Tathmini ndogo tu ya ahadi zilizotimizwa tayari na CHADEMA Arusha kupitia kwa G. Lema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tathmini ndogo tu ya ahadi zilizotimizwa tayari na CHADEMA Arusha kupitia kwa G. Lema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Imnyagi, Jan 11, 2012.

 1. I

  Imnyagi Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni kwa ajili ya wale ambao ni wapenda maendeleo tu tukiweka siasa na majungu pembeni kwanza tujadiliane kidogo kama mbunge wako ametimiza ahadi kwa kiasi gani kupitia chama chake.

  Ni mara chache sana ninaweza kuwaamini wanasiasa kwa ahadi zao kutokana na tabia halisi walizo nazo, mara nyingi hawako wakweli bali wanakuwa na ubabaishaji wa hali ya juu na ahadi nyingi ambazo kuzitekeleza ni mpaka tena waulizwe kwa kushituliwa na wananchi wao au viongozi dini zao ili kuwaepusha na dhambi za uongo.

  Hapa nitajaribu kufupisha kwa kadiri ya uwezo wangu kuhusu mambo ambayo kwangu mimi kama mwananchi ninayependa maendeleo ninavutiwa kwayo ambayo nimeyajua baada ya kuhudhuria mikutano kadhaa ya CDM.tangu 5 Jan.2012.

  Godbless Lema Mbunge ni zaidi ya vile watu wengi wananvyomuona au kumsema kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari na ninakiri kuwa sikuwa nampa alama kubwa sana kutokana na watu kumponda kuwa ni muhuni, hajasoma na anayependa fujo na maandamano siku zote badala ya kushughulika na kero za jimbo lake.

  Katika mikutano yake ambayo mingi amekuwa akiifanya kuanzia 05 Jan.2012 na sasa kupita kila kata hakuna mahali ambapo amekuwa akihutubia na mtu akapita na usafiri wake bila kusimama na kumsikiliza kwa dakika 10 mpaka 15 au hata wengine kukaa kabisa mpaka mkutano uishe kutokana hotuba zake ambazo zina ukweli mtupu kutokana na mifano halisi ya mambo yanavyoonekana kwa sasa hapa nchini.

  Hapa nitaweka baadhi ya ahadi zake ambazo ameshatimiza kwa ujasiri mkubwa tena bila hata kushirikiana na halmashauri ya jiji la Arusha kwa sababu ya mgogoro wa meya ambapo amesema kama angekuwa na meya ambaye ameshinda ki halali tungekuwa mbali zaidi ya hapo.

  Chadema Arusha inasomesha wanafunzi wa shule za Sekondary zaidi ya 400 inawalipia ada pamoja na matibabu yaani wamewapatia mpaka wafadhili waliowakatia bima hizo za maisha na watoto hao sasa wako kidato cha pili mwaka huu na namba hiyo iliathirika kwa kiwango fulani baada ya baadhi ya wazazi zaidi ya sitini kupewa form za kujaza pamoja na picha za watoto wao passport size kukosa hata shilingi 3000 za kupigia picha walikuja kugundua hilo baada ya kuwafuatilia wazazi hao.

  Aliahidi Kujenga hospitali ya wanawake na watoto na ndani ya mwaka mmoja ameshapata kiwanja maeneo ya Burka Estate ambacho ni kikubwa na kinatosha kujenga hospitali kubwa ya kisasa kabisa na kiwanja hicho kina thamani zaidi ya milioni 400. Wakati kuna waziri wa maliasili na utalii kafanya miradi ya shilingi milioni 500 akiwa na nafasi kubwa ya kufanya mambo mengi kuliko 500 ml.

  Alikataa bungeni kupewa bajaji kwa ajili usafiri wa wanawake akijenga hoja kuwa hivi bajaji hizo ambazo wanataka kutoa kwa ajili ya wanawake wagonjwa zinaweza kweli kumpelekea mama Salma Kikwete au mke wa waziri yeyote yule Hospital kama akizidiwa? Na kwamba hayo magari ya thamani kubwa waliyojigawia yanafanana na hali ya maisha ya wanyonge? Na Job Ndungai akamwonya aache ukorofi wake naye alinyamaza na kuwaambia hatachukua vibajaji hivyo bali atawatafutia wananchi wake usafiri utakaowafaa kwendea hospitali na ndipo marafiki wachache walipochanga gari kwa ajili ya wagonjwa (Ambulance) ambapo baada ya kusikia tena amekwenda magereza kwa hiari ili kupinga uonevu wa Polisi dhidi ya raia kwa maana kama yeye Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anashambuliwa hovyo na Polisi na kuja kuwakamata wachadema ofisi kwake je watoto wa kiswahili si ndiyo wamejaa magereza na huko magereza hakuna watoto wa uzunguni au Njiro! Baada ya marafiki na wapenda chadema waliposikia ujasiri wake huo waliongeza gari lingine la wagonjwa na hivyo kufanya kuwa na magari mawili ya wagonjwa na siyo vibajaji tena kama ccm walivyopendekeza.

  Alishapewa mchango Trekta jipya ambalo lina Thamani ya zaidi ya milioni 35 na linafanya mradi kulima shamba kubwa kwa ajili ya uzalishaji na biashara ambapo angeweza kulichukua Trekta hilo na kumpelekea baba yake akalitumie.

  Kuhusu michango mbalimbali ambayo amekwisha kuitoa magereza hospitalini makanisani misikitini kwa yatima na wajane hataki hata kuizungumzia maana hiyo ni kama sadaka kwa Mungu yeye na familia yake.

  Nimejaribu kuweka ahadi ambazo Chadema imezifanya mpaka sasa hapa Arusha ila huyu Mbunge ukimsikiliza hauwezi kumchoka hakuna kitu ambacho anakiongea hakina maana au ni cha kipumbavu kila anachokiongea ukilinganisha na ukweli hauhitaji elimu kubwa sana ili kumwelewa kuwa mtu huyu anasimamia nini hasa kuhusu haki ya wanyonge wa chini ambapo amesema yeye atahakikisha anakuwa sauti ya wanyonge popote na amewataka watanzania kutoka kwa ujasiri na kudai haki zao za msingi bila kuogopa polisi na alisema kuwa ccm wamebakiwa na bunduki tu maana hata hao waliozishika ni CDM. Ndiyo maana walipata kura nyingi kwenye maeneo ya polisi na wanajeshi hivyo ametahadharisha ccm.kuwa macho maana siku zao zimekwisha kwa mambo wanayoyafanya.

  Ningetamani kama kila mtanzania mwenye akili timamu angepata nafasi ya kumsikiliza huyu Mbunge G. Lema angebadilisha mtazamo wake kwa mifano na matendo amabyo tayari ameshafanya kwenye medani za kisiasa na kwa mtindo huu nina uhakika wananchi wengi watajiunga na Chadema maana mikutano yake yote ambayo nimeweza kuhudhuria anajaza watu na saa zinavyokwenda ndipo inazidi kuongezeka baada ya wengine kutoka makazini na kujiunga kwenye mikutano yake.
   
 2. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ikiwa hayo yote ni kweli hongera zake! Maana CCM wamekaa miaka yote lakini barabara za Arusha ni mbaya sana! Hebu wamelize migogoro madiwani wapatikane wasimamie halmashauri Jiji letu lisonge mbele!
   
 3. L

  Luiz JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazeni buti makamanda wanainchi tumejenga sana imani na nyie big up sana MP, lema.
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndiyo Chadema bana! Na Lema ndiye mbunge wa chadema.Nimekuwa nikijiuliza hivi nusu ya wabunge wangetoka chadema ingekuwaje? Hakika tungekuwa tunaogelea kwenye dimbwi la maendeleo.
   
 5. t

  true JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Mkuu umelisahau moja la msingi sana na ndo kubwa zaidi, kawafungua uelewa na utambuzi wa haki zao kwa wana ARUSHA na baadhi ya Watanzania pia.

  Tunahitaji chama na viongozi wenye kutimiza ahadi zao...
   
 6. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Vp alizungumza kama anachukua posho au hachukui?
   
 7. j

  j707 New Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Glema ni mfano wa kuigwa hongera zake
   
 8. I

  Imnyagi Member

  #8
  Jan 12, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo amelisema kwamba amejivunia kuwaunganisha wananchi katika kudai haki zao bila woga na mpaka sasa Arusha ni mfano wa kuigwa kwa ujasiri wa wananchi wake na yeye analitahmini hilo ndiyo maana anapita kuwashukuru wananchi na kuwaomba waendelee kuwa na Imani naye na CDM. Kwa ujumla mpaka kieleweke kifupi ameongea mambo mengi ya maana na yenye ukweli mtupu na hayahitaji kamusi ili uweze kuelewa ana maanisha nini. Sema siwezi kuweka hapa yote.
   
 9. I

  Imnyagi Member

  #9
  Jan 12, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ameliongelea ki utaalam na mapana sana na alisema yeye aliongezewa posho bila kujua mpaka mke wake akawa anashangaa na alisema hiyo inatumika sana bungeni kama aina ya rushwa kwa wabunge ili kuwafumba macho na waangalie maisha yao ili wawasahau wananchi wa kawaida na pia kusiwe na kelele au kumpigia Rais kura ya kutokuwa na imani naye pale mambo yanapokwenda mrama.
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu Imnyagi,
  Bravo sana kwa coverage hii!
  Watu wengine hatuelewagi hadi tuandikiwe...thanks alot!
   
 11. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Hapo ni bla bla tu, tulishafanyia analysis ya kila kitu. Kati ya hayo uliyoyataja, kipi kilikuwa kwenye kampeni zake? Alitoa ahadi nyingi sana na hamna hata moja ameitekeleza. Umeleta hapa vitu ambavyo ni irrelevant, ambavyo hata mtu wa kawaida asiye mbunge anaweza kuvifanya.

  Kusomesha hao wanafunzi 400 tulifanya calculations ni around 16m kwa mwaka, hela ambayo ni ndogo sana kwa mbunge plus wafadhili wanaomsaidia.

  Jipangeni tena mje na hoja za kumtetea na wala si habari za kutetea.

  Halafu huyu mbunge mwambieni pia aache kujitangaza sana kupitia hapa JF na kwenye media nyingine. Kuna wabunge wanafanya mambo mazito na makubwa ya kimaendeleo lakini hawapigi domo.
   
 12. I

  Imnyagi Member

  #12
  Jan 12, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pj Tuko wengi ambao tulikuwa tunakihukumu CDM. Na mbunge huyu hasa pale ambapo tulipoona uongozi wa juu unamuunga mkono lakini ki ukweli huyu jamaa ana hoja za nguvu na za msingi kwa mtu yeyote mwenye akili timamu wakiwemo wenyewe ccm na vyama vingine na ndiyo maana viongozi wao wanarudisha kadi na kujiunga CDM.
   
 13. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hongera zake, Arusha Development Fund inafanya vyema!
   
 14. I

  Imnyagi Member

  #14
  Jan 12, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rejao labda una hoja ya msingi tujaribu kukumbushana aliahidi nini? Maana mimi sikuwepo kwenye Kampeni ambacho hajakifanya? na katika kuvitelekeza ndani ya mwaka mmoja baadhi tu ya ahadi zake na zingine za ziada kwa maana hiyo basi atakuwa amevuka lengo ndani ya mwaka mmoja kuliko baadhi ya wengine kwa maana ameyafanya yale yaliyoko ndani ya uwezo wa chama chake tena bila kupewa ushirikiano na halmashauri na vyombo vya usalama nathubutu kusema amevuka malengo, hivyo nakushauri uje na hoja ya msingi na siyo Siasa ya chuki za vyama.

  CDM. Kusomesha watoto hao kwa tathimin ndogo tu bado wanastahili pongezi zao kwani kuna watoto wangapi kwenye majimbo ya chama tawala tena hata mawaziri wenye dhamana kubwa na bado kuna watoto wenye shida kiasi cha watoto kusoma kwa masaa manne manne kwa ili kubadilisana sare za shule na hawasaidiwi hata kwa kwa milioni moja halafu wewe unaona 16ml. ni ndogo!? Tumia akili na uje na hoja ya msingi.

  Kama ni ushabiki wa kisiasa kwa sasa CDM. Kinakubalika mpaka vijijini maana watu wanaeleweshwa na kuwaelewa na wana imani
  na CDM. Kwa sasa.

  Waswahili husema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni hakuna mtu anayempigia Lema na chama chake kampeni hapa tunaongea ukweli halisi kwa yale tunayoyaona yamekwishafanyika na ndiyo maana nikasema hii hoja ni kwa ajili ya wapenda maendeleo siyo kama unavyodai wewe nakuhisi uko kisiasa zaidi na kupinga maendeleo yaliyokwisha kufanywa CMD.
   
 15. M

  Maengo JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  God bless you Lema.....
   
 16. R CHUGGA

  R CHUGGA Senior Member

  #16
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mpe hoja huyo inaonekana kabisa analeta siasa za magamba hapa wakati wa2 wanaongelea maendeleo tupunguze ushabiki kama jambo lina ukweli lazima lisemwe!
  Rejao ameahidiwa kuongezewa posho yake na magamba so tumwache ajitahidi na kazi aliyotumwa na wachumia tumbo wenzake!
   
 17. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi kusomesha watoto yatima kwenye shule za kata tena kwa kusaidiwa na na wafadhili unaweza kujisifia kweli? Mbona Kafulila anasomesha watoto 300, Vick Kamata anasomesha watoto 400.

  Shule za kata kila mtu anaweza kusomesha ada ya mtoto mmoja ni 1500 x 400=600.000 tu
   
 18. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Bora umesema. Watu ni wepesi sana kusahau ahadi za kimaendeleo alizoahidi wakat wa kampeni, wanashupalia vitu Lema anavyofanya ambavyo hata raia wa kawaida anaweza kuifanya.
  Kwa mashabiki wa Lema, mnatakiwa mfanye analysis ya jiji la Arusha kabla na baada ya Lema kiuchumi, kisiasa na kijamii.
   
 19. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Imnyagi,
  Sina haja ya kujaza server ya JF kwa kurudia rudia ahadi za Lema ambazo zipo kwenye thread nyingi sana hapa.

  Nieleze, kiuchumi lema amefanya nini? Uchumi wa Arusha sasa upoje?
  Kisiasa..siasa za Arusha zipoje? Ameshindwa hata kuwamanage madiwani wake na kufanya nao kazi pamoja. Utulivu upo?
  Kijamii..social responsibility yake iko poor kabisa. Hiyo kusomesha watoto everybody can do. Hospital za Arusha zina hali gani? Ushafika hapo kalolen? Mount Meru je? Shule za Arusha zina hali gan? Maisha ya wakaz wa Arusha yapoje?
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Nimepitia hii yote sijaona sehemu yoyote Lema, katumia pesa yake kama mbunge..

  Hizo Ambulance mbili umesema zimetolewa na wafadhili wake, ilo la kusomesha watoto yatima shule za kata, limetolea ufafanuzi na Rejao na Mchuzi wa Bata.

  Lema alikataa bajaji halafu akachukua milioni 90 kununulia gari lake binafsi.

  Posho na mikopo anayochukuwa bungeni unajua kazi yake? Anajenga jumba la kifahari maeneo ya Njiro, vipi kaishawambia?

  Mbona ujaweka zile ahadi za Machinga Complex mbili.

  Njoo na tathimini ingine hii umechemka hakuna kitu.
   
Loading...