Tathmini ya bajeti iliyopita itusaidie kuandaa bajeti mpya ya 2012/13

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
Jana niliishiwa nguvu kidogo baada ya kugundua kuwa bajeti iliyopita ya wizara ya uchukuzi utekelezaji wake haufiki ata 50% kwa mujibu wa kamati ya bunge.

Sasa najiuliza fedha ambazo zilizotengwa zilienda wapi na zimefanya nini?
I am sure kuna ufujaji apo.

Na mwaka huu tunaambiwa bajeti itakwenda as far as 15 trillion kuna haja ya kufanya tathmini ya bajeti iliyopita ili tujue tuliitekeleza kwa % ngapi then ambayo hayakutekelezwa yaingizwe kwa bajeti mpya!
 
Kama tunatenga bajeti then utekelezaji wake haufiki hata asilimia hamsini yanini kutenga hiyo bajeti bora tuliache liende tu haina maana watu wazima na kengele zao wanakaa pale bungeni wanapanga na kujadili bajeti ambayo haitekelezeki, ni kuharibu kodi zetu. hii nchi kila ukigusa kiongozi ni Dr mara Profesa lakini malimbukeni matupu....
 
Budjet is a financial plan and a list of all planned expenses and revenues.
Can you fail 50% to implement what you planned for?
Then there must be something very serious missing in your forecasted expenses and revenue!
 
Kwa ujumla sio miuondombinu tu karibu taasis zote imekuwa hivyo. Hii imepelekea ofisi mbalimbali kuendeshwa kiubabaishaji tu. Wenyewe watakuambia hali hii imechangiwa na wahisani kugoma kutoa hela mpaka mafisadi wawajibishwe na kuyumba kwa uchumi duniani-ni upuuzi mtupu. Utakumbuka Mkapa alikuwa anapunguza utegemezi wa bajeti yetu kutoka kwa wahisani taratibu kila mwaka na alikuwa ana akiba ya hela kwa miaka miwili hivyo hata kama masuala yakiteteleka serikali haikuathurika sana lakini kwa JK sera yake ni kuomba omba. Sasa mjomba huyu kwanza yeye kwake kila kitu ni kipaumbele, anataka sifa aonekane bajeti ni kubwa wakati hana uwezo wa kukusanya hizo fedha, hana uwezo wa kusimamia rasilimali. Matokeo yake anatupa bajeti makaratasi. Bora kuwa na bajeti ndogo na vipaumbele vichache kila mwaka na kuhakikisha bajeti inaenda kwa 100% kuliko anavyofanya sasa.
 
Back
Top Bottom