Tathmini: Uongozi wa Rais Samia Suluhu ndani ya mwaka mmoja

Anaandika, Robert Heriel

Taikon wa Fasihi.

Hii ni tathmini ya uongozi wa Mama Samia Suluhu tangu alipoingia madarakani mwaka Jana 2021 mwezi machi, zikiwa zimebaki siku chache kukamilika mwaka mmoja.

Tathmini hii ni kulingana na mtazamo wangu, Uelewa wangu, na vile mambo niyaonavyo.

Dondoo
1. Utangulizi
2. Kujitambulisha na kuchagua upande
3. Upimwaji
4. Kushindwa
5. Kushinda
6. Nini KIFANYIKE.
7. Hitimisho.

1. Samia Suluhu Hassan ni Rais wa sita tangu nchi yetu ipate Uhuru
Licha ya sifa zingine zote, lakini kitu pekee ambacho kitabaki Kama historia Kwa taifa letu kupitia yeye ni kuwa ndiye Rais wakwanza mwanamke katika nchi yetu.

Kuingia Kwa Samia Suluhu katika nafasi ya Urais hakukupokelewa vizuri na waliowengi ukizingatia kuwa Nchi yetu Kama zilivyonchi za Afrika ni nchi yenye Dhana ya Mfumo dume. Na siajabu mpaka hivi leo wapo watu ambao bado hawamkubali Raia Samia kutokana na jinsia yake.

Rais Samia anayokazi ya ziada kuitengeneza njia ya wanawake wengine wa nchi yetu Kwa kufanya mazuri ili kuondoa dhana kuwa mwanamke hawezi kushika nafasi ya juu ya kiuongozi ndani ya nchi.

Hata hivyo Kama nikiambiwa niseme ukweli, nitasema kuwa, Kwa nchi yetu hii bado Dhana potofu kuhusu mfumo dume ipo, hivyo hata Samia angefanya mazuri Kwa kiwango gani, bado kwenye jamii watu wakiambiwa wapige Kura anaweza asipewe Kura na waliowengi.
Hivyo ni muhimu elimu ya jinsia izidi kutolewa ili kuleta Uelewa na mipaka ya kijinsia jamii iweze kuelewa manufaa yake.

2. Rais Samia aliweza kujitambulisha baada ya kutambulishwa na chama chake
Kujitambulisha ni hatua ya awali kabisa katika suala la uongozi na Maisha. Kujipambanua yeye ni Nani, falsafa yake ya maisha, na matazamio yake.

Katika kujitambulisha Mama Samia mara kadhaa alikuwa akieleza kuwa yeye ni Rais mwenye umbile(jinsia) ya kike. Jambo ambalo angelisema mara moja au mbili lingeeleweka lakini kulirudia rudia ilifanya wengine tuanze kuona kuna tatizo, sio ajabu niliwahi andika makala inayomshauri aachane na kuelezea jinsia yake kwani hiyo haileti tafsiri nzuri. Hiyo ilikuwa miezi sita ya Mwanzo, baadaye akaacha nafikiri ni baada ya kuanza kuzoea na ku-master kazi yake mpya.

Mama Samia Katika kuchagua upande Kama nikimtathmini na nikiambiwa niseme ukweli wowote, nakiri kuwa amechagua upande wa KIBEPARI, ambayo kimsingi ndio msingi wa biashara katika Karne yetu.

Upande wa kibepari unapendelewa zaidi na matajiri, hivyo Kwa kuuchagua upande huo ni dhahiri kuwa biashara nyingi zitaneemeka na matajiri wataongezeka.

Hata hivyo hatuweza kukataa kuwa Gap baina ya Tajiri na Masikini tunalitarajia kuongezeka Kwa miaka mitatu mpaka mitano inayokuja ikiwa Hali itaendelea kama ilivyosasa.

Mama Samia Katika kuchagua upande wa kibepari, anapendelea demokrasia ya kiuchumi zaidi kuliko ya Kisiasa, na Kama itakuwepo demokrasia ya Kisiasa basi isiguse maslahi ya kiuchumi.

Demokrasia ya kiuchumi itaruhusu nchi kufunguka Kwa wenye mitaji na mitandao au waliopo kwenye mifumo. Lakini wale wasio na kimoja Kati ya hivyo basi habari Yao itakuwa imekwisha.

Mfumo wake ni mzuri Kwa kiasi kikubwa kwani angalau kundi Fulani litanufaika na kunufaisha makundi mengine.

3. Kupimwa ni sehemu muhimu baada ya kujitambulisha
Mama Samia alipimwa Kwa namna kadhaa, iwe na watu wampendao au watu wamchukiao.
Kupimwa ni kupimwa tuu. Lengo la kupokea ni kumfanya mpimwaji aonyeshe uwezo wake.
Katika matokeo Kwa mujibu wangu, matokeo yananiambia kuwa amefaulu kwa 60% tu.

πŸ“Ndani ya chama chake amefaulu Kwa 100% Kwa kudhibiti wanaoitaka nafasi yake.
πŸ“ Vyama vingine vya Siasa amefaulu Kwa 40%. Kesi ya Mbowe na wenzake ni sehemu ya changamoto iliyomshushia maksi.
πŸ“ Uchumi amepata 60% kilichomkosesha naksi nyingi ni kupanda bei Kwa baadhi ya bidhaa.
πŸ“ Uhusiano kimataifa amefaulu 100%
πŸ“ Uhusiano wa kujenga umoja ndani ya nchi amefaulu 50% zingine amekosa kutokana na nature ya nchi yetu hasa ya Mfumo dume, pia baadhi ya makundi(Kama yapo) kuhusu sukuma gang Vs Msoga gang. Haya ameyakuta hivyo yeye sio chanzo Ila yatahesabiwa kwani anawajibu WA kuyaondoa.

πŸ“ Ulinzi na Usalama ndani ya nchi na mipaka amefaulu Kwa 90% hizo Asilimia 10 alizokosa ni kutokana na kuripotiwa baadhi ya matukio ya mauaji na kuungua Kwa masoko. Kwenye kuungua Kwa masoko bado watu hawaridhishwi na matokeo ya uchunguzi.

Kwenye matukio mengine ya uhalifu Kama mauaji huku wanajitahidi kufuatilia na hii inafanya watu wasione kwamba serikali inahusika na matukio hayo, tofauti na awamu iliyopita.

πŸ“ Mahusiano ya vyombo vya Dola na Raia amepata 70%. Hizo 30 alizokosa ni kutokana na baadhi ya Askari wasio waaminifu kujiingiza katika uhalifu na kulichafua Jeshi la polisi. Matukio ya polisi kuhusishwa na Rushwa na matukio ya mauaji pia yamefanya baadhi ya wananchi kukosa Imani na vyombo vya Dola.

Serikali inapaswa ifanye marekebisho na kulisuka upya Jeshi la polisi.

πŸ“ Uhuru wa vyombo vya habari na wananchi kutoa maoni 90%. Kwa sasa vyombo vya habari na watu wanauhuru WA kutoa maoni na ndio maana sasa tunaweza sikia habari nzuri na mbaya Maeneo yote nchini.

4. Katika maisha kupo kushindwa pia
πŸ“Raia Samia Suluhu ameshindwa kudhibiti ongezeko la bei Kwa baadhi ya bidhaa hasa vyakula.

πŸ“ Mama Samia ameshindwa kufanya maridhiano na wanachama wa CHADEMA. Kila mmoja hataki kujishusha.

πŸ“ Mama Samia Ameshindwa kuitisha uchunguzi wa matukio ya mauaji na utekaji yaliyotokea yaliyo Kwa mrengo wa Kisiasa. Hata hivyo Kwa vile ndio kwanza mwaka mmoja, ngoja tuwe na subira huenda ataunda tume ya uchunguzi.

πŸ“ Mama ameshindwa kuzuia pesa ya kuingiziwa umeme ibaki Ile Tsh 20,000 na kuipeleka zaidi ya laki tatu Kwa baadhi ya Maeneo.

5. Kushinda na Kufanikiwa
πŸ“ Mama Samia amefanikiwa kuifungua nchi hasa Kwa wale wenye macho, mitaji na connection.

πŸ“ Mama Samia amefanikiwa kuleta mahusiano mazuri kimataifa na wawekezaji.

πŸ“ Mama Samia amefanikiwa kutoa wazo na kulisimamia kuhusu ujenzi wa madarasa na limefanikiwa Kwa kiwango kikubwa.

πŸ“ Mama Samia amejitahidi kuleta USAWA wa kijinsia ingawaje bado anakazi ya ziada.

πŸ“. Mama Samia amefanikiwa kuzimudu Siasa za demokrasia Kwa kuachia Uhuru wa kukosolewa na kushambuliwa.

πŸ“ Mama Samia amefaniliwa mpaka hivi sasa kudhibiti maadui wa awali ndani ya chama chake.

πŸ“ Mama Samia amefanikiwa kutokuwa na migogoro na chuki Kwa wafanyabiasha wakubwa. Hii italeta Uhuru katika uwekezaji kwani matajiri watakuwa huru kutumia mitaji Yao.

πŸ“ Mama Samia amejitahidi kuonyesha uhalisia wa nchi yetu kuwa ni masikini na bila mikopo hakuna tutakachofanya zaidi ya kuchelewa tuu.

πŸ“ Mama Samia amefanikiwa kutokuwa na adui mwenye chuki iliyopitiliza ukilinganisha na Mtangulizi wake.
Adui zake wanachuki za wastani na hawajamkamia kikamilifu.

πŸ“ Mama Samia amefanikiwa kuongoza Kwa Asilimia kubwa pasipo kutumia mihemko na maneno machafu Kwa kuponda na kukashifu watu wengine.

6. Nini kifanyike
πŸ“ Katiba mpya ni MUHIMU mengine yafuate.

7. Hitimisho
Binafsi uongozi wa Mama Samia licha ya kuwa na mapungufu ya hapa na pale lakini ni wazo wengi wetu tuna Amani.
Hayo mengine ni mapungufu ya kibinadamu ambayo hayajavuka mipaka.

Ninaufurahia uongozi wa Samia, maboresho machache yajikite kwenye elimu ya utambuzi Kwa wananchi, Wananchi wasiwe tegemezi Kwa serikali, kila kitu wasiilaumu serikali Bali wawe Sehemu ya kutatua kero na changamoto zinazoikabili nchi.

Kingine, masuala ya uvyama Vyama ndio yanaharibu nchi. Pawepo na Sera kuu za nchi Kwa miaka kumi kumi, na kila chama kiandike ilani yake kupitia Sera za nchi na kuzitekeleza pindi kishikapo Dola.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Umechambua kwelikweli ndugu ... Ila ukweli utabaki pale pale kila kiongozi atakaye pata nafasi ya kuongoza Taifa kwa ngazi ya Rais

Mimi na wananchi jukumu letu kubwa ni kuniombea na kuwaelimisha wananchi wenzetu dhana kamili ya uongozi na wajibu wa serikali kwa wananchi wake pamoja na wajibu wa raia kwa serikali yao ili kusukuma kwa pamoja gurudumu la maendeleo na kuilinda Aman, umoja na mshikamano, bidii na uzalendo .
 
Umechambua kwelikweli ndugu ... Ila ukweli utabaki pale pale kila kiongozi atakaye pata nafasi ya kuongoza Taifa kwa ngazi ya Rais Mimi na wananchi jukumu letu kubwa ni kuniombea na kuwaelimisha wananchi wenzetu dhana kamili ya uongozi na wajibu wa serikali kwa wananchi wake pamoja na wajibu wa raia kwa serikali yao ili kusukuma kwa pamoja gurudumu la maendeleo na kuilinda Aman, umoja na mshikamano, bidii na uzalendo .
Mama anaupiga mwingi sana kiukweli

Screenshot_20220322-101627.png

Screenshot_20220322-101518.png

Screenshot_20220322-093437.png

Screenshot_20220319-161330.png

Screenshot_20220319-072518.png

Screenshot_20220317-181419.png
 
Samia ni Rais dhaifu ambae ataacha historia mbaya Tanzania kuliko marais wote.

Ni rais ambae atajuta maisha yake yote kuwa Rais.
 
Hakuna Katiba ya kuwaingiza chadema madarakani,hiyo haipo na haitakuwepo.

Serikali itafanya marekebisho yatakayowanufaisha wananchi tuu.
Una akili fupi kupindukia.Ninyi ndiyo huwa nawaita kuwa ni Mapaka.

Wananchi walivyotoa maoni kwenye tume ya warioba kuwa wanahitaji katiba mpya walikuwa ni chadema?

Mzee warioba aliekusanya maoni hayo alikuwa ni chadema?Kikwete alieanzisha mchakato ule alikuwa ni chadema?
 
Anaandika, Robert Heriel

Taikon wa Fasihi.

Hii ni tathmini ya uongozi wa Mama Samia Suluhu tangu alipoingia madarakani mwaka Jana 2021 mwezi machi, zikiwa zimebaki siku chache kukamilika mwaka mmoja.

Tathmini hii ni kulingana na mtazamo wangu, Uelewa wangu, na vile mambo niyaonavyo.

Dondoo
1. Utangulizi
2. Kujitambulisha na kuchagua upande
3. Upimwaji
4. Kushindwa
5. Kushinda
6. Nini KIFANYIKE.
7. Hitimisho.

1. Samia Suluhu Hassan ni Rais wa sita tangu nchi yetu ipate Uhuru
Licha ya sifa zingine zote, lakini kitu pekee ambacho kitabaki Kama historia Kwa taifa letu kupitia yeye ni kuwa ndiye Rais wakwanza mwanamke katika nchi yetu.

Kuingia Kwa Samia Suluhu katika nafasi ya Urais hakukupokelewa vizuri na waliowengi ukizingatia kuwa Nchi yetu Kama zilivyonchi za Afrika ni nchi yenye Dhana ya Mfumo dume. Na siajabu mpaka hivi leo wapo watu ambao bado hawamkubali Raia Samia kutokana na jinsia yake.

Rais Samia anayokazi ya ziada kuitengeneza njia ya wanawake wengine wa nchi yetu Kwa kufanya mazuri ili kuondoa dhana kuwa mwanamke hawezi kushika nafasi ya juu ya kiuongozi ndani ya nchi.

Hata hivyo Kama nikiambiwa niseme ukweli, nitasema kuwa, Kwa nchi yetu hii bado Dhana potofu kuhusu mfumo dume ipo, hivyo hata Samia angefanya mazuri Kwa kiwango gani, bado kwenye jamii watu wakiambiwa wapige Kura anaweza asipewe Kura na waliowengi.
Hivyo ni muhimu elimu ya jinsia izidi kutolewa ili kuleta Uelewa na mipaka ya kijinsia jamii iweze kuelewa manufaa yake.

2. Rais Samia aliweza kujitambulisha baada ya kutambulishwa na chama chake
Kujitambulisha ni hatua ya awali kabisa katika suala la uongozi na Maisha. Kujipambanua yeye ni Nani, falsafa yake ya maisha, na matazamio yake.

Katika kujitambulisha Mama Samia mara kadhaa alikuwa akieleza kuwa yeye ni Rais mwenye umbile(jinsia) ya kike. Jambo ambalo angelisema mara moja au mbili lingeeleweka lakini kulirudia rudia ilifanya wengine tuanze kuona kuna tatizo, sio ajabu niliwahi andika makala inayomshauri aachane na kuelezea jinsia yake kwani hiyo haileti tafsiri nzuri. Hiyo ilikuwa miezi sita ya Mwanzo, baadaye akaacha nafikiri ni baada ya kuanza kuzoea na ku-master kazi yake mpya.

Mama Samia Katika kuchagua upande Kama nikimtathmini na nikiambiwa niseme ukweli wowote, nakiri kuwa amechagua upande wa KIBEPARI, ambayo kimsingi ndio msingi wa biashara katika Karne yetu.

Upande wa kibepari unapendelewa zaidi na matajiri, hivyo Kwa kuuchagua upande huo ni dhahiri kuwa biashara nyingi zitaneemeka na matajiri wataongezeka.

Hata hivyo hatuweza kukataa kuwa Gap baina ya Tajiri na Masikini tunalitarajia kuongezeka Kwa miaka mitatu mpaka mitano inayokuja ikiwa Hali itaendelea kama ilivyosasa.

Mama Samia Katika kuchagua upande wa kibepari, anapendelea demokrasia ya kiuchumi zaidi kuliko ya Kisiasa, na Kama itakuwepo demokrasia ya Kisiasa basi isiguse maslahi ya kiuchumi.

Demokrasia ya kiuchumi itaruhusu nchi kufunguka Kwa wenye mitaji na mitandao au waliopo kwenye mifumo. Lakini wale wasio na kimoja Kati ya hivyo basi habari Yao itakuwa imekwisha.

Mfumo wake ni mzuri Kwa kiasi kikubwa kwani angalau kundi Fulani litanufaika na kunufaisha makundi mengine.

3. Kupimwa ni sehemu muhimu baada ya kujitambulisha
Mama Samia alipimwa Kwa namna kadhaa, iwe na watu wampendao au watu wamchukiao.
Kupimwa ni kupimwa tuu. Lengo la kupokea ni kumfanya mpimwaji aonyeshe uwezo wake.
Katika matokeo Kwa mujibu wangu, matokeo yananiambia kuwa amefaulu kwa 60% tu.

πŸ“Ndani ya chama chake amefaulu Kwa 100% Kwa kudhibiti wanaoitaka nafasi yake.
πŸ“ Vyama vingine vya Siasa amefaulu Kwa 40%. Kesi ya Mbowe na wenzake ni sehemu ya changamoto iliyomshushia maksi.
πŸ“ Uchumi amepata 60% kilichomkosesha naksi nyingi ni kupanda bei Kwa baadhi ya bidhaa.
πŸ“ Uhusiano kimataifa amefaulu 100%
πŸ“ Uhusiano wa kujenga umoja ndani ya nchi amefaulu 50% zingine amekosa kutokana na nature ya nchi yetu hasa ya Mfumo dume, pia baadhi ya makundi(Kama yapo) kuhusu sukuma gang Vs Msoga gang. Haya ameyakuta hivyo yeye sio chanzo Ila yatahesabiwa kwani anawajibu WA kuyaondoa.

πŸ“ Ulinzi na Usalama ndani ya nchi na mipaka amefaulu Kwa 90% hizo Asilimia 10 alizokosa ni kutokana na kuripotiwa baadhi ya matukio ya mauaji na kuungua Kwa masoko. Kwenye kuungua Kwa masoko bado watu hawaridhishwi na matokeo ya uchunguzi.

Kwenye matukio mengine ya uhalifu Kama mauaji huku wanajitahidi kufuatilia na hii inafanya watu wasione kwamba serikali inahusika na matukio hayo, tofauti na awamu iliyopita.

πŸ“ Mahusiano ya vyombo vya Dola na Raia amepata 70%. Hizo 30 alizokosa ni kutokana na baadhi ya Askari wasio waaminifu kujiingiza katika uhalifu na kulichafua Jeshi la polisi. Matukio ya polisi kuhusishwa na Rushwa na matukio ya mauaji pia yamefanya baadhi ya wananchi kukosa Imani na vyombo vya Dola.

Serikali inapaswa ifanye marekebisho na kulisuka upya Jeshi la polisi.

πŸ“ Uhuru wa vyombo vya habari na wananchi kutoa maoni 90%. Kwa sasa vyombo vya habari na watu wanauhuru WA kutoa maoni na ndio maana sasa tunaweza sikia habari nzuri na mbaya Maeneo yote nchini.

4. Katika maisha kupo kushindwa pia
πŸ“Raia Samia Suluhu ameshindwa kudhibiti ongezeko la bei Kwa baadhi ya bidhaa hasa vyakula.

πŸ“ Mama Samia ameshindwa kufanya maridhiano na wanachama wa CHADEMA. Kila mmoja hataki kujishusha.

πŸ“ Mama Samia Ameshindwa kuitisha uchunguzi wa matukio ya mauaji na utekaji yaliyotokea yaliyo Kwa mrengo wa Kisiasa. Hata hivyo Kwa vile ndio kwanza mwaka mmoja, ngoja tuwe na subira huenda ataunda tume ya uchunguzi.

πŸ“ Mama ameshindwa kuzuia pesa ya kuingiziwa umeme ibaki Ile Tsh 20,000 na kuipeleka zaidi ya laki tatu Kwa baadhi ya Maeneo.

5. Kushinda na Kufanikiwa
πŸ“ Mama Samia amefanikiwa kuifungua nchi hasa Kwa wale wenye macho, mitaji na connection.

πŸ“ Mama Samia amefanikiwa kuleta mahusiano mazuri kimataifa na wawekezaji.

πŸ“ Mama Samia amefanikiwa kutoa wazo na kulisimamia kuhusu ujenzi wa madarasa na limefanikiwa Kwa kiwango kikubwa.

πŸ“ Mama Samia amejitahidi kuleta USAWA wa kijinsia ingawaje bado anakazi ya ziada.

πŸ“. Mama Samia amefanikiwa kuzimudu Siasa za demokrasia Kwa kuachia Uhuru wa kukosolewa na kushambuliwa.

πŸ“ Mama Samia amefaniliwa mpaka hivi sasa kudhibiti maadui wa awali ndani ya chama chake.

πŸ“ Mama Samia amefanikiwa kutokuwa na migogoro na chuki Kwa wafanyabiasha wakubwa. Hii italeta Uhuru katika uwekezaji kwani matajiri watakuwa huru kutumia mitaji Yao.

πŸ“ Mama Samia amejitahidi kuonyesha uhalisia wa nchi yetu kuwa ni masikini na bila mikopo hakuna tutakachofanya zaidi ya kuchelewa tuu.

πŸ“ Mama Samia amefanikiwa kutokuwa na adui mwenye chuki iliyopitiliza ukilinganisha na Mtangulizi wake.
Adui zake wanachuki za wastani na hawajamkamia kikamilifu.

πŸ“ Mama Samia amefanikiwa kuongoza Kwa Asilimia kubwa pasipo kutumia mihemko na maneno machafu Kwa kuponda na kukashifu watu wengine.

6. Nini kifanyike
πŸ“ Katiba mpya ni MUHIMU mengine yafuate.

7. Hitimisho
Binafsi uongozi wa Mama Samia licha ya kuwa na mapungufu ya hapa na pale lakini ni wazo wengi wetu tuna Amani.
Hayo mengine ni mapungufu ya kibinadamu ambayo hayajavuka mipaka.

Ninaufurahia uongozi wa Samia, maboresho machache yajikite kwenye elimu ya utambuzi Kwa wananchi, Wananchi wasiwe tegemezi Kwa serikali, kila kitu wasiilaumu serikali Bali wawe Sehemu ya kutatua kero na changamoto zinazoikabili nchi.

Kingine, masuala ya uvyama Vyama ndio yanaharibu nchi. Pawepo na Sera kuu za nchi Kwa miaka kumi kumi, na kila chama kiandike ilani yake kupitia Sera za nchi na kuzitekeleza pindi kishikapo Dola.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Umekuwa na open mind, japo kwa mbali naona unaupenda ubepari zaidi na ndiyosababu ya kutoa mchango ambao ni positive.

Hata hivyo ni ukweli usiopingika, Mh. Rais amefanya kazi kwa ufanisi wa juu na pia kutoa demokrasia ya kweli kwa watu wa makundi yote.

Mh. Rais ameonyesha wazi ni mwanamke pekee anayependa kuinua wanawake wenzake tofauti kubwa sana na viongozi wengi wanawake wanapofanikiwa. Hili halija surface sana.

Na unaona kabisa upande wa kumwinua mwanamke anapata asilimia 100 ukilinganisha na wanawake ambao wameshika nafasi katika nchi hii, hongera sana Rais wetu na kila laheri katika juhudi zako hizi njema.

Kitu pekee ambacho napingana na Mh. Rais ni kuendelea kuwafanya watanzania kujiona hawawezi kitu chochote, huko tulishatoka na ni bahati mbaya sana alishindwa kuendeleza imani hiyo na badala yake akageuka 360 degeree kinyume na mtangulizi wake, kwahilo hapana.

Angeboresha namna tu na siyo kugeuka na kuturudisha ambapo ki mawazo tulishaanza kujiona tunaweza.
 
Umekuwa na open mind, japo kwa mbali naona unaupenda ubepari zaidi na ndiyosababu ya kutoa mchango ambao ni positive.

Hata hivyo ni ukweli usiopingika, Mh. Rais amefanya kazi kwa ufanisi wa juu na pia kutoa demokrasia ya kweli kwa watu wa makundi yote.

Mh. Rais ameonyesha wazi ni mwanamke pekee anayependa kuinua wanawake wenzake tofauti kubwa sana na viongozi wengi wanawake wanapofanikiwa. Jili halija surface sana. Na unaona kabisa upande wa kumwinua mwanamke anapata asilimia 100 ukilinganisha na wanawake ambao wameshika nafasi katika nchi hii, hongera sana Rais wetu na kila laheri katika juhudi zako hizi njema.

Kitu pekee ambacho napingana na Mh. Rais ni kuenslea kuwafanya watanzania kujiona hawawezi kitu chochote, huko tulishatoka na ni bahati mbaya sana alishindwa kuendeleza imani hiyo na badala yake akageuka 360 degeree kinyume na mtangulizi wake, kwahilo hapana. Angeboresha namna tu na siyo kugeuka na kiturudisha ambapo ki mawazo tulishaanza kujiona tunaweza.

Upo sahihi Mkuu. Ile mushi alitoa masomo ambaye Rais amepata A kulingana na mtazamo wake, nikamwambia nasubiri masomo aliyopata F.

Kama atashindwa nitayaandika hapa
 
Back
Top Bottom