Tathmini ya Chabruma Juu ya Upigaji Kura BMK, Chereko kwa CCM, Kilio kwa UKAWA,AKIDI KIULAINI

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777


Wadau, amani iwe kwenu.


Kwa sasa tunaelekea mwisho wa safari Katika Mchakato wa Kupata Katiba Mpya. Hakika ilikuwa ni safari ndefu ambayo ilijaa milima, mabonde na makorongo ya kila aina. Wengi wamesafiri hadi mwisho wa Safari, mmoja aliishia njiani kutokana na kifo ( RIP SHIDA SALUM) na wachache waliishia njiani kutokana na kushindwa mikiki na ugumu wa safari. Waliofika mwisho tuwapongeze na wale walioishia njiani kutokana na ugumu wa safari tuwapongeze pia kwani walijaribu.

Katika uzi huu, tathmini yangu itajikita kwenye hatua ya kupiga kura ili kupata Katiba inayopendekezwa. Hii ni hatua muhimu sana ambayo kila Mtanzania yupo macho kufuatilia kinachoendelea ndani ya Bunge hilo ili kujua matokeo yake. Hata wale wenzangu ambao hawakufika mwisho wa safari kutokana na uchovu ( UKAWA) wamefuatilia kwa karibu na wakati mwingine wamelazimika kutoa matamko kwa lengo la ama kuwaharibia wale ambao wanajiandaa kukabidhiwa vyeti vya Uzalendo na Ushujaa au kuwapongeza wale ambao wameshindwa muda mfupi kabla ya kufika kileleni. Pia UKAWA wamewatumia mawakala wao kama Jaji Warioba na timu yake kupaza sauti ili mchakato usifike mwisho ambapo Warioba alisema kuwa ataingia mtaani kupambana na Wajumbe wa Bunge Maalum japo hajafanikiwa kufanya hivyo baada ya wananchi kumpuuza. Pia kuna Waraka uliandaliwa na baadhi ya Maaskofu ambao ulisomwa Makanisani lengo likiwa ni kuwandaa waamini wao wasikubaliane na Katiba inayopendekezwa. Kwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu yote hayo yameshindikana na mchakato unafikia mwisho salama salmini

IDADI YA WABUNGE NA AKIDI INAYOTAKIWA
Kabla ya mchakato wa kupiga kura haujaanza, baadhi ya wanasiasa ambao ni kundi la UKAWA walisikika wakipaza sauti kuwa ijapokuwa Sammuel Sitta analazimisha bunge liendelee, Akidi haiwezi kupatikana kwa upande wa Zanzibar. Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad kwa nyakati tofauti wamenukuliwa wakisema kuwa AKIDI kwa upande wa Zanzibar haiwezi kupatikana. Hakika wajinga walipuuza maneno hayo ila yalisaidia kwa werevu kama Sammuel Sitta na wengine kujipanga na kuweka mikakati ya kufanikisha akidi. Huku Lipumba na kundi lake wakilala fofofo kwa kuamini kuwa akidi ya Zanzibar haiwezi kupatikana werevu waliendelea kujipanga kuhakikisha kuwa mambo hayaharibiki. Lipumba na wenzake waliamini hivyo kwa kuwa wabunge wote wa CUF ukimuondoa Hamad Rashid walifanikiwa kuwadhibiti wasirudi Dodoma. Pia walifanikiwa kuwadhibiti baadhi ya wabunge wa kundi la 201. Lipumba na kundi lake waliachwa midomo wazi tarehe 29 Septemba 2014, siku ya kwanza ya upigaji kura. Akitoa idadi ya wajumbe wa bunge hilo, Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Sammuel Sitta amesema kuwa idadi ya Wabunge wote wa Bunge Maalum ni 629. Kati ya hao Idadi ya Wabunge wa Tanzania Bara ni 419 na Wazanzibari ni 210. Akidi inayotakiwa ni 280 kwa Tanzania Bara na 140 kwa Zanzibar.

Idadi iliyopo kabla ya kuanza kupiga kura ni 295 kwa Tanzania Bara na 142 kwa Zanzibar. Kwa hali hiyo, kuna ziada ya wajumbe 15 kwa Tanzania Bara na 2 kwa Zanzibar. Ukiongeza na idadi ya wale walio hija na wagonjwa, basi akidi imepatikana kiulaini.

Takwimu hiyo iliwashtua sana UKAWA na hakika iliwanyima usingizi. Kwa hali hiyo, walilazimika kutumia mbinu za medani kuharibu kwenye hatua ya upigaji kura. Mbinu zilizotumika ni kushawishi baadhi ya wabunge wa kundi la 201 wapige kura za hapana. Pia waliwatumia waume wa wabunge wa kike ili wake zao wapige kura za HAPANA na kuwatisha kuwa wasipofanya hivyo, basi wajue kuwa hawana ndoa. Hilo walifanikiwa kwa wabunge wa Kiume wawili, ambao walipiga kura ya HAPANA kwa Ibara zote na wanawake wanne ambao ni wake wa Makada wa CUF pia wakipiga kura ya HAPANA. Baada ya wabunge hao kutekeleza matakwa hayo kwa shinikizo, Lipumba na wenzake wakipata maelekezo na akina Mbowe walilala tena usingizi fofofo huku Sitta na timu yake wakipanga mikakati ya kucounter hali hiyo.

Kosa jingine walilofanya UKAWA ni kupuuza kipengele cha kuunda Kamati ua Mashauriano ambacho ndicho kilichotumiwa na Sitta kuwamaliza UKAWA na kushinda fitina zao. Baada ya Wabunge sita wa Zanzibar kupiga kura ya Hapana kwa Ibara zote, Mwenyekiti Sitta alicheza kama Pele kwa kuunda kamati ya Mashauriano ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan kushughulikia jambo hilo kutokana na wajumbe wawili kuomba kusikilizwa. Hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 54 na 36 ya Bunge Maalum.

Kuona hivyo, Lipumba na kundi lake wakashtuka kutoka kwenye usingizi mzito. Wakaanza kumchafua Sitta kwenye mitandao ya kijamii kwa kumpakazia kuwa ameunda kamati ya Kuwatisha wajumbe waliopiga kura za hapana. Pia, waliwasiliana na Makada wao ambao wake zao walipiga kura ya HAPANA ili wawaambie wake zao Waondoke Dodoma na kurejea Zanzibar kwa madai ya kutishiwa kuuawa. Hata hivyo, ni wabunge wawili tu ambao ni Salma Said na Fatma Mohamed ndio walifanikiwa kuwashawishi ambapo waliondoka kwenye viunga vya bunge hapa Dodoma Jumanne tarehe 30 Septemba 2014.

Lipumba na kundi lake wakashindwa kuwashawishi wale wanawake wawili na wanaume wawili ambao wapo tayari kubadili maamuzi yao na kesho watapiga tena kura baada ya kukutana na kamati ya mashauriano. Baadhi yao wanasema kuwa walipiga kura ya HAPANA kwa shuruti na wengine wanasema kuwa hawakuelewa jinsi ya kupinga Ibara.

Kilio kingine kwa UKAWA ni kura za Mtandao. Wabunge wa Zanzibar wa kura za mtandao ni 8 ambao nimedokezwa kuwa wote wamepiga kura za NDIYO kwa Ibara nyingi. Hawa hawakuwa kwenye mamlaka ya UKAWA. Hakika imekuwa ni pigo kubwa kwa UKAWA kwani kelele zote walizopiga, hatimaye wameangukia pua.


DONDOO MUHIMU ZA ZOEZI LA UPIGAJI KURA

* Idadi ya Wabunge ni 629
* Wabunge wa Tanzania Bara ni 419
Wabunge wa Zanzibar ni 210
*Akidi inayotakiwa kwa Tanzania Bara ni 280 na Zanzibar ni 140
Waliopiga kura Bungeni kwa Tanzania Bara ni 332 na Zanzibar ni 143
*Kura za HAPANA Bungeni ni 6 kwa Zanzibar na 1 kwa bara. Kati ya hizo 6 za Zanzibar, 2 zinabaki hivyo kwa vile wabunge wameondoka Dodoma. Hizo 4 zilizobaki zitabadilika baada ya wahusika kupiga kura upya hapo kesho
* Kura za Mtandao za Zanzibar nje ya kura 2 za UKAWA zipo 8 na zote ni za NDIYO. Kwa upande wa Bara, za Mtandao zipo 18 ambazo zote ni za NDIYO
* Wabunge wa UKAWA waliopiga kura za Mtandao ni wawili na wote ni wa Zanzibar Wote wamepiga kura ya NDIYO.
* Mwanasheria wa Zanzibar kapiga kura ya NDIYO kwa Ibara nyingi. Hili nalo ni pigo kwa UKAWA kwani waliamini kuwa wamefanikiwa kumshawishi ajitoe kwenye Kamati ya uandishi na asipige kura
* Idadi ya Wabunge wote waliopiga kura ni 503. Kati ya hao, wabunge 350 ni wa Tanzania Bara na 153 ni wa Zanzibar
* Kura zote za Ndiyo ni 496. Kati ya hizo, za bara ni 349 na Zanzibar ni 147.
* Kura zote za HAPANA ni 7. Kati ya hizo ya bara ni 1 na Zanzibar ni 6
* Ziada ya kura baada ya kupatikana akidi kwa kura za NDIYO ni 69 kwa Tanzania Bara na 7 kwa Zanzibar.

NB: TAKWIMU HIZI SI RASMI. Nimezikokotoa kulingana na data nilizopata kwa wadau mbalimbali. Matokeo kamili yatatangazwa kesho.

Kwa TAKWIMU hizi, ni kilio kwa UKAWA na CHEREKO KWA CCM. Mwisho, niwaombe UKAWA kukubali matokeo kwani hila zote walizofanya zimeshindikana. Pia watambue kuwa mchakato wa kutunga katiba mpya ndani ya mfumo wa vyama vingi ni mapambano na daima chama chenye dola ndicho kinachotoa muelekeo wa Muundo wa Katiba Inayopendekezwa. Wingi wa wabunge wa CCM na mikakati imara na makini imefanikisha upatikanaji wa Katiba iliyojaa matumaini ya Watanzania wengi. Tumpambe Sitta Mauaaaaaaaaaaaa!



 
"The world wide impossible politics are possible in Tanzania".

The reason is that,majority of the electorate in this country is comprised of "irresponsible citizen" and this is why the rulers do whatever they want without fear of being voted out of power.

By mimi.
 
lazima mjifariji na mtafute kila namna kuupamba uongo

Tunachojua ni kuwa katiba imebuma kura 7 plus za siri za hapana plus Mwanasheria wa Zanzibar
 
Ondoka na hesabu zako za kichina, hata wakirudia, waliotoka kura zao bado ni hapana, imekula kwenu nalabuk
Mkuu, hata wakipiga tena kura ya HAPANA akidi imepatikana kiulaini kwani kutakuwa na ziada ya kura 7
 
wananchi nao tukiikataa wataunda kamati ya mashauriano tena? mbona watu tumeshajua ukweli ni upi 6 analazimisha nyekundu kuwa nyeupe, aya tunakusubili babu kilembwe uje.
 
Hahahahahaaaaa. UKAWA bana. Eti wanamfungia mbunge asipige kura
 
yaani. CHABURUMA umewezaje kutabiri zile kura zoote za siri ni za ndio??
kweli we ni zaidi sheh yahaya...
_na je umewezaje kutabiri kuwa waliopiga HAPANA live woote watabadili msimamo yao na hasa ikiwa wananchi wameshawaona live kuwa walipiga za HAPANA???
_nakushauri acha kuchukulia mambo kirahisi hivyo mkubwa
 
Last edited by a moderator:
Chabruma , kura za siri zilikuwa ngapi za ndio na Hapana ?
Kura zote za Siri zimepiga kura ya NDIYO. Japo kuna baadhi ya wabunge wamepiga kura ya HAPANA kwa baadhi ya Ibara ila kwa jumla yake za Siri zote zimepiga kura ya NDIYO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom