Tathmini uchaguzi mdogo udiwani;Kata nyingi kwenda CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tathmini uchaguzi mdogo udiwani;Kata nyingi kwenda CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by utaifakwanza, Nov 13, 2017.

 1. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2017
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,059
  Likes Received: 1,614
  Trophy Points: 280
  Tathmini na utafiti makini uliyofanywa kuhusu uchaguzi mdogo wa kuziba mapengo ya madiwani mbalimbali unaoendelea hivi sasa nchini ni kwamba, CCM itazoa kata nyingi kuliko vyama vingine huku ikifuatiwa kwa mbaaali na CHADEMA halafu CUF na ACT.
  Utafiti huo umebaini kuwa sababu zinazoipa CCM kushinda kata nyingi ni kasi ya utendaji kazi wa Rais Magufuli ambayo inawakonga nyoyo watanzania na hivyo kuwa na imani kubwa na chama hicho. mambo makubwa yaliyofanywa na serikali ya CCM chini ya rais Magufuli ndani ya miaka hii miwili ni kutumbua majipu katika maeneo mbalimbali ya utumishi wa umma, kukomesha ufisadi na rushwa, kuziba mianya ya uvujaji rasilimali za nchi maeneo ya madini, kurudisha nidhamu ya utumishi wa umma na kusimamia ipasavyo falsafa ya hapa kazi tu.
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2017
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 35,219
  Likes Received: 11,266
  Trophy Points: 280
  Endelea kupima upepo tu, Kimara wanawasubili kwa hamu tu ili muyajuwe machungu ya waliobomolewa nyumba zao.
   
 3. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2017
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,519
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Aiseeee toa figures basi pia ueleze kata zipi zilikua chama gani na sasa zitachukuliwa na chama gani. Utafiti huwa hauongei kama nyimbo za pwani.
   
 4. lumbi lumbi

  lumbi lumbi Member

  #4
  Nov 13, 2017
  Joined: May 30, 2017
  Messages: 83
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Tafiti gani hii hakuna figures, tupe statistics kwamba unayoyasema haya hapa. Unabwabwaja tu.
   
 5. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2017
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,688
  Likes Received: 1,364
  Trophy Points: 280
  Acha porojo basii, miaka yote ccm huwa inazoa kata nyingi kuliko vyama vyingine katika chaguzi ndogo, hii inajulikana. Hayo masifa mengine ni ngonjera tu, eti kukomesha ufisadi na rushwa!
   
 6. NDULUMESO

  NDULUMESO JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2017
  Joined: Nov 21, 2013
  Messages: 211
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  Ccm nadhani inaweza kushinda kata nyingi kweli lakini si kwa sababu hizo ulizozitaja mkuu.
  Labda sana sana kwasababu ya goli la mkono na pia kuifanya Tbc kuwa kama yao kusifia mambo ya serikali hii na kwakuwa ina coverage kubwa kufanya wananchi wengi hususani wa vijijini kuamini hayo wanayoaminishwa.
  Vinginevyo ngoja tusubiri tuone
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2017
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 35,219
  Likes Received: 11,266
  Trophy Points: 280
  Wanachi wenye njaa wanaweza kuaminishwa na TBC kwamba wameshiba pilau la kuku?
   
 8. M

  Magimbi JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2017
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 1,044
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  Kama watatangazwa walioshinda na si WASHINDI basi kazi itakuwa pevu. Kikubwa wasimamizi wasiwe na hofu na wakumbuke majukumu yao bila uwoga. CCM tunashinda mara nyingi inajulikana....
   
 9. Jaby'z

  Jaby'z JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2017
  Joined: Jan 15, 2013
  Messages: 2,234
  Likes Received: 2,353
  Trophy Points: 280
  tuliza wenge kaa chini
   
 10. Mdudu halisi

  Mdudu halisi JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2017
  Joined: May 7, 2014
  Messages: 2,415
  Likes Received: 3,663
  Trophy Points: 280
  Jambo jingine kubwa alilofanya Magufuli ni kuchota mabilioni ya fedha bila idhini ya Bunge kisha kwenda kujenga uwanja wa ndege huko kijijini kwao ambako hakuna hata mtu anayeweza kumudu gharama za usafiri wa ndege.
   
 11. M

  MAGALLAH R JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2017
  Joined: Nov 1, 2014
  Messages: 262
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Huu sio utafiti bali ni mawazo tu ya mtoa mada
   
 12. M

  Martin George JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2017
  Joined: Jun 4, 2017
  Messages: 1,508
  Likes Received: 1,301
  Trophy Points: 280
  Kama kweli umefanya utafiti basi wewe ni kanjanja, haihitaji utafiti kujua CCM itashinda kata 37 na UKAWA 6!!
   
 13. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2017
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,412
  Likes Received: 2,242
  Trophy Points: 280
  UJINGA ULIOTUKUKA, FANYA NAMNA YA KUPIGA KURA HAPA UTAPATA MAJIBU, KUANGUKA KWA CCM NI UTENDAJI WA MWENYEKITI WAO, OPPOSITE IS TRUE!
   
 14. M

  Martin George JF-Expert Member

  #14
  Nov 13, 2017
  Joined: Jun 4, 2017
  Messages: 1,508
  Likes Received: 1,301
  Trophy Points: 280
  Tena siyo mawazo ni ndogo!
   
 15. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #15
  Nov 13, 2017
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 6,651
  Likes Received: 7,516
  Trophy Points: 280
  Hili neno hili...

  "Utendaji wa Rais"
   
 16. Msukuma_De_Great

  Msukuma_De_Great JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2017
  Joined: Nov 26, 2016
  Messages: 880
  Likes Received: 638
  Trophy Points: 180
  Cheo cha pole pole kinakufaa
   
 17. makarihodari

  makarihodari Member

  #17
  Nov 13, 2017
  Joined: Oct 30, 2017
  Messages: 40
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  Yaani magufuli kwa miaka miwili ametuaminisha kuwa mafisadi ni seth,rugemalila,na viongozi wa club ya simba na hakuna kiongozi yeyote wa ccm aliyewahi kujihusisha na ufisadi toka tupate uhuru.
  Ccm hoiyeee
   
 18. Y

  YusuJo JF-Expert Member

  #18
  Nov 13, 2017
  Joined: Apr 10, 2016
  Messages: 528
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 80
  Kimara hata kabla ya kuvunjiwa sidhani kama waliwahi kuwa watu wa CCM kwa hiyo hakuna la ajabu wakiendelea na msimamo wao
   
 19. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #19
  Nov 13, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,174
  Likes Received: 9,992
  Trophy Points: 280
  Yaani bila ya kujipendekeza huwezi kuwa mwana CCM bora! Hapa Iringa inawezekana CCM ikapigwa mbili bila, sijui kwingine.
   
 20. mafinyofinyo

  mafinyofinyo JF-Expert Member

  #20
  Nov 13, 2017
  Joined: Nov 29, 2012
  Messages: 2,985
  Likes Received: 1,263
  Trophy Points: 280
  Labda muibe kura kama kawaida yenu
   
Loading...