Tathmini yangu fupi kuhusu Baraza Jipya la Mawaziri

O
Baada ya wanachi wa Tanzania kuchagua maendeleo ya kijani nchi nzima, kwa kuwapigia kura za kutosha wagombea wa CCM na kuufutilia mbali upinzani wa kupinga maendeleo ya nchi yetu. Wakati napitia matokea ya sehemu mbalimbali nikapata fikra pevu za kuangalia namna baraza la mawaziri litakavyokuwa. Hii ni tatmini yangu fupi kwa baraza jipya la mawaziri.

Waziri Mkuu
Kutakuwa na vita kubwa ya Uwaziri mkuu, Kassim Majaaliwa amefanya kazi kubwa sana ya kuufuta upinzani, pia amechangia kiasi kukubwa cha kupata hizi kura za kishindo. Naona atakuwa na upinzani mkubwa wa Dr Tulia, katika kuteuliwa kuwa waziri mkuu. Mwanamama huyu amekuwa na taswira nzuri mbele ya Mh Rais kwa kutekeleza yale ya kuwabana wapinzani wa kupinga maendeleo bungeni. Kura yangu ya Uwaziri Mkuu naona ikimuangukia Dr Tulia.

Waziri wa TAMISEMI
Mh Selemani Jaffo ataendelea na wadhifa wake. Hakika ameitendea vyema hii wizara toka akiwa naibu waziri na baadae kuwa Waziri kamili.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto.
Mh Ummy ataendelea na wadhifa wake, amekuwa taswira sahihi ya namna ya kuendesha wizara nyeti.

Wizara ya Fedha
Mh Doto Biteko atakuwa waziri kamili wa wizara hii, ili kuendeleza yale mazuri aliyofanya wakati akiwa waziri wa Madini

Wizara ya Uwekezaji
Mh Anjela Kairuki naona akirudi kuwa waziri wa wizara hii baada ya kuteuliwa katika zile nafasi kumi za Mh Rais

Wizara ya Viwanda
Mh Mpango atakuwa waziri wa wizara hii, ili litatikea ili kumpisha Doto Biteko katika wizara ya Fedha.

Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi
Mh William Lukuvi ataendelea kuwa waziri, japo naona kama karata anatakiwa kuzichanga vizuri

Wizari ya Utalii
Mh Dr Hamis Kingwangala ataendelea kuwa waziri

Wizara ya Kilimo
Namuona Mh Hussein Bashe akiwa waziri kamili wa wizara hii ya kilimo

Wizara ya Michezo
Mh Jokate Mwegelo atateuliwa kuwa mbunge na baadae kupewa wizara hii ya Michezo, Habari na Utamaduni. Hii inatokana na kazi yake nzuri na ya kutukuka akiwa kama Mkuu wa wilaya ya Kisarawe

Wizara ya Vijana,
Mh Mavunde ataendelea kuwa waziri kamili wa wizara hii ya kuawasaidia vijana

Wizara ya Utumishi wa Umma
Mh Jenista Mhagama atakuwa waziri wa wizara hii ili kuendelee kusimamia miongozo ya utumishi wa umma na kuboresha maslahi ya watumishi wa umma

Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Mh Luago Mpina atakabidhiwa wizara hii.

Wizara ya Nishati
Mh Medard Kalemani ataendele kusambaza umeme vijijini kwa kasi kubwa baada ya kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa.

Spika wa Bunge
Kama Waziri mkuu atachagulia Mh Kassim Majaliwa, naona kabisa Mh Tulia atakuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge litahitajika kuwa na nguvu kwani naona kutakuwa na hoja nzito nzito zitakazotikisa Muungano wa Tanzania, ikiwa Zanzibar itakuwa chini ya ACT.

Wizara nyingine naomba muendele kupendekeza
Umesahau kuwataja watu wafuatao:- 1. Kurwa Biteko
2. Doto James
3. Aliyeongoza Kura za naomi Jimbo la kawe
4. Mbunge wa jimbo la busanda mkoa wa geita
 
Ndoto hii. Magufuli will surprise all of you.

Anaweza hata akawachagua baadhi ya wapinzani kuwa wabunge na kuwapa Uwaziri😊
 
CCM hawana utaratibu wa kugawana vyeo mitandaoni kama upande ule mwingine ambao jamaa kabla hata ya matokeo kutangazwa akadai yeye ni waziri mkuu.
 
CCM hawana utaratibu wa kugawana vyeo mitandaoni kama upande ule mwingine ambao jamaa kabla hata ya matokeo kutangazwa akadai yeye ni waziri mkuu.
Tathmini ni tofauti na kugawa. Tunajua mwenye mamlaka ni Mh Rais na wasaidizi wake. Sisi tunachojaribu ni kuendana nq upepo unavyovuma
 
Umeeleweka nasoma kichwa cha habari. Nimesema hii ni tamthimini yangu na sijamfunga yoyote kusema tofauti. Mh Rais yeye ndiyo atakayekuja kuitimisha haya yote kulingana na maono yake makuUmeeleweka
 
Tathmini ni tofauti na kugawa. Tunajua mwenye mamlaka ni Mh Rais na wasaidizi wake. Sisi tunachojaribu ni kuendana nq upepo unavyovuma
Haya nimekuelewa ,

Ila huo sio utaratibu wa Chama kugawana vyeo mitandaoni.
 
Namuona Mwana FA akiwa either waziri au naibu waziri wa michezo

Huku Yule jamaa aliyetoka CRDB kuwa waziri wa Fedha
 
Kufuatia matokeo ya uchaguzi mkuu ambapo asilimia 99 ya wabunge watakuwa wakitoka CCM basi, na pia kwa kuwa zipo sura mpya kabisa ambazo zimeingia bungeni kwa mara ya kwanza na nyingine kuendelea kukalia nafasi zao basi, huu uzi ni mahsusi kwa ajili ya kuwatambua wale ambao dalili zinaonyesha kuwa watakuwa sehemu ya baraza la mawaziri

Wafuatao ni top 10 ya wale ambao hawajawahi kuwa wabunge lakini kwa vyovyote wengi wao watakuwa sehemu ya baraza jipya la Mawaziri, wapo watakaokuwa mawaziri kamili na wengine manaibu

1. Charles Kimei
2. Prof. Adolf Mkenda
3. Prof. Kitila Mkumbo
4. Askofu Josephat Gwajima
5. Jerry Slaa
6. Mrisho Gambo
7. Fredy Lowassa
8. Shaashisha Mafuwe
9. Patrobas Katambi
10. Kirumbe Ng'enda

Lakini pia wapo wengine watakaoteuliwa kuwa wabunge na Mh, hivyo wana nafasi kubwa pia ya kuwa ndani ya baraza hilo!

Kwa hizo sura mpya, na maeneo ambayo pia waligombea ni wazi kabisa ni mkakati mahsusi wa kuwaingiza sehemu nyingine nyeti zaidi!

N.B: Ieleweke kuwa Mh, naye hatabiriki pengine anaweza akabadilisha upepo humo angani na akaendelea na lile baraza lake la awali!
 
Back
Top Bottom