Tathmini: Kesho bora ya Tanzania inategemea uwepo wa Katiba Mpya

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,828
Mabibi na mabwana ni ukweli usiopingika kuwa kesho yetu iliyo bora zaidi inategemea sana uwepo wa katiba mpya. Kwa hali tuliyofikia kunahitajika zaidi mustakabala mpya wa utangamano. Ni wazi kuwa hayupo mmoja ambaye kwa dhati yake asiyekwazika kabisa kwa lolote na katiba iliyopo labda tu, kwa kutokujua au kuwa mnufaika wa moja kwa moja na mapungufu ya katiba hii tuliyo nayo sasa.

Si Mataga, si CCM, si CUF, si ACT, si Chadema nk. Ni chama gani kwa dhati yao wanaishabikia katiba hii kuwa ndiyo mustakabala bora kabisa tunayoistahili?

Si manguli wa siasa wakiwamo kina Bashiru, kina Pole pole, Warioba, Butiku, nk wote hao wangependa uwepo wa katiba nyingine. Wala si hii ambayo ni wazi kuwa wengine katika hawa bila ya kutarajia kwa katiba hii, wamejikuta wakivunjika mioyo ghafla na kweli kweli. Hawakujua kuwa walistahili katiba mpya mapema, lakini sasa wanajua. Jambo la kheri tu.

Kundi pekee linaloishabikia katiba iliyopo kwa dhati (kuacha mambumbu) ni dogo sana na hili ni lile tu linalonufaika madarakani moja kwa moja kibinafsi kutokana na katiba iliyopo. Hawa wala si wengi kuvihimili vishindo vya watakao mabadiliko.

Kizingiti pekee kilichopo kuifikia azma hii inayotakikana na wengi ni kukosekana kwa umoja. Ni vipi Mataga wa CCM na CCM yenyewe iweze kushirikiana na vyama vingine kama Chadema kudai katiba mpya? Hilo haliwezekani japo wote Chadema na CCM wakiwamo Mataga wanaihitaji mno katiba mpya yenye kuwapa wote uhakika zaidi wa kesho.

CCM kushirikiana na wengine kwenye hili, ni rahisi zaidi kwa Ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Ni wazi kuwa wajinga ndiyo waliwao na ndiyo iliyo hali halisi!

Kupatikana kwa katiba mpya itakayo wanufaisha wote wakiwamo Chadema, kwa msimamo wa CCM ni bora isipatikane tu. Ya kuwa ni heri hali iliyopo iendelee kuliko kwa namna yoyote kuja pia kuwanufaisha Chadema. Ndivyo ilivyo hasa kwa kuzingatia kuwa pamoja na mapungufu yaliyopo, bado pia CCM ndiye aliye mnufaika zaidi.

Anayebakia kwenye harakati hizi za kupata katiba mpya na ya haki, ni Chadema na wachache wengine lakini si CCM. Kwa hali hii upatikanaji wa katiba mpya si rahisi sana, lakini si kuwa eti haiwezekani.

Kunahitajika kujizatiti vilivyo. Kutambua nini kinahitajika, kuwatambua washirika, kuwatambua maadui na kutambua nini cha kufanya kuhusu wote hao na lini.

Hakuna harakati zisizokuwa kuwa na wahanga. Ni muhimu kutambua viwango vyote vya uhanga unaoweza kutokea kutokana na jitihada za namna hii na kuona namna ya kuzi assimilate, accommodate au kuzifidia.

Kwamba litakayemkuta akale tu na wakwao, hiyo si katika zama hizi na kwa niaba na maslahi ya wote!

Hadi hapa tulipo leo, uzoefu uliopo unatosha sana.

Kutegemea kuwa pana mnufaika mmoja mahali kwa utashi wake tu atakuja siku moja akatupa katiba muafaka isiyokuwa na mapendeleo yoyote, haiwezi kuwa option.

Hali kadhalika kutegemea kuwa kwa kudra ya mwenyezi Mungu, siku moja mambo yatabadilika yenyewe ghafla na kuwa sawa, hilo pia haliwezi kuwa option.

Kulielewa tatizo kwa mapana, marefu na kimo chake ni mwanzo mwema wa kulitafutia suluhu ya kudumu.
 
Hii Katiba ya ccm ya mwaka 1977 ni tamu sana kwa wale tu wanao nufaika kwa namna moja au nyingine (walio ndani ya mfumo). Ukiwa nje ya huo mfumo, aisee hii Katiba ni mbovu mpaka basi!

Na kama huamini, muulize Lowasa wa ccm na yule wa ukawa uone majibu yake! Au muulize Sumay wa Ccm na yule wa Chadema! Au Membe wa Ccm na yule wa ACT Wazalendo! Hakika majibu yao yatakuwa tofauti kabisa kuhusu Katiba Mpya.
 
Hii Katiba ya ccm ya mwaka 1977 ni tamu sana kwa wale tu wanao nufaika kwa namna moja au nyingine (walio ndani ya mfumo). Ukiwa nje ya huo mfumo, aisee hii Katiba ni mbovu mpaka basi!

Na kama huamini, muulize Lowasa wa ccm na yule wa ukawa uone majibu yake! Au muulize Sumay wa Ccm na yule wa Chadema! Au Membe wa Ccm na yule wa ACT Wazalendo! Hakika majibu yao yako tofauti.

Mkuu nakubaliana na wewe lakini mwulize Bashiru, Pole pole na hata Majaliwa. Si hao tu hata Mataga na waumini wa awamu ile wakwambie.

Wote wanataka katiba mpya. Ila wanapokumbuka "Chadema" naye atanufaika? Heee! Wanaona mbona ni heri ya nusu shari!

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Baada ya miaka 60 ya Uhuru, Watanzania tunashindwa kudai Katiba bora ya kutuunganisha site katika kujenga nchi yetu kwa kuikabidhi CCM maamuzi ya iwapo tudai/kuhitaji Katiba ya Tanzania?CCM wakifahamu kabisa kuwa hatuna umoja wanatuaminisha kwamba Katiba siyo kipaumbele chao nasi tunalazimika kukubali.Wamefikia hata viongozi kuanzia vitongoji,vijiji,kata na wabunge wanapita bila kupingwa nasi tunakubali!
Kiujumla tunasikitisha mno,sifahamu tatizo letu ni uoga ama hofu au ujinga!Katiba ni Haki yetu Wananchi na siyo siasa za vyama.
 
Chakula kuiva ni lazima kitokote sawa sawa. Uliyoyaorodhesha yote ndiyo kutokota kwenyewe huko.

Chadema wanabeba dhima kubwa zaidi kwenye kuipigania katiba mpya kwa sababu wanayo nia, wamedhamiria na wako organized zaidi.

Kama ilivyo kwenye mada ni muhimu wawatambue washirika, maadui na kiwango cha wahanga watakaotokea.

Katiba mpya ipo karibu sasa kuliko wakati mwingine wowote kabla.
 
Tatizo linalokwamisha katiba mpya katika nchi hii ni dhana kwamba hii ajenda mpaka impendezee rais aliyeko madarakani. That's all.

Kwa swala la katiba mpya, kwa kuwa ccm waliishagundua kitambo kwamba hii katiba ya sasa ndio uhai wao kamwe hawawezi kukubali ibadilishwe ila njia pekee ya kuwalazimisha ni shinikizo kali kutoka nje, bila ya hivyo, tusahau kabisa.
 
Mkuu kama ilivyo katika mada hili si la kutegemea nia ya njema ya rais au mtu yeyote:

IMG_20210620_184906_989.jpg

Hili liko upande zaidi wa CHADEMA wenye nia, dhamira na organization advantage dhidi ya wengine.

Bado shinikizo la kutosha la ndani linatosha sana. Hili ni letu zaidi kuliko wa nje.
 
Chakula kuiva ni lazima kitokote sawa sawa. Uliyoyaorodhesha yote ndiyo kutokota kwenyewe huko.

Chadema wanabeba dhima kubwa zaidi kwenye kuipigania katiba mpya kwa sababu wanayo nia, wamedhamiria na wako organized zaidi.

Kama ilivyo kwenye mada ni muhimu wawatambue washirika, maadui na kiwango cha wahanga watakaotokea.

Katiba mpya ipo karibu sasa kuliko wakati mwingine wowote kabla.
Nakubaliana nawe kuwa CHADEMA wanabeba dhima kubwa kwa sababu ya dhamira yao ya msingi ya Democracy.Ila tatizo ni propaganda za CCM kwamba Wananchi hawahitaji Katiba Bali maendeleo ambayo hata hivyo hayaonekani kwa sababu ya Katiba mbovu.
CCM wanatumia vitisho kuwahadaa Watanzania kwamba wanaodai Katiba ni wabinafsi.Wanawazubaisha Wananchi kwenye kuzindua madaraja na makongamano&fiesta.Kila shughuli ya kitaifa wanavaa jezi zao na kuburudika na singeli za kina Zuchu bila kuwapa Wananchi fursa ya elimu ya uraia.
Tuanzishe harakati za kudai Katiba bila kuhusisha itikadi za vyama.
 
Kuna vyama karibu 19 lakini hitaji la Wananchi karibu 60M lisubiri liamuliwe na chama kimoja, it's a shame.

Hitaji lolote la watu wengi lahitaji coordination. Haliwezi kudaiwa haphazardly.

Je ni CCM ata coordinate hili? Ni CUF, ACT au TLP?

Huo ndiyo ulio ukweli.
 
Mkuu nakubaliana na wewe lakini mwulize Bashiru, Pole pole na hata Majaliwa. Si hao tu hata Mataga na waumini wa awamu ile wakwambie.

Wote wanataka katiba mpya. Ila wanapokumbuka "Chadema" naye atanufaika? Heee! Wanaona mbona ni heri ya nusu shari!

Au nasema uongo ndugu zangu?
Tatizo la wananchi wa tanzania wanaona bora kusiwe na katiba mpya kuliko katiba ikaja na kuwafaidisha wapinzani. Hii mentality ni ya kimaskini sana
 
Tatizo la wananchi wa tanzania wanaona bora kusiwe na katiba mpya kuliko katiba ikaja na kuwafaidisha wapinzani. Hii mentality ni ya kimaskini sana

Mkuu wala si wananchi wa Tanzania hao:

"Tatizo la 'wananchi wa tanzania' wanaona bora kusiwe na katiba mpya kuliko katiba ukaja ..."

Hao ni CCM tu mkuu!

Hii ni kama ilivyo angaziwa kwenye mada na kunukuliwa pia hapa chini:

IMG_20210620_200421_312.jpg
 
Nakubaliana nawe kuwa CHADEMA wanabeba dhima kubwa kwa sababu ya dhamira yao ya msingi ya Democracy.Ila tatizo ni propaganda za CCM kwamba Wananchi hawahitaji Katiba Bali maendeleo ambayo hata hivyo hayaonekani kwa sababu ya Katiba mbovu.
CCM wanatumia vitisho kuwahadaa Watanzania kwamba wanaodai Katiba ni wabinafsi.Wanawazubaisha Wananchi kwenye kuzindua madaraja na makongamano&fiesta.Kila shughuli ya kitaifa wanavaa jezi zao na kuburudika na singeli za kina Zuchu bila kuwapa Wananchi fursa ya elimu ya uraia.
Tuanzishe harakati za kudai Katiba bila kuhusisha itikadi za vyama.

Mkuu kama ilivyo elezwa kwenye mada. Watu wote wakiwamo CCM wanaoihitaji katiba mpya. Tofauti iliyoko ni kuwa CCM wana maslahi tofauti na ndiyo maana kwao pamoja na hitaji lao, lakini ni bora inajieleza iliyopo. Hii ndiyo inayopelekea janja janja zote unazoziongelea wewe.

Kwamba:

"Tuanzishe harakati za kudai Katiba bila kuhusisha itikadi za vyama."

Nani atakaye ratibu na kulisukuma hilo? Unadhani linaweza kutokea spontaneously kama mvua?

Chadema wako katika nafasi nzuri zaidi ya wengine wote ya kukinukisha hadi akili ikawaingia walioko madarakani kuuona umuhimu. Ndipo haya unayoyasema yanaweza kuzaliwa.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Nakubaliana nawe kuwa CHADEMA wanabeba dhima kubwa kwa sababu ya dhamira yao ya msingi ya Democracy.Ila tatizo ni propaganda za CCM kwamba Wananchi hawahitaji Katiba Bali maendeleo ambayo hata hivyo hayaonekani kwa sababu ya Katiba mbovu.
CCM wanatumia vitisho kuwahadaa Watanzania kwamba wanaodai Katiba ni wabinafsi.Wanawazubaisha Wananchi kwenye kuzindua madaraja na makongamano&fiesta.Kila shughuli ya kitaifa wanavaa jezi zao na kuburudika na singeli za kina Zuchu bila kuwapa Wananchi fursa ya elimu ya uraia.
Tuanzishe harakati za kudai Katiba bila kuhusisha itikadi za vyama.

Nisiache kuongezea taasisi nyingine iliyoshiba inayoweza pia kulisukuma suala hili vilivyo ni hawa jamaa (Shura ya ma Imam):

IMG_20210620_101733_140.jpg

Hawa jamaa nao wamewiva na wako organized. Wakijiridhisha kuwa wanachokitaka ni halali nao si haba.

Hata hivyo kwa mujibu wa mama Samia, ukitaka kwenda mbali nenda na wenzako!
 
Kabla ya kuanza kuidai katiba inabidi tupate Elimu kwanza, umuhimu wa katiba na mapungufu ya katiba iliyopo ndio tuendelee la sivyo ni ngumu kidogo, nionavyo mie.
 
Kabla ya kuanza kuida katiba inabidi tupate Elimu kwanza, umuhimu wa katiba na mapungufu ya katiba iliyopo ndio tuendelee la sivyo ni ngumu kidogo, nionavyo mie.

Ni kweli kuwa elimu ni muhimu sana.

Kama ilivyo kwenye mada, ukiondoa wachache wanufaikao moja kwa moja (na kibinafsi tu) wengine waishabikiao katiba hii ni kwa kutokujua tu!

Katika lundo la wasiojua wamo hasa hawa kutokea awamu ya tano:

Kwa jinsi walivyo brainwashed kuwasubiri hao kuelewa inaweza kuwa ni rahisi zaidi kuwasubiria wamasai kuukumbatia uvaaji wa suruali.

La msingi ni kuwa mengi yaliyo fyongo na yanayolalamikiwa na wengi yanatokea kutokana na ubovu wa wazi wa katiba iliyopo:

1. Angalia chaguzi zilivyo kosa haki.
2. Angalia utitiri wa viongozi wa serikali wasio na tija wala kuwa na ridhaa ya wananchi.
3. Angalia maamuzi ya uendeshaji nchi yalivyo pokwa toka kwa wananchi na kuwa ni ya kikundi cha watu kwa maslahi yao.
4. Angalia keki ya taifa inavyoliwa na kutembea katika watu na familia zile zile.
5. Angalia vyombo vilivyo paswa kutulinda vilivyo geuka kuwa vya kutukandamiza.
6. Angalia mzigo wa kodi toka kwa watawala wanavyobebeshwa wananchi. Nini uhalali wa Mawaziri, wabunge na wa namna hiyo kutokulipa kodi stahiki ila sisi?
7. Angalia uozo wa kina SABAYA na kuwa waliendelea kuwapo kama majembe kweli kweli ya serikali yetu kwa mujibu wa katiba.
8. Angalia kimuhe muhe kilichompata mama, katiba iliyopo tu ilipowekwa majaribuni.
9. Vipi haya mambo ya ajira? Kwa nini kusiwepo utaratibu mpya wa watu kutokutumikia serikalini na kwenye taasisi zake bila ukomo ili kuhimiza kujiajiri na kutoa nafasi mpya za ajira?
10. Kwa nini wanasiasa wasistaafu sanjari na kada zingine zote?
11. Nk nk.

Tuidai katiba mpya wakati pia elimu ikitolewa. Kwa hakika, hadi hapa wametuchelewesha sana!

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Nakubaliana nawe kuwa CHADEMA wanabeba dhima kubwa kwa sababu ya dhamira yao ya msingi ya Democracy.Ila tatizo ni propaganda za CCM kwamba Wananchi hawahitaji Katiba Bali maendeleo ambayo hata hivyo hayaonekani kwa sababu ya Katiba mbovu.
CCM wanatumia vitisho kuwahadaa Watanzania kwamba wanaodai Katiba ni wabinafsi.Wanawazubaisha Wananchi kwenye kuzindua madaraja na makongamano&fiesta.Kila shughuli ya kitaifa wanavaa jezi zao na kuburudika na singeli za kina Zuchu bila kuwapa Wananchi fursa ya elimu ya uraia.
Tuanzishe harakati za kudai Katiba bila kuhusisha itikadi za vyama.

Kwa taarifa yako katiba ni jambo la kisiasa, unawezaje kutenga hisia ama itikadi za kisiasa. Kwa dhati ya moyo wako, ukiacha wanasiasa hasa wa upinzani, ni taasisi gani au mtu mwingine unamuona akidai katiba mpya kwa nguvu zake zote? Hebu tuambie ww, ukiacha hizo itikadi za kisiasa, ni platform gani tunaweza kukutana na kudai hiyo katiba mpya?
 
Back
Top Bottom