Uchaguzi 2020 Tathmini: Tamasha la CCM lilikuwa la hovyo na aibu tupu

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,035
Kwanza kabisa waandaaji hawakuwa na uhakika wa kile walichokua wanataka kukifanya! Hawakujua agenda au maudhui ya kusanyiko hilo, matokeo yake ilikua kama gulio la wahuni au tuite panya road.

Pili, hakukua na nidhamu, lugha za kihuni (Mbasha, Halafu wewe ni bangi sana), kulikuwa na kupigana hadharani tena wakiwa "live"! Maana yake ni kwamba hawa walikua wahuni, wasiojitambua, wafia tumbo, wasio na uhakika na kesho yao.

Tatu, ni miongoni mwa matamasha ya hovyo kupata kutokea Tanzania, kiasi kwamba isingekua tukio la hao Wahuni kufanyiana vurugu basi hakuna NTU angejua kabisa uwepo wa Tamasha hili. Yaani hata mdundiko wa mtaani una afadhali.

Nne, walishindwa kabisa kupeleka " meseji" waliyotumwa waipeleke maana hata wao wenyewe hawakua na uhakika na meseji yenyewe!

Tano, kuna taarifa kuwa tukio zima lilitawaliwa na vitendo vya kihalifu, kuibiana, kashfa, ngono zembe na mengineyo.

Takukuru ya CCM inabidi wapitie mapato na matumizi ya hii shughuli.

Ubora wake, walifanikiwa kulipa vijana waliowaita Wasanii kwa pesa ndogo ndogo na wengine kukopwa kwa ahadi ya kutumika kwenye kampeni (kuwa compasated) basi hilo tu.

Mwisho, next time tumieni Waandaji ambao sio Wapigaji (hata hivyo sidhani kama kwa CCM unaweza kuwapata, I stand to be corrected).

Nawasilisha, ongezeni mapungufu yao ili kuwasaidia.
 
Kinachonishangaza ni kuona chama kikiwa kimya dhidi ya tukio la kihuni lililofanywa na Adam Mchomvu. Naomba chama kuanzia Sasa, kimuadhibu Mchomvu kwa kuidhalilisha brand ya CCM na siku nyingine watumie washereheshaji wanaojielewa. R. I. P Efraim Kibonde.
 
Kwanza kabisa waandaaji hawakua na uhakika wa kile walichokua wanatgaka kukifanya! Hawakujua agenda au maudhui ya kusanyiko hilo, matokeo yake ilikua kama gulio la wahuni au tuite panya road.

Pili, hakukua na nidhamu, lugha za kihuni (Mbasha, Halafu wewe ni bangi sana), kulikua na kupigana hadharani tena wakiwa "live"! Maana yake ni kwamba hawa walikua wahuni, wasiojitambua, wafia tumbo, wasio na uhakika na kesho yao.

Tatu, ni miongoni mwa matamasha ya hovyo kupata kutokea Tanzania, kiasi kwamba isingekua tukio la hao Wahuni kufanyiana vurugu basi hakuna NTU angejua kabisa uwepo wa Tamasha hili. Yaani hata mdundiko wa mtaani una afadhali.

Nne, walishindwa kabisa kupeleka " meseji" waliyotumwa waipeleke maana hata wao wenyewe hawakua na uhakika na meseji yenyewe!

Tano, kuna taarifa kuwa tukio zima lilitawaliwa na vitendo vya kihalifu, kuibiana, kashfa, ngono zembe na mengineyo.

Takukuru ya CCM inabidi wapitie mapato na matumizi ya hii shughuli.

Ubora wake, walifanikiwa kulipa vijana waliowaita Wasanii kwa pesa ndogo ndogo na wengine kukopwa kwa ahadi ya kutumika kwenye kampeni (kuwa compasated) basi hilo tu.

Mwisho, next time tumieni Waandaji ambao sio Wapigaji (hata hivyo sidhani kama kwa CCM unaweza kuwapata, I stand to be corrected).

Nawakilisha, ongezeni mapungufu yao ili kuwasaidia.....
Hapo kwenye kupitiwa mahesabu nilikuwa na kula nimepaliwa
 
Back
Top Bottom