Tathmini: Zitto Kabwe ni sawa na akina Freeman Mbowe mia moja (100)?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Nimepita sehemu nikakuta huu mjadala wananchi wanajadili uwezo wa kisiasa kwa kumlinganisha Zitto Kabwe na Freeman Mbowe. Nilisimama pembeni ili kusikiliza kwa makini nini hasa chanzo na mantiki ya mjadala huo.

Baadhi ya watu kwenye mjadala huu walikuwepo wanazuoni, wanahabari, wastaafu na makundi ya watu mbalimbali.

Mhariri mmoja mkongwe wa gazeti maarufu lenye magazeti dada yanayochapishwa karibu nchi zote za jumuiya ya Afrika ya Mashariki alisema "kwa mambo yalivyo sasa ni dhahiri kisiasa Zitto Kabwe ni zaidi ya Freeman Mbowe mia moja (100)" akaendelea kusema "sababu zangu ni kama ifuatavyo; Mbowe aling'ara akiwa na Zitto, popote pale hususani Bungeni alimbeba Mbowe kwani wakati Dr. Slaa alipoacha ubunge, Zitto aliuficha udhaifu wa Mbowe Bungeni"

Mdau mwingine alimuuliza swali "Kaka, kwani ZZK alikuwa mwenyewe?" Jibu: "kwa kweli Kitili alikuwa msanifu (architect) hodari asiyeonekana akifanya kazi kwa uratibu mahiri wa Dr.Slaa" akaendelea "ndio maana hata press za Chadema siku hizi si habari". Kwa kumaliza akasema "Mbowe alijua kwa Zitto kutoka Chadema angekufa kisiasa matokeo yake sasa amesimama kuliko Chadema"...akasema " kwa ulinganisho wa Zitto labda Mbowe wawe mia". Kwa kweli sikuchangia lolote nikaona niulete mjadala huu jamvini.

Je ni kweli Zitto = Freeman 100?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe alichukua chama mwaka uliofuata akapata wabunge kibao 2005, akapata wabunge zaidi 2010, akaongeza wabunge mwaka 2015.

Mbowe kashachukua tuzo ya kiongozi bora wa upinzani Afrika

Zitto alichukua chama 2014 na akashinda ubunge mwenyewe. ungesema kwamba Mbowe mmoja ni zitto 100. ungeeleweka

Zitto kahongwa sana na makampuni ya madini na serikali kipindi yupo PAC. utamlinganisha vipi na Mbowe ambaye mnamtafuta kila muda kumhonga imeshindikana!?
 
Wabunge wa 2015 ni wa Lowassa na anaondioka nao

Utakuwa hukusikia vizuri, Zitto mmoja ni sawa na mwenyekiti mmoja wa CCM taifa na wabunge wa CCM 99 ndiomaana walishindwa kuendesha bunge lililopita wakawa wanajadili mipango ya kumuua Zitto atakaporudi nchini, kwa ufupi waliunda wizara isiyo rasimi ya kujadili namna ya kumuua Zitto.
 
Mkuu Wakudadavua, utawala na menejimenti ya shughuli za chama cha siasa, kwa kiasi kikubwa hufanana sana uendeshaji wa shughuli za biashara. Mh. Mbowe ni mfanyabiashara maarufu na mwenye mafanikio makubwa sana, hata sera na itikadi za chama chake ni za kibepari. Amezaliwa na kukulia katika familia ya kitajiri yenye maono ya kibepari, pengine naweza kusema ni kwa kariba ya viongozi wenye maono ya kibepari chama cha Republican na ya watu kutoka familia za kina Bush na Trump kwa kule Marekani.

Huwezi kufanya ulinganisho wenye uhalisia kwa kumfananisha na Mh. Zitto Zuberi Kabwe, ambaye ni msomi kijana, mwenye maono ya kijamaa. Huyu kakulia familia ya kawaida sana, ni mtu mwenye shahuku kubwa ya kuifanyia makubwa nchi hii kama Tundu Lissu. Kwa ulinganisho na kule Marekani, naweza kumfananisha na matazamo wa kisera wa chama cha Democratic na kariba ya watu kama Bill Clinton na Barack Obama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe alichukua chama mwaka uliofuata akapata wabunge kibao 2005, akapata wabunge zaidi 2010, akaongeza wabunge mwaka 2015.

Mbowe kashachukua tuzo ya kiongozi bora wa upinzani Afrika

Zitto alichukua chama 2014 na akashinda ubunge mwenyewe. ungesema kwamba Mbowe mmoja ni zitto 100. ungeeleweka

Zitto kahongwa sana na makampuni ya madini na serikali kipindi yupo PAC. utamlinganisha vipi na Mbowe ambaye mnamtafuta kila muda kumhonga imeshindikana!?
Huwezi kupuuza nguvu ya Dr.Slaa,Kitila,Zitto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabunge wa 2015 ni wa Lowassa na anaondioka nao

2015 Lowassa aliikuta cdm imekolea ile mbaya. Kama alileta wabunge 2015 akiwa na miezi miwili, je ndani ya miaka miwili aliyokaa cdm alileta wabunge wangapi au alifungua matawi mangapi ya cdm? Bado mnadhani watu hawaijui ukweli? Na hii 2020 Bashiru leo kasema dola ndio itawapa ccm ushindi na sio kwa kura!
 
1A44EB19-E620-4E00-943B-00850CB5AE49.jpeg
 
Ukijibiwa hoja zako please nitaarifu na mimi sipo upande wowote ila CHADEMA ni wazuri kwenye siasa za matukio na maisha ya watu binafsi kwenye kujibu hoja za msingi ni watupu hasaa kwa kifupi ni sifuri plus kila mfuasi/mwanachama wao ni mwanaharakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom