Uchaguzi 2020 Tathmini yangu kwa wiki mbili za kampeni. CCM anaongoza kwa mbinu na mikakati bora

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,457
1,440
Nimefuatilia kwa umakini kuhusu kampeni zinazoendelea hadi sasa. Kimsingi CCM inaongoza kwa mikakati na mbinu bora zaidi kuliko vyama vingine vya Chadema,ACT nk na hivyo kuwa na nafasi nzuri ya kushinda asilimia 80+ Hii ni kutokana na sababu zifuatazo:

1. CCM imeweza kuwatumia makada wake kikamilifu walosambaa nchi nzima wakifanya kampeni kwa mpigo wakati wapinzani wamemwachia mgombea uraisi pekee kwa sasa.kwa mfano tumeona huko zanzibar juzi makada wengine wa Chadema hawakuwepo kabisa inaonekana wamejikita kwenye majimbo yao wakipigania uhai wao.

2. CCM wamaonekana kuwa wako makini - serious-kupambana kwelikweli kwa nguvu zote bila kupuuza chochote mbele yao na wakijibu hoja za wapinzani na hapohapo wakifafanua sera zao wakati wapinzani wanatumia muda mchache kuelezea sera zao na hususani kuelezea kwa kina udhaifu wa sera za chama tawala na madhara yake kiuchumi na ustawi wa jamii kwa kipindi cha muda mfupi na mrefu badala yake wanatoa hoja nyepesi.

3.CCM wanatumia saikolojia ya kujaza watu kwenye mikutano ili kujenga mob sychology kuonyesha kukubalika kwao kwa wananchi ili baadaye tarehe 28.9.2020 wapigiwe kura kwa imani kuwa hiki ndicho chama kinachokubalika na wengi na kwa kuchagizwa na propoganda sahihi

4.Wana uwezo kifedha na logistiki vitu ambavyo vimewarahisishia zaidi kuyafikia maeneo yote muhimu ya wilayani majimboni na vijijini.

5.Mikoa yenye kura nyingi ya kanda ya ziwa mgombea wao ameitumia vizuri fursa ya kujitangaza pamoja na wagombea ubunge na madiwani kwenye mikutano ya kampeni.Aidha ameweza kufukia mashimo ya waliachwa kwenye kura za maoni.

6.CCM inajitahidi kutoacha pengo au mwanya kwa wapinzani sasa hivi kusini kuna JK na Mama SAmia na kaskazini Waziri Mkuu wakati wapinzani hawaonekani kusambaa nchi nzima nguvu kubwa kila mmoja kwenye jimbo lake. Kutoka na uhaba wa fedha wameshindwa kusambaza nguvu kazi zao kusaidia majimboni.

7.Mgombea uraisi anaeleweka kwa lugha nyepesi kwa wananchi na anazungumzia maendeleo yanayoonekana. Hii inamwongezea hali ya kuaminika zaidi akipewa madaraka. Mbinu ya kutumia vikundi visivyoonekana,wanamuziki na coverage ya media siyo ya kupuuza hata kidogo inasaidia sana kwa CCM
8. Kampeni ya kitanda kwa kitanda na uwepo wa matawi na mashina kwa chama cha CCM inawabeba sana kufikia ushindi. Hivyo wamekuwa na malengo ya muda mrefu ya kutafuta ushindi mengine siwezi kuyasma hapa kwa sababu za kimkakati na malengo ya muda mfupi yote yanabebana interchangebly.

8.Kwa ujumla vyama vya upinzani kwa kipindi hiki cha mwanzo vinaonekana kupoteana. Ni kama wanasindikiza tu au kukamilisha matakwa ya kikatiba bila kuwa na mwelekeo thabiti. Niseme CCM anashinda mapema tu bahati nzuri Mgombea uraisi wa Chadema amekiri leo mbele ya waandishi wa habari kuwa kazi ni nzito na kuwa wana changamoto ya fedha. Hii ni dalili ya kukubali kushindwa vinginevyo wabadilishe mbinu za mchezo na waanze pia kushawishi vyombo vya habari kuwatangaza badala ya mitandao ya kijamiii pekee. Kwa msingi huo wapinzani mkishindwa msilalamikie Tume ya uchaguzi kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki hali ndiyo hiyo inajieleza yenyewe.
 
Uliandika vizuri ila pointi ya 8 haihusian na mada tajwa


But kaa ukijua tulionewa na kunyanyaswa tupo wengi
Hadi kufikia Mwenyekiti wa ccm kijiji kumfokea headmaster hakianani lazima utawala wa sheria urudishwe nchi hii
 
Kuanzia kesho soma tena hii post yako,na uondoe makando kando yote.
Mechi zinaanza kupigwa kesho
 
CCM wametumia mbinu ya kuwaengua wapinzani na kutumia dola kuwakataza wasifanye siasa kwa miaka mitano sasa wanatumia mbinu ya ukabila kanda ya ziwa na kwingineko.
 
Nimefuatilia kwa umakini kuhusu kampeni zinazoendelea hadi sasa. Kimsingi CCM inaongoza kwa mikakati na mbinu bora zaidi kuliko vyama vingine vya CHADEMA, ACT nk na hivyo kuwa na nafasi nzuri ya kushinda asilimia 80+.

Hii ni kutokana na sababu zifuatazo:
  1. CCM imeweza kuwatumia makada wake kikamilifu waliosambaa nchi nzima wakifanya kampeni kwa mpigo wakati wapinzani wamemwachia Mgombea uraisi pekee kwa sasa. Tumeona huko Zanzibar makada wengine wamejikita kwenye majimbo yao wakipigania uhai wao.
  2. CCM wameonekana kuwa wako makini kupambana kwelikweli kwa nguvu zote bila kupuuza chochote mbele yao na wakijibu hoja za Wapinzani na hapohapo wakifafanua sera zao.
  3. CCM wanatumia saikolojia ya kujaza watu kwenye mikutano ili kujenga mob psychology kuonyesha kukubalika kwao kwa wananchi ili baadaye tarehe 28.9.2020 waweze kuungwa mkono na idadi kubwa na hatimaye kupigiwa kura.
 
Come on now dndagula, we as CHADEMA have survived the past 20+ years under extreme oppression under every single president of this country.

We know Voting Meko out will not change our condition. But again No President from the Green will change our condition to the better, therefore We must change the ruling system or suffer the consequences later.
 
Mikakati ya Kubeba watu kwenye Maroli, kufunga shule kwa wanafunzi?
Kujaza Fiesta?

Na kuchezeshwa singeli?
 
119057614_197973511683765_7178176507246786920_n.jpg
 
Wamefanikiwa kuwaengua Wapinzani kinyemela na kutumia dola kuua demokrasia.
 
Kwa kubeba wanafunzi na akina Alikiba kwenye uzinduzi?
Hili ndilo kosa unalofanya kutokujua kuwa hao wanaobebwa karibu wote ni wapiga kura.

Kumbuka kuwa CCM ina hazina ya wanachama hai milioni nane. Ukichanganya na wapya wanaopatikana mikutanoni hizo ni kura nyingi sana.
 
Back
Top Bottom