Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu zangu,
Nimepita sehemu nikakuta huu mjadala wananchi wanajadili uwezo wa kisiasa kwa kumlinganisha Zitto Kabwe na Freeman Mbowe. Nilisimama pembeni ili kusikiliza kwa makini nini hasa chanzo na mantiki ya mjadala huo.
Baadhi ya watu kwenye mjadala huu walikuwepo wanazuoni, wanahabari, wastaafu na makundi ya watu mbalimbali.
Mhariri mmoja mkongwe wa gazeti maarufu lenye magazeti dada yanayochapishwa karibu nchi zote za jumuiya ya Afrika ya Mashariki alisema "kwa mambo yalivyo sasa ni dhahiri kisiasa Zitto Kabwe ni zaidi ya Freeman Mbowe mia moja (100)" akaendelea kusema "sababu zangu ni kama ifuatavyo; Mbowe aling'ara akiwa na Zitto, popote pale hususani Bungeni alimbeba Mbowe kwani wakati Dr. Slaa alipoacha ubunge, Zitto aliuficha udhaifu wa Mbowe Bungeni"
Mdau mwingine alimuuliza swali "Kaka, kwani ZZK alikuwa mwenyewe?" Jibu: "kwa kweli Kitili alikuwa msanifu (architect) hodari asiyeonekana akifanya kazi kwa uratibu mahiri wa Dr.Slaa" akaendelea "ndio maana hata press za Chadema siku hizi si habari". Kwa kumaliza akasema "Mbowe alijua kwa Zitto kutoka Chadema angekufa kisiasa matokeo yake sasa amesimama kuliko Chadema"...akasema " kwa ulinganisho wa Zitto labda Mbowe wawe mia". Kwa kweli sikuchangia lolote nikaona niulete mjadala huu jamvini.
Je ni kweli Zitto = Freeman 100?
Sent using Jamii Forums mobile app