Tathmini ya matumizi ya fedha katika uchaguzi mdogo Igunga na mahitaji ya kijamii Igunga

Guyton

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
263
78
Leo katika pitapita yangu fb nikakutana na uchanganuzi huu ambao binafsi nimependa kuwashirikisha nanyi;

Siku za karibuni kulikua na uchaguzi Igunga, katika uchaguzi huo vyama vingi vilishiriki lakini vyama vikubwa vitatu ndio vilionekana kuchuana vikali, vyama hivyo ambavyo ni CCM, CHADEMA na CUF imeripotiwa vimetumia jumla ya sh. Bil 3 na mil 550 uku CCM pekee ikitumia bil 3, CHADEMA mil 400 na CUF mil 150.

Ripoti za waandishi mbalimbali wa habari walioenda igunga kipindi cha uchaguzi zinasema Igu...nga ina tatizo sugu la maji, na katika hotuba ya wizara ya maji iliyosomwa katika bunge la bajeti 2010/2011, Jedwali Na. 9, lenye kichwa cha habari FEDHA ZILIZOTUMWA KWENYE HALMASHAURI KUANZIA MWEZI JUNI 2007 HADI MEI 2011 linaonesha igunga imetumiwa jumla ya sh. 1,201,310,526 kwa lugha nyepesi ni takribani bil 1 na mil 200 katika miaka 4 ya fedha.Lakini kampeni za siku 21 zimetumia bil 3 na mil 550.

Waandishi wemeripoti kuwa Igunga kuna ufukara, sasa hotuba ya bajeti 2010/2011 iliyosomwa bungeni, kwenye ukurasa 120, nanukuu ‘’ Aidha, jumla ya shilingi bilioni 4,925.6 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ambapo shilingi bilioni 1,871.5 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 3,054.1 ni fedha za nje’’ bil 1871.5 ukizingatia kuna wilaya 127, basi kila wilaya kwa mgawo ambao sio rasmi basi itapata takribani bil 14, sasa bil 3.55 zilizotumika Igunga kwenye uchaguzi(siku 21) ni 25%.

Vijana mnasemaje?? Kweli hawa watu wanamalengo ya dhati ya kutukomboa??
 

Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,965
2,389
kichefu chefu.. Me nangoja siku ya kuingia barabarani tu, na sitorudi nyumbani mpaka waondoke madarakani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom