Tathmini ya Sangu J kuhusu uzinduzi wa albamu ya #AFROEAST ya Harmonize

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
By Sangu Joseph

March 14, 2020 tulishuhudia Mkali Konde Boy, Tembo, Mmachinga wa zamani Harmonize akiweka historia ya kuzindua Albamu kibabe ya AfroEast na haya ni maoni yangu.

Kiukweli tangu nipate akili ya kufuatilia masuala ya burudani, Jumamosi niliona uzinduzi wa level ya juu sana na kibabe kama wote hapa nchini

STEJI/ JUKWAA

Kwanza tuanzie hapa steji haikua ya kitoto nadhani ni kutokana na mchango wa bosi kubwa Majizo kuingilia kati suala kama alivyoeleza Konde Boy mwenyewe kupitia joto la asubuhi kwa Gerald Hando.

Ile steji haikuwa ya kawaida. Ilikuwa imewekewa muda maalum, ukifika huo wakati inajifunga, na kwa host alikua limited na muda wa kuuliza maswali na Konde Boy kujibu, steji ilipojifunga na seti zilibadilishwa kwa ajili ya ngoma nyingine.

Steji na Sound ilikua safi kama inavyokuaga kwenye matamasha ya Mkuu Majizo.

MUUNGANIKO WAWATANGAZAJI/ COOPERATES/ WASANII

Moja ya creativity kubwa ambayo niliikubali sana ni pale tu ambapo kulikua na watu maalum waliokuwa wakitambulisha nyimbo ambazo Harmonize alikua akienda kuziimba.

Pale tulishuhudia Wakurugenzi wa Kampuni / Wasanii na Watangazaji wakitambulisha ngoma iliyokua kwenye Albamu then Konde Boy anaiimba baada ya hapo alipata nafasi ya kumuuliza maswali Konde Boy ambayo ilikua content kubwa sana kwa Blogs, website na Mitandao ambayo kazi yao kutoa taarifa.

Kwa Cooperates kama Sayona unaona kabisa alitendewa haki kwa sababu kuna wakati Konde Boy aliwapa mention moja kubwa na kibabe kabla hajajibu swali, hakika pale nadhani Sayona alifurahi sana.

Kuuliza swali kwa Bosi swali Multichoice Nataka Shelukindo pale kuli-secure endorsment nyingine yano mfanyabiashara muaminifu ukiingia naye makubaliano na anaweza kukupa Bonus kwenye mkataba mliosaini (Safi Sana).

Kwa watangazaji uliona jinsi walivyogawanywa; walikua wa maeneo mbalimbali Ile ilijibu kile ambacho nilikiandika miezi michache iliyopita (Tathmini yangu kwa Harmonize nje ya WCB) kuwa angehitaji kurejesha mahusiano na media ambalo kwa lile tukio amefanikiwa kwa asilimia 200.

Inaendelea.

#KijanaMzalendo #IloveTZ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom