Uchaguzi 2020 Tathmini yangu juu ya Uchaguzi Mkuu 2020: Hakuna sababu nzuri ya kukataa kuteua wabunge wa Viti Maalum CHADEMA

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
986
1,000
1605829845328.png

Tundu Lissu (Mgombea Urais wa Chadema) na Job Ndugai (Spika)

Kuna mdau kanitumia kitabu cha Gene Sharp (2012), kiitwacho "From Dictatorship to Democracy: A Conceptual Framework for Liberation."

Yaani, "Safari ya Kutoka Kwenye HImaya ya Kidikteta Kuelekea Kwenye HImaya ya Kidemokrasia: Mawazo Ambayo ni Msingi wa Hoja za Kuendeleza Mapambano ya Ukombozi." (Tafsiri yangu).

Mdau huyu amenitaka nikisome na kisha nijibu swali hili: Kama wabunge wa viti maalum wanatokana na kura za mgombea urais, na kama kura za mgombea urais wa CHADEMA zilizotangazwa na tume ni sehemu ya kura zote ambazo Chadema wanadai kwamba walipata, uamuzi wa kukataa kuteua wabunge wa viti maalum wa Chadema ili waende Bungeni kula kiapo na kuchapa kazi ya ubunge unachangia vipi katika kuimarisha demokrasia nchini Tanzania?

Nimekisoma kitabu na kukimaliza. Kina kurasa 100, na kimeandikwa kwa Kingereza chepesi. Ninaelewa mengi yaliyojiri katika siku zote za uchaguzi mkuu wa 2020. Pia najua malalamiko kadhaa ya vyama vya upinzani. Baada tafakari nimefikiria kama ifuatavyo:

Mosi, kama mgombea urais wa Chadema (Lissu) alipata kura X, na NEC ikatangaza kwamba Lissu kapata kura Y, ni wazi kwamba kura X ni kubwa kuliko kura Y, yaani X>Y.

Pili, Tofauti kati ya kura X na kura Y, tuseme kura Z, ndizo kura zinazobishaniwa. Chadema wanapinga kutotangazwa kwa kura Z. Yaani, Chadema wanapinga kutangazwa kwa kura Y pekee bila kujumlisha kura Z.

Tatu, kura Y zilizotangawa na NEC ni sehemu ya kura X zinazotamkwa na viongozi wa Chadema.

Nne, wabunge wa viti maalum wa Chadema wanatokana na kura Y, ambazo ni kura halali.

Kwa hiyo, idadi ya wabunge wa viti maalum kupitia Chadema iliyotangazwa na NEC ni idadi ya wabunge iliyotokana na kura halali.

Lakini, kama Chadema wanasema kuwa LIssu alipata kura ambazo ni ndogo kuliko zile zilizotangazwa na NEC, basi hitimisho langu linaporomoka hadi kuwa kifusi; na nitaungana nao katika msimamo wa kukataa kuteua wabunge wa viti maalum.

Nitatoa mifano miwili ili kufafanua hitimisho langu hili.

Mfano wa kwanza, ni mfano wa mtu aliyefukuzwa kazi, akamshitaki mwajiri kwenye Mahakama ya Kazi, Makahaka ikaamuru alippwe Milioni 10 kama fidia. Ikiwa mwajiri atamlipa milioni 3 pekee, anazipokea na kuzitumia kama gharama za kuweka wakili ili ambane mwajiri kwa hoja kwamba malipo ya milioni tatu "pekee" hayatoshi, lakini baada ya kuchukua milioni tatu.

Na mfano wa pili ni wa kifalsafa zaidi. Tunapotaja fasili ya umbo linaloitwa pembetatu tunasema hivi: "Pembetatu ni umbo lenye kona tatu pekee na pande tatu pekee."

Katika fasili hii neno "pekee" ni muhimu sana, kwani hata mraba unazo pembe tatu na kona tatu pia. Lakini mraba hauna pembe tatu "pekee" wala pande tatu "pekee."

Kwa mujibu wa mifano hii miwili, sasa nahitimisha hoja yangu. Katika kura za mgombea urais, Tundu Lissu, Chadema hawadai kura Y pekee, kama ilivyotangazwa na NEC. Wanadai kura Y na kura Z, ambapo tayari wamekwishapatiwa kura Y, lakini bado kupatiwa kura Z, kama watathibitisha kwamba zipo.

Hivyo, Chadema wanaweza, na wanapaswa kupokea kura Y na kuendelea kudai kura Z, kwa kuweka bayana hoja isiyoruhusu hewa wala maji kupenya.

Kwa mantiki hii, Chadema hawapaswi kuona shida kuteua wabunge wa viti maalum ili waende Bungeni kuapa. Nashauri wafanye hivyo leo.

Hapa nimejaribu kufikiri kwa sauti kwa kuzingatia hoja zilizojengwa na Gene Sharp (2012) katika kitabu chake kiitwacho "From Dictatorship to Democracy: A Conceptual Framework for Liberation."

Kwa mujibu wa kitabu hiki, kukataa kuteua wabunge wa viti maalum, kama wanavyofanya Chadema kwa sasa, ni aina mojawapo ya udikteta; na majadiliano ya maana hufanyika kati ta "mdikteta" na "mdemokrasia."

Yaani, Chadema inabidi waonyeshe kwa mawazo, maneno na vitendo kwamba wao ni "wademokrasia" ili wapate uhalali wa kumkabili yule anayeitwa "mdikteta."

Nimeambatanisha kitabu hicho hapa chini, kwa ajili ya wale wenye utayari wa kujisomea.

Huu ni mtazamo wangu, na ninawajibika kikamilifu kusanifu hoja hii yenye kutetea mtazamo huu.

Mama Amon,
Sumbawanga Kusini.
 

Attachments

 • File size
  925.9 KB
  Views
  13
 • 1605829804278.png
  File size
  119.9 KB
  Views
  0

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
7,893
2,000
asante kwa ushauri ambao pia hutuko tayari kuufata.

kukubali ushauri huu ni kuunga mkono ufedhuli uliofanywa na CCM na vijibwa vyake.
Mkuu Daudi Mchambuzi sikutegemea wala sitegemei uunge hoja kama hiyo, yenye nguvu kimantiki. Hakika wewe ni mtu wa mwisho kufanya hivyo ila wa kwanza kuunga udikteta ulioko ndani ya CHADEMA km kuwafukuza uanachama,bila kujitetea, wabunge waliogoma kuunga amri ya kususia bunge la bajeti kwa ajili ya korona. Ninahisi hata Mbunge wa Nkasi wa CHADEMA aliyekubali kuapishwa na kushiriki uzinduzi wa Bunge la 12 huenda akafukuzwa chamani.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,359
2,000
Kwa heshima, sikubaliani na kauli yako hii hapa.
Kwani mwajiriwa aliyelipwa milioni tatu hapo juu, akazipokea, na kisha akaendelea kudai ziada, alikuwa ameunga mkono ufedhuli wa mwajiri mkorofi?

Ni hivi, tunakuheshimu sana na ushauri wako tunauheshimu pia, lakini hatuko tayari kwa hilo. Kama ni kupoteza si vibaya tukipoteza zaidi fullstop.
 

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
986
1,000
Ni hivi, tunakuheshimu sana na ushauri wako tunauheshimu pia, lakini hatuko tayari kwa hilo. Kama ni kupoteza si vibaya tukipoteza zaidi fullstop.

Dah! Nyie watu wa huko Dar naona ngangari kweli.
Huku kwetu Sumbawanga tunaangalia mengi.
Poa tu.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,359
2,000
Mkuu Daudi Mchambuzi sikutegemea wala sitegemei uunge hoja kama hiyo, yenye nguvu kimantiki. Hakika wewe ni mtu wa mwisho kufanya hivyo ila wa kwanza kuunga udikteta ulioko ndani ya CHADEMA km kuwafukuza uanachama,bila kujitetea, wabunge waliogoma kuunga amri ya kususia bunge la bajeti kwa ajili ya korona. Ninahisi hata Mbunge wa Nkasi wa CHADEMA aliyekubali kuapishwa na kushiriki uzinduzi wa Bunge la 12 huenda akafukuzwa chamani.

Hakuna atakayemfukuza, na ushauri huo tumeutoa kwa chama, yeye aendelee na wajibu wake lakini ajue fika hatuafiki mchakato huu wa kishenzi. Ni juu yake kusaka maisha ya familia yake, ila sisi tunaangalia mustakabali wa chama.
 

Godfrey-K

JF-Expert Member
Jan 5, 2016
1,855
2,000
Kukubali kuteua viti maalumu ni kukubali uhalamia na ufedhuli uliofanywa na tume kwa maelekezo ya CCM. Mimi nilishiriki kusimamia uchaguzi huu, niliyoyaona yanatisha.

Nimeeleza kidogo tu kuwa kwenye kituo changu nilichosimamia Tundu Antipas Lissu alipata kura 79 na Magufuli alipata kura 31 lakini Lissu akandikiwa kura 6 na Magufuli kura 379 sasa hapo unakubali vipi? Ni bora kuacha tu.
 

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
986
1,000
Waliokutuma waambie hatupo tayari kushiriki kuhalalisha uovu!

Naona umekuwa "kijana wa kijana " squared hadi ukawa mtoto!
Hakuna mahali hoja yangu inaweza kutumika kuhalalisha uovu wowote.
Kwa taarifa yako, Lissu ni mwanasheria, na anaelewa fika nilichokiandika hapa.
Anaweza kupata shida kuikubali hoja kwa sababu nyingine, lakini sio sababu za kimantiki.
Soma hoja yangu tena.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,359
2,000
Dah! Nyie watu wa huko Dar naona ngangari kweli.
Huku kwetu Sumbawanga tunaangalia mengi.
Poa tu.

Mama Aron hilo bunge lingekuwa na meno, wangalau tungekubali kushiriki kwa shingo upande, ila sio bunge hili kibogoyo. Tulikuwa tukishuhudia hotuba za kambi ya upinzani zikizuiwa kusomwa bungeni, na hata zikisomwa hufanyiwa uhariri mkubwa hadi kupoteza maana ya hotuba husika.

Tulikuwa tukiona wabunge wa upinzani wakitolewa kwa uonevu na udhalilishwaji mkubwa, leo mama Aron umesahau na kuja na hadithi za X na Y! Unataka hao wapinzani waende wakadhalilishwe na kutumika kama chambo, na kuhalalisha ule umwagaji damu na wizi wa kura wa aibu? Kama unataka wakachukue hela sema waachwe wakachukue hela, lakini sio kushiriki bunge.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,359
2,000
Naona umekuwa "kijana wa kijana " squared hadi ukawa mtoto!
Hakuna mahali hoja yangu inaweza kutumika kuhalalisha uovu wowote.
Kwa taarifa yako, Lissu ni mwanasheria, na anaelewa fika nilichokiandika hapa.
Anaweza kupata shida kuikubali hoja kwa sababu nyingine, lakini sio sababu za kimantiki.
Soma hoja yangu tena.

Hakuna mwenye akili timamu ambaye ana tatizo na mantiki ya hoja yako, tatizo lipo kwenye uhalisia.
 

Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
8,531
2,000
Naona umekuwa "kijana wa kijana " squared hadi ukawa mtoto!
Hakuna mahali hoja yangu inaweza kutumika kuhalalisha uovu wowote.
Kwa taarifa yako, Lissu ni mwanasheria, na anaelewa fika nilichokiandika hapa.
Anaweza kupata shida kuikubali hoja kwa sababu nyingine, lakini sio sababu za kimantiki.
Soma hoja yangu tena.
Unachokishawishi ni chadema wakubali kupeleka wabunge wa viti maalum huku ukijua vyema hawatambui uchaguzi ulifanyika
 

Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
8,531
2,000
Kwa kumbukumbu zangu katika profile hii, unaona mie sina uwezo wa kusanifu hoja hii, mpaka nitumwe na mtu baki?

Hebu futa kauli yako yenye dharau isiyokubalika.
Wewe unatambua kabisa chadema hawatambui uchaguzi wa mwaka huu lakini unashawishi wakubali kupeleka wabunge viti maalum.

Kwanini nisiseme umetumwa kuja kushawishi ujinga?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom