Story of Change Tatio la nguvu za kiume na ukweli wake

MOJA 01

New Member
Aug 22, 2021
1
45
Maana halisi ya nguvu za kiume inaweza kuwa tofauti kulingana na mtazamo wa mtu na mtu. Nitajaribu kuelezea kuhusu matatatizo au tatizo la nguvu za kiume na kutoa suluhuhisho rahisi ambalo kila mmoja wetu anaweza kuelewa.

Nini maana ya nguvu za kiume?

Kuna maana kuu tatu zinazoelezea nini maana ya nguvu za kiume, nazo ni

(a) Nguvu za kiume ni kuwa na uwezo wa kumpa mwanamke mimba

(b) Nguvu za kiume ni kuweza kuhimili dakika kuanzia tano, kumi, ishiri hadi sitini (saa nzima na kuendelea) kwenye sita kwa sita/(kuchelewa kufika kileleni).

(c) Uwezo wa kusimamisha uume/Kama ukishindwa kusimamisha uume basi hapa una tatizo la nguvu za kiume/Hanithi.

Angalia mfano huu hapa chini.

Kuna wanaume watatu;-

Wa kwanza, anaweza kusimamisha uume na anaweza kumtia mwanamke mimba ila huchukua dakika moja tu kwenye tendo, na muda mwingine huchukua sekunde ishirini/tako tatu tu anamwaga.

Wa pili, huyu hawezi kusimamisha na hawezi kumtia mwanamke mimba

Wa tatu, huyu anaweza kusimamisha uume vizuri, anaweza kufanya mapenzi zaidi ya nusu saa lakini hawezi kumtia mwanamke mimba.

Yupi ana tatizo la nguvu za kiume?

Kwa hiyo sasa kwenye maana hizo hapo kuu tatu A, B au C usipokuwa na uwezo mmoja kati ya huo hapo unaweza kuwekwa kwenye kundi la kuwa wewe ni mwanaume usiye kuwa na uwezo wa nguvu za kiume.

Katika maelezo hayo niliyo yatoa hapo juu watu wengi huwa wanashindwa kutofautisha kati ya tatizo la kwanza la pili na la tatu. Kushindwa huku kutofautisha kunawapelekea kujumuisha matatizo yote matatu na kuonekana kama vile ni tatizo moja, ukweli ni kwamba yapo tofauti.

Muda mwingi sana watu wengi tumekuwa na hulka ya kusema wanaume wana matatizo ya nguvu za kiume kumbe tatizo lao kubwa ni kukosa kuwa na BREKI tu. Hapa inabidi unielewe vizuri kidogo, watu wengi tumekuwa tukihusisha maana ya nguvu za kiume na uwezo wa kukaa dakika nyingi kwenye tendo: mfano, ukiwa unafanya mapenzi na mwanamke na ukawahi kumaliza(ukatumia dakika chini ya tano au kumi) hapo wewe utajiona kama vile hauna nguvu za kiume, kitu ambacho siyo sahihi.

Kutokuwa na uwezo wa kukaa muda mrefu kwenye tendo hiyo siyo tatizo la nguvu za kiume bali ni breki. Unaweza kujiuliza nini maana ya breki au kwa nini nasema hilo ni tatizo la breki na siyo nguvu za kiume? Chukuwa mfano huu,

Kijana mmoja anaendesha baiskeli lakini hii baiskeli haina breki(fupa), mara akafika kwenye mteremko mkali sana alipokuwa akiteremka kwa bahati mbaya akatokea mbuzi akiwa anakimbia na akakatiza mbele yake.

Je, unadhani nini kitatokea hapo?

Kwenye hali kama hiyo hapo lazima itatokea ajali tu, maana kubwa ni kwamba yule kijana atajitahidi kushika breki lakini kumbuka ile baiskeli haina hizo breki.

Maana ya mfano huu ndio unawakilisha uhalisia wa watu wengi kwenye jamii yetu, wanaume wengi hawana tatizo la nguvu za kiume bali wana shida ya breki.

Mwanaume yeyote anayeona kwamba yeye analo tatizo la nguvu za kiume ajiulize swali hili moja kubwa Je, anaweza kusimamisha uume?

Kama anaweza kusimamisha uume wake hata kwa dakika moja basi ajue fika kwamba yeye ni mzima wa afya. Kama hajaridhika ajiulize tena swali la pili Je, anaweza kumpa mwanamke mimba?

Kama Jibu ni ndiyo, basi hasiwe na wasiwasi wala shida ya kujiumiza kichwa na kukosa raha kila wakati, kwani hana tatizo na ni mzima wa afya kabisa.

Maswali hayo mawili yanatoa ufafanuzi na mwanga wa kuona tupo wapi kwenye swala hili, kwa hiyo kama mwanaume unaweza kumpa mimba mwanamke na unaweza kusimamisha uume hata kwa dakika kadhaa ujue wewe hauna tatizo la nguvu za kium, upo fiti.

SASA KAMA HAUSUMBULIWI NA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

JE, UNASUMBULIWA NA NINI HASWA?

Kulijibu swali hili inabidi turejee kwenye mfano wetu wa Baiskeli, mfano huu unawakilisha kundi kubwa la watu wengi wanaoona kuwa wapo kwenye hili janga la kukosa nguvu za kiume.

Kama ilivyokuwa baiskeli na miili yetu inafanana kwa kiasi kikubwa na baiskeli, uwezo wa kukaa muda mrefu kwenye tendo la ndoa(kufanya mapenzi) kunategemea na breki zako zina uwezo gani. Kama baiskeli haina breki nzuri basi jua kuwa hata ufanye nini hutoweza kutatua tatizo lako. Tatizo litaisha pale utakapokaza breki au kuweka breki mpya.

Breki kwenye mwili wa mwanaume huwa ndio kitu pekee kinachoweza kumpa uwezo wa kufanya mapenzi kwa muda mrefu bila ya kuhofika kuwahi kufika kileleni mapema (pre-mature ejaculation). Kuna hospital moja kubwa Mjini Dar es salaam inacho kitengo cha maalum cha kushughulikia kuwahi kufika kileleni(pre-mature ejaculation) hii ikiwa na maana kuwa hili tatizo ni kubwa sana, linalopelekea watu wengi kuhisi ni tatizo la nguvu za kiume.

KWA NINI KUWAHI KUFIKA KILELENI SIYO TATIZO LA NGUVU ZA KIUME.

Wanaume wengi duniani huwa tumezaliwa tukiwa na udhaifu wa breki, siyo wanaume wote. Kuna baadhi ya wanaume wanao huu uwezo wa kufanya mapenzi muda mrefu bila ya kufika kileleni(breki zao zipo vizuri), wamezaliwa hivyo. Wengi wetu hatuna huu uwezo wa kuchelewa kufika kileleni, lakini hilo siyo tatizo bali tupo hivyo na tumezaliwa hivyo, Hapa inabidi nikuelewesheni kidogo kwa nini nasema kwa msisitizo kuwa siyo tatizo.

Kama wanaume wengi tumezaliwa hatuna uwezo wa kufanya mapenzi muda mrefu bila kufika kileleni, elewa kuwa hilo siyo tatizo bali ni hali ya kawaida.

Kutoweza kutofautisha kati ya matatizo ya nguvu za kiume na kuwahi kufika kileleni mapema ndiko kunakopelekea watu wengi ( hapa najumuisha hadi wataalam wa afya ) kuhisi wanaume wengi wana shida ya nguvu za kiume.

Hii siyo sahihi kabisa na inaenda kinyume na uhalisia uliopo, jua kuwa uwezo wa kufika mapema kileleni kwa wanaume wengi hilo ni jambo la kawaida na kama wewe ni mwanaume jua kuwa upo vizuri kabisa na hauna tatizo lolote lile, hata kama unachukuwa sekunde mbili hauna tatizo(upo-fiti).

TUFANYE NINI KUONGEZA UWEZO WA KUCHELEWA KUFIKA KILELENI/ JINSI YA KUBORESHA BREKI ZETU.

Hapa nataka kuboresha na kutoa watu tongo-tongo kwenye hili swala la nguvu za kiume na breki, tumeendelea kudanganjwa na watu wengi kuwa ili tuweze kupata nguvu zetu za kiume inabidi tufanye vitu vifuatavyo:-

a) Mchuzi wa pweza, Huu ni uongo wa muda mrefu na wa wakati wote ambao umekuwa ukitumika kuwaongopea wanaume kuwa watakuwa na uwezo wa kipekee kwenye sita kwa sita kama wakinywa mchuzi wa pweza na nyama yake. Jiulize ni kwa muda gani umekuwa ukinywa mchuzi wa pweza, je kuna mabadiliko yeyote umeyaona? Kama yapo ujue wauzaji wa mchuzi wa pweza wamekuwekea dawa za kuongeza hamu(Viagra).

b) Alkasusu imekuwa maarufu sana kwa siku za hivi karibuni, lakini hakuna matokeo ya mwendelezo kwenye uboreshaji wa wewe mwanaume kuchelewa kufika kileleni. Kama unahisi nakuongopea hebu jaribu kuacha kunywa alafu uone kitatokea kitu gani. Watu wengi wamekuwa wakiingizwa kwenye hili janga la kunyweshwa madawa ya kuongeza nguvu za kiume bila wao kujijua. Dawa hizi unaweza kuwekewa kwenye chakula maji au hata maziwa na vile vile kwenye supu. Kuwa makini na jua ukweli kwani ukweli utakuweka huru.

c) Karanga/Nazi na mihogo mibichi ni chakula kama vyakula vingine, tumezoea kusifia kuwa vina mchango kwenye kuboresha tendo lakini hakuna uhusiano wowote ule.

d) Asali na Tende hazina uhusiano wowote na wewe kuchelewa kufika kileleni au kuwa na nguvu nyingi.

e) Mbegu za maboga zina zinki nyingi, hizi uboresha mbegu za kiume na siyo kukupa wewe uwezo wa kuchelewa kufika kileleni. JUA TOFAUTI.

f) Dawa za miti shamba/dawa za kimasai/vumbi la Kongo na dawa za hospitali, hapa inabidi ujiulize swali moja hivi kama ukiwa hauna hizi dawa Je, Tendo huwa linakuwaje kwa upande wako?

g) Tatizo la kisaikolojia, wanaume wengi hii ndio sehemu pekee ambayo huwa wanaikimbilia kwenye masuala ya kuwahi kufika kileleni/tatizo la nguvu za kiume, wengi wao husingizia kazi nyingi na kuchoka vile vile kusongwa na mawazo.

Ukweli utabaki kuwa vitu hivi vyote havitupi uwezo wa kudumu wa kuwa na breki/kuchelewa kufika kileleni, bali vimekuwa kama ni suluhisho la muda mfupi na pia si-suluhisho kabisa, lakini zimekuwa ni njia za kujipatia pesa kwa wafanya biashara.

Kwenye baadhi ya vitu nilivyoweka hapo juu watu wengi wanaamini ukitumia basi utajiongezea nafasi ya kuwa mshindi kwenye sita kwa sita na tatizo lako la nguvu za kiume (kuwahi kufika kileleni mapema) litaisha. Katika uongo mkubwa ambao watu wengi huwa wanajiongopea ni huu hapa. Huwezi kutoa shida ya breki kwa kula chakula au matunda bali kwa kufanya mazoezi tu.

Haya mazoezi hayajumuishi mazoezi ya kukimbia au kunyanyua vitu vizito bali ni mazoezi maalum kwa ajili ya kuongeza breki zako. Mara nyingi haya mazoezi hua yanatakiwa kufanywa kwa muda wa kuanzia miezi mitatu haidi mwaka mmoja ili kupata matokeo sahihi na kuongeza uwezo wa breki kwenye mwili wa mwanaume.

Moja kati ya haya mazoeiz linaitwa kegel, nimesema ni moja kwa kuwa yapo mengi na huwa yanaleta matokeo tofauti tofauti.

Lingine ni jaribu ukiwa unaenda kukojoa husiwe unakojoa moja kwa moja bila kuweka vituo, jaribu kuukata mkojo wako hata mara moja au mbili kila unapokojoa.

Naamini kwa hiki kidogo unaweza kuboresha na kuimarisha uwezo wako, nashauri jiupushe sana na kutumia madawa yeyote yale, yawe ya asili(miti shamba ) au ya hospitalini. Shida ya dawa ni kuwa unakuwa mtumwa wa dawa/teja, siku ukipata miadi ya kukutana na mwanamke na hauna dawa hapo ndipo utakapochanganyikiwa.

STAY SAFE.
 
Upvote 1

Dremix

New Member
Jul 9, 2018
1
45
Kwaiyo mtu mwenye tatizo la kuwahi kileleni akitumia Hilo zoezi la kegel atakuja kutengemaa na kupona?
 

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
16,411
2,000
Tatizo la nguvu za kiume linakuzwa na wajasiliamali wanaojiita ni wataalamu wa tiba.....

Ukubwa wa tatizo la nguvu za kiume unatengezwa katika misingi ya hofu na wasi wasi wafanyabiashara wauze dawa zao.......

Vijana wengi wamepata madhara na wengi wanaendelea kupata madhara kwa kijtibu ugonjwa wasiokuwa nao........

Mtu isipomfaa akili yake basi utamdhuru ujinga wake......
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
25,542
2,000
Vijana wengi wamepata madhara na wengi wanaendelea kupata madhara kwa kijtibu ugonjwa wasiokuwa nao........
vijana wengi wana usongo wa mawazo, maisha magumu hawajui kesho yao !! wana wasiwasi sababu kiuchumi hawako vizuri, na ki kawaida pesa inaleta ahueni katika afya ya mwili hasa wakati wa kujamiiana.

Nakubaliana na wewe, hili tatizo linakuzwa ila halijawa hatua kubwa kiasi hiki.
 

shibela

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
492
1,000
Tatizo la nguvu za kiume linakuzwa na wajasiliamali wanaojiita ni wataalamu wa tiba.....

Ukubwa wa tatizo la nguvu za kiume unatengezwa katika misingi ya hofu na wasi wasi wafanyabiashara wauze dawa zao.......

Vijana wengi wamepata madhara na wengi wanaendelea kupata madhara kwa kijtibu ugonjwa wasiokuwa nao........

Mtu isipomfaa akili yake basi utamdhuru ujinga wake......
Tatizo katika uhalisia wake lipo pia
 

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
16,411
2,000
Ni kweli huo ni uwanja mwingine mkuu ila hela za Corona serikali yako tayari imechukua tena mara 2 hivi

Maisha ndivyo yalivyo

Pumzika kwa amani Corona
Kweli mkuu serikali yetu ni kama serikali zingine za dunia ambazo zinalazimika kuendana na uelekeo wa upepo unapovuma....
 

Thad

JF-Expert Member
Mar 14, 2017
13,049
2,000
Asante kwa kunifumbua macho, kumbe wanaume wengi wana tatizo la ukosefu wa break za kiume na sio upungufu wa nguvu za kiume!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom