Tathmini ya Dar Mpya: Matokeo na matarajio kwa umma

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,031
2,000
Dar Mpya ni zoezi lililokuwa na mafanikio na changamoto nyingi!
  1. Kwa mtazamo wangu, sikutegemea kuona zoezi likiendeshwa vile, nakumbuka kuanzisha uzi ulioomba wana Dar tumsapoti Makonda kutokana na kauli zake alizozitoa alipokuwa akihojiwa na clouds fm ktk power breakfast! kinyume chake ndicho nilichokiona ktk zoezi zima, hapakuwa na ujenzi wa Dar mpya hata kidogo! ilikuwa ni platform ya mashtaka na kuzungumzia kero za raia wachache kuliko kutaka kujua umma unasaidiwaje!
    • kesi mbili za ardhi za aina moja zilitosha kuelewa changamoto za ardhi na vikao vingeendelea kujadili nini kifanyike ktk ngazi 3 husika, 1 serikali za mitaa, manispaa na wizara ya ardhi! yes wapo ambao walikuwa wanataka kushtaki so zoezi la ukamataji na kufungua kesi kwa watendaji zingepewa nafasi maalum ofisini kwa mkuu wa wilaya/mkoa na wangetengeneza kamati maalum ya kutatua migogoro iliyopo sasa ambayo bado ingeendelea kama Dar mpya campaign nje ya media coverage!
  2. watumishi wa umma hawakutendewa haki na wengi walidhalilishwa bila ya sababu za msingi. kuna baadhi ya maswali hata angeulizwa waziri mwenye dhamana ktk idara husika asingekuwa na majibu lkn bado watendaji walitakiwa kuijibia serikali au kuambulia kashfa toka kwa mkuu wa mkoa. kumtaka afisa wa kitengo Fulani ajue kila linalotokea ktk manispaa na akikosea kuwa hana maana ni uonevu, maana hata mkuu wa mkoa pia naye anawajibu wa kulijua hilo lililotokea ktk mkoa wake lkn naye hakuwa na taarifa!
  3. makonda hakuwasaidia wananchi waliokuwa wameumizwa na sera mbaya au taratibu mbovu zilizoletwa na serikali kuu. mfano wahanga wa bomoabomoa, haikutosha kusema tu kuwa maeneo mnayoishi sio salama mtakufa ndio maana tumewatoa! wanaokufa kwa ajali barabarani ni wengi kuliko wanaokufa kwa mafuriko, kwanini tusivunje na barabara kwa kuwa zinaua sana! wananchi hawakugoma kutoka, wao wametaka wapewe fidia au msaada mwingine wa kuwahamisha, na kwa just kusema kuwa wote walipewa ardhi mabwepnde sio sahihi, ilipaswa itolewe lists ya wahanga wote waliolipwa na maeneo wanayotoka ili kila mlalamikaji iwepo status yake na ifahamike kwa umma!
nje ya kasoro hizi kumekuwa na mafanikio kwa kiasi.
  1. watendaji wengi wa Dar wameonesha utulivu wa hali ya juu, wamejitahidi kupatikana na kutolea ufafanuzi mambo mengi na kujibu kero za raia! pamoja na ukorofi wa wananchi na kero za mkuu wa mkoa, wengi wameonesha professionalism na walibaki kuwa composed na hii ni sehemu ya adabu ya utumishi wa umma! wasionekane kama wajinga, wengi walifuata taratibu za utumishi na kutoonesha utovu wa nidhamu kwa boss wao, na huu ni msingi mkuu wa uwajibikaji kwa watendaji. nawapa big up wtumishi wa umma wote wa Dar na Tanzania kwa ujumla!
  2. kero nyingi zilitatuliwa au kupatiwa majibu ya ufumbuzi hapohapo.
  3. taifa limejifunza juu ya migogoro mingi ya ardhi ambapo watendaji wa serikali za mitaa wamkuwa sehemu kuu ya kero za raia. pia kuna baadhi ya watumishi nao wamekuwa ni changamoto. huku wizara ya ardhi ikiwa mama wa madhambi yote na kuwa mwiba kwa wananchi, jambo linalopaswa kutengenezewa mjadala wa kitaifa ktk ofisi ya lukuvi.
Siioni Dar mpya, bado matarajio yangu ni kuiona Dar ileile kiutendaji. kukosekana kwa mikakati na maazimio ya pamoja baina ya serikali na wakazi imefanya niamini kuwa bado wananchi watatakiwa kuendelea kusubiri fungu la serikali ambalo halitoshi anyway.
 

Bila shuka

JF-Expert Member
Oct 14, 2014
598
500
Dar mpya mvua ikinyesha maji hayana pakwenda n barabara hufuruka mitaa huwa mafuriko
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom