MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavipa vyama vyote vya siasa nchini kufanya shughuli za kisiasa ikiwa ni pamoja na kufungua matawi maeneo mbali mbali, kukagua uhai wa chama, kuwashawishi wananchi ili kupata uungwaji mkono.
Vyama vya siasa pia vina haki ya kikatiba kutoa elimu kuhusu utekelezaji wa sera mbali mbali unaofanywa na serikali, vyama vya siasa vinavyo wajibu hata wa kutoa elimu ya uraia, vyama vya siasa vinavyo wajibu wa kotoa elimu ya katiba kwa wananchi.
Kabla ya kufikia uchaguzi mwingine ni lazima chama cha siasa kihakikishe kua kinajiandaa kwa kutafuta wapiga kura katika maeneo mbali mbali ya nchi ili itakapofika muda wa kampeni basi itakua ni rahisi kuwafikia wafuasi wake.Kuna idadi ya wanachama ambao chama kinatakiwa kua nao ili kukidhi matakwa ya kisheria kua na sifa ya kua chama cha siasa.
Ikumbukwe kua kila chama kina misingi yake kuanzia ngazi za chini, katika ile misingi hua kuna wasimamizi wake ambao ndio viongozi wasimamizi wa ustawi wa chama husika. Lazima viongozi wa kitaifa wapate muda wa kupitia katika misingi ya vyama vyao ili kuendelea kuwajengea uwezo wasimamizi wa misingi hiyo. Kwahiyo muda wa kufanya siasa hauna kikomo wala muda maalum, ni nafasi tu ya chama chenyewe kulingana na uwezo wake.
Kazi nyingine ya vyama vya siasa kwa sababu katiba inaruhusu kuunda serikali kivuli kwa chama chenye wabunge wengi baada ya chama tawala, ni lazima viikosoe serikali iliyoko madarakani pale panapohitaji kukosolewa. Mataifa yote yenye mfumo wa vyama ni kawaida sana kwa upinzani kuikosoa serikali.
Isichukuliwe kama kukosolewa serikali na upinzani ni kukwamisha maendeleo! Sijawahi kusikia kwa taifa la Marekani limekwama kimaendeleo sababu tu kwamba vyama vya upinzani vilikua vikifanya mikutano. Nchi za wenzetu siasa inafanyika na maendeleo ni makubwa sana tu.Suala ni kuangalia ni wapi tulijikwa na kurekebisha kasoro zilizopo lakini sio kuzuia vyama vya upinzani kufanya siasa.
Hivyo basi, ni jambo jema sana kuviachia vyama vya kisiasa kuendelea na majukumu yake ya kisiasa kwa sababu chama chenyewe ndio siasa, na huu ndio mzizi wa kujenga mshikamano na umoja wa watu katika taifa linalotaka kuendelea.Hii ndio inayoitwa demokrasia ya vyama vingi.Haya yote yanawezekana Kama vuguvugu la vyama vingi silingekuepo ndani ya taifa letu.
Nchi yoyote duniani ambayo haijatulia kisiasa(Political instability) vyanzo vyake kwa kiasi kikubwa hutokana na ukosefu wa demokrasia na hapo ndipo vikundi vyenye nia ovu hapata nafasi ya kupenya na kusababisha vurugu.