Tathmini yangu fupi kuhusu Baraza Jipya la Mawaziri

Baada ya wanachi wa Tanzania kuchagua maendeleo ya kijani nchi nzima, kwa kuwapigia kura za kutosha wagombea wa CCM na kuufutilia mbali upinzani wa kupinga maendeleo ya nchi yetu. Wakati napitia matokea ya sehemu mbalimbali nikapata fikra pevu za kuangalia namna baraza la mawaziri litakavyokuwa. Hii ni tatmini yangu fupi kwa baraza jipya la mawaziri.

Waziri Mkuu
Kutakuwa na vita kubwa ya Uwaziri Mkuu, Kassim Majaaliwa amefanya kazi kubwa sana ya kuufuta upinzani, pia amechangia kiasi kukubwa cha kupata hizi kura za kishindo. Naona atakuwa na upinzani mkubwa wa Dr. Tulia, katika kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Mwanamama huyu amekuwa na taswira nzuri mbele ya Rais kwa kutekeleza yale ya kuwabana wapinzani wa kupinga maendeleo Bungeni. Kura yangu ya Uwaziri Mkuu naona ikimuangukia Dr. Tulia.

Waziri wa TAMISEMI
Selemani Jaffo ataendelea na wadhifa wake. Hakika ameitendea vyema hii Wizara toka akiwa naibu waziri na baadae kuwa Waziri kamili.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto.
Ummy Mwalimu ataendelea na wadhifa wake, amekuwa taswira sahihi ya namna ya kuendesha wizara nyeti.

Wizara ya Fedha
Doto Biteko atakuwa Waziri kamili wa wizara hii, ili kuendeleza yale mazuri aliyofanya wakati akiwa Waziri wa Madini

Wizara ya Uwekezaji
Anjela Kairuki naona akirudi kuwa Waziri wa Wizara hii baada ya kuteuliwa katika zile nafasi kumi za Rais

Wizara ya Viwanda
Mh Mpango atakuwa waziri wa wizara hii, ili litatikea ili kumpisha Doto Biteko katika wizara ya Fedha.

Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi
William Lukuvi ataendelea kuwa Waziri, japo naona kama karata anatakiwa kuzichanga vizuri

Wizari ya Utalii
Dr. Hamis Kingwangala ataendelea kuwa Waziri

Wizara ya Kilimo
Namuona Hussein Bashe akiwa Waziri kamili wa wizara hii ya kilimo

Wizara ya Michezo
Jokate Mwegelo atateuliwa kuwa Mbunge na baadae kupewa Wizara hii ya Michezo, Habari na Utamaduni. Hii inatokana na kazi yake nzuri na ya kutukuka akiwa kama Mkuu wa wilaya ya Kisarawe

Wizara ya Vijana,
Antony Mavunde ataendelea kuwa Waziri kamili wa wizara hii ya kuawasaidia vijana

Wizara ya Utumishi wa Umma
Jenista Mhagama atakuwa Waziri wa Wizara hii ili kuendelee kusimamia miongozo ya utumishi wa umma na kuboresha maslahi ya Watumishi wa Umma

Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Luago Mpina atakabidhiwa Wizara hii.

Wizara ya Nishati
Medard Kalemani ataendele kusambaza umeme vijijini kwa kasi kubwa baada ya kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa.

Spika wa Bunge
Kama Waziri mkuu atachagulia Kassim Majaliwa, naona kabisa Tulia atakuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge litahitajika kuwa na nguvu kwani naona kutakuwa na hoja nzito nzito zitakazotikisa Muungano wa Tanzania, ikiwa Zanzibar itakuwa chini ya ACT.

Wizara nyingine naomba muendele kupendekeza

Chaka
 
Back
Top Bottom