
 4. m

  mharakati JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  chadema ongezeni wabunge urais hampati 2015 labda 2025 tena mkimtoa Mbowe kama m/kiti..wekeni sura ya kitaifa zaidi
   
 5. m

  mharakati JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hivi mbowe, zitto hawawezi kuwa mafisadi na wenyewe? kitu gani kinawafanya mfikiri hawa jamaa watakuwa wasafi wakati watarithi mfumo wa kifisadi toka CCM pindi wakipata hayo madaraka...ufisadi ni mfumo mzima wa kisiasa, kijamii na kuchumi...sobodo anawapa hela sasa hivi, mtakataa vipi hela za kina manji, patel, somaiya, rostam, lowassa na nk? bado sijasikia jinsi gani CDM wataweka mkakati gani kuua huu mfumo wa kifisadi...na yule mke wa Slaa anaonekana ni fisadi kabisa kama mama Mkapa
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Tatizo la CCM ni Makundi yaliyosababishwa na Ufisadi! Kila kundi kwa upande wake linataka liishinde kundi lingine kwa ufisadi.
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  TATIZO LA CCM HIVI SASA NI MADAI YA UKWAPWAJI WA RAIS KIKWETE MWENYEWE NA KULE KUONEKANA KUSHINDIKANA CHA KUMFANYA WAKATI KILA KONA ANAHISI DOLA YATOSHA KUMKINGA VYA KUTOSHA

  You are such a wise young man, Advocate Jasha.

  Tatizo la CCM wala si la kiitikada kama Daktari Bana anavyajaribu kuwaaminisha, nasema tatizo la CCM wala si makundi kama ambavyo Mzee Mkama anavyojaribu kupaka mafuta mgongo wa chupa, ndio nasema hiviiii, tatizo la CCM wala si swala la kiu ya urais na usemi kwamba eti watu wnapigania kumbo kufa na kupona juu ya hilo nakataa kata kata kwa kuwa najua fika kwamba tatizo la CCM hivi sasa ni uporaji wa mali ya umma unaofanya na uongozi wa juu kabisa katika nchi yetu hivyo watu wachache tu mle ndani HUZIDIANA MGAO na kuanza kununiana mwisho wa siku majambazi kuchinjana wenyewe kwa wenyewe hata kabla yetu sisi wenye mali kuwagusa.

  Lakini kwa kuwa sisi siku zote ni wale mafundi wa kutibu goti kwa dawa maumivu ya kichwa kama ambavyo wafanyavyo Muhimbili kwetu kila uchao, tutaendelea kujizungusha weeeee bila tija yoyote mwisho kuibuka tu na maneno ya kifedhuli kwamba eti hatuna ushahidi na ufisadi ndani ya chama chetu; bure kabisa na wala hamna kitu pale!!

  Tiba pekee ya kukifanya CCM ipone ni NEC wa chama hicho kujikamua kupata ule ujasiri wa Marehemu Mwalimu Nyerere na kuutumia ujasiri huo KUMUITA NYUMBANI RAIS KIKWETE, kama ambavyo ANC ilivyofanya kwa Mbeki kule bondeni, ili huyu baba akapishe uchunguzi wa kina (Public Inquest) kufanyika juu ya madai mbali mbali ya rushwa dhidi ya yake mwenyewe na uongozi wake.

   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KATIKA HILI LA MIKANGANYIKO JUU YA 'LA KUVUNDA LA EXECUTIVE CORRUPTION' CCM ITOKE VIPI: MOST URGENTLY EXERCISE RIGHT OF RECALL OF THE PRESIDENT ILI MPONE

  Chaguni ni kwa CCM hivi sasa kati ya kufa KI-LOFA KATIKA SIASA ZA NCHI HII kwa kumuona Kikwete ni wa maana zaidi kuliko chama chao na kwamba vile vile ni wa maana zaidi kuliko taifa letu la Tanzania au wajikomboe kwa ku-EXERCISE RIGHT OF RECALL OF THE PRESIDENT that is worst off diminishing their party's political fortunes and future.

  Laa sivyo, kama ambavyo tulivyowahi kuwaonya mapema zaidi huko nyuma - KILA KITU NI MDORORO MTINDO MMOJA mpaka CCM kugota kwenye aibu ya mwaka.

  Najua wengi hamtoamini haya ninayoyasema mpaka kuja kuyaona kwa macho na hatimaye kuyagusa kwa mikono ila wenye wenye upeo wa kuona mbali zaidi tayari wanazo taarifa hizi kibindoni.

  Watanzania Uwezo Tuna!!
   
 9. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  We waache tu wacheze 'kidali po' mwisho wa siku watapata adhabu yao kutoka kwa watz.
   
 10. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mke wa Slaa aliwahi kushika nafasi katika serikali mpaka ukasema anaonekana Fisadi??
  Usiwe na mawazo pungufu!!!
   
 11. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Unakumbuka Jeet Patel alitoa pesa kwa John Malechera kupitia kwa Anne kilango???
  Hizo pesa zilikwenda wapi??
  Anna kilango alifanywa nini??
   
 12. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Hatua ya kwanza kushughulikia ufisadi (kleptocracy) ni kuunda katiba mpya ambayo inasisitiza uwajibikaji na uwazi kwa watendaji kuanzia mkuu wa nchi hadi mkuu wa kijiji. Hiki ndicho CDM walikuwa wamekieleza kwa uwazi katika ilani yao ya uchaguzi wa 2010 na ndio unaona hadi leo hii wanapigania kupitia bungeni. Tukijenga utamaduni wa watawala kuwajibika kwa wananchi kila atajejiingiza katika vitendo vya ufisadi - awe rais awe mwenyekiti wa kijiji bila kujali ni wa chama gani kipo madarakani - atakumbana na rungu la pilato. Huu utamaduni wa ufisadi unalindwa na katiba yetu iliyochoka. Haishangazi kwa nini CCM wanataka ibakie ile ile kwa kuilemba na maneno matamu!!!!
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,898
  Trophy Points: 280
  Ndo maana hatuwaachi kwenye mijadala humu,tunahakikisha na mafurushi yao kama vile RICHMOND wanaabeba accordingly,hasafishwi mtu humu...Garbages zao watazibeba hadi siku wanaingia kaburini,they chose it!
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Naona ni vyote ambayo ufisadi ndo zaidi
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CCM na ufisadi ni damdam; hafukuzwi mtu mle maana ndio maslahi yao kichama inakoegemea.
   
Loading...