Tathmini: Hofu ya Zanzibar kumezwa kwenye Muungano yaongezeka kwenye awamu hii ya tano

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Kwa takribani wiki moja na ushei hivi, tulipiga kambi Zanzibar na kubahatika kupata udadisi wa kinachoendelea. Zanzibar kunaonekana kuko shwari kwa nje nje lakini kwa ndani utapata kujuwa hasa nini kinaendelea.

Maelezo yafuatayo yatasaidia kutoa picha halisi kwa tahmini ya Mwandishi na kile alichokiona.

Tathmini hii ibaki kuwa ni ya Mwandishi mwenyewe na haihusiani na taasisi au mamlaka yoyote.

HOFU YA ZANZIBAR KUMEZWA KWENYE MUUNGANO KWENYE AWAMU HII.
Hio hofu ipo juu sana. Mwandishi alipata ufafanuzi mbali mbali kutoka vyanzo tofauti na kubaini kuwa kuna hofu kuu. Hofu hii iko ndani ya SMZ yenyewe na hata kwa wananchi wa kawaida.

Kupitia vyanzo hivyo kuna malalamiko kwa baadhi ya Viongozi ndani ya SMZ na watendaji kulalamikia kuhusu Zanzibar kupoteza nguvu zake ndani ya Muungano na kukosa baadhi ya mashirikiano licha ya mapambio yaliyopo. Mifano ya wazi iliyotolewa kwa siku za karibuni ni SMT kushindwa kusaini mkopo ambao ungeisadia Zanzibar kujenga Bandari yake eneo maarufu la MPIGA DURI. Bandari hii imeahidiwa kwenye ilani ya CCM ya 2015 - 2020.

SMZ kukosa mashirikiano ya JMT kuhusu uimarishwaji wa ujenzi wa uwanja wa Ndege eneo la kukaa Abiria ambapo mradi huo hadi sasa haujakamilika.

Kuna malalamiko mengine mengi kuhusu ushirikishwaji wa Zanzibar kwenye mambo kadhaa ambayo maamuzi yake huathiri moja kwa moja mamlaka za Zanzibar. Kwa Mfano Mwandishi alibaini mvutano uliopo baina ya TFF na ZFF. Licha ya kuwa Michezo si suala la Muungano, TFF inalalamikiwa kwa kuhodhi Utambulisho wa Tanzania na kufaidi misaada ya maendeleo na kuiacha Zanzibar pweke.

Mwandishi alibaini kuwepo mgogoro unaofukuta kati ya TFF na ZFF. Aidha aliweza kubaini kufanyika hatua za makusudi kutoka pande mbili ili kutuliza hali.

Vile vile hofu ipo hata katika ulingo wa siasa za CCM yenyewe kama chama tawala. Mwandishi aliweza kubaini kuibuka kwa kambi za CCM Zanzibar. Kilichopo ni Urais baada ya Dr Shein. Ndani ya Serikali na kwenye Chama kuna kuwindana kwa kambi hizo.
Mwandishi amebaini kuwepo Kambi kuu mbili moja ikijinasibisha na Uungwaji mkono kutoka Bara na Moja ikijibainisha na Uzanzibari. Kwa maana kwamba CCM Zanzibar wana kilio cha muda mrefu cha kutaka mgombea atokane na maamuzi ya Zanzibar yenyewe na sio maamuzi kutoka upande wa Bara.

Kilichobainika CCM Zanzibar inaona hatari iliyopo ya kupatiwa mgombea kutoka Bara na hivyo kutokuwa na Uzalendo wa Maslahi ya Zanzibar kwenye Muungano. Pamoja na kwamba wote wana itikadi moja na ilani moja liunapokuja suali la utashi ndipo hofu ilipo.

Lengine ni hofu ya Utawala uliopo kwenye Muungano na maamuzi yasiyotabirika. Hili nalo lipo. Kuna hofu ndani ya watendaji SMZ na kwenye CCM kwamba Zanzibar kunahitajika Kiongozi Imara na shupavu ambaye atakuwa na uthubutu wa kuipigania Zanzibar. Taarifa zinabainisha kwamba kwa miaka ya hivi karibuni kumekosekana haiba hio na kila kitu kuhusu Zanzibar kukosa nguvu. Jambo hili linaleta lawama hata kwa Uongozi wa SMZ uliopo sasa. Hali hio inazidisha uvumi kwamba sasa Zanzibar inakwenda kuwa Mkoa moja kwa moja.

Utawala wa Rais Magufuli wa Kufanya Maamuzi ya Haraka nao unatia hofu wanasiasa wa Zanzibar kwa baadhi ndani ya CCM na nje ya CCM.

Kwa upande wa WANANCHI WA KAWAIDA, nako kuna hofu za aina hio. Wananchi wengi wengi wanakutajia moja kwa moja mtazamo wao. Ukigusa suali tu nafasi ya Zanzibar kwenye Muungano ni ipi ? unakutana na majibu yaliyofanana. HAIPO. na hicho kidogo kilichokuwepo kinakwenda kupotea . Hayo ndio majibu. Wananchi wengi mwandishi aliokutana nao wanatoa mifano ya Kutotambuliwa Kitambulisho cha Mzanzuibar Mkaazi kwenye mambo ya kitaifa kama Passpoprt na Usajili wa Laini za Simu na hivyo kuhitimisha kudhoofu kwa utambulisho wa Zanzibar kwenye Muungano na kupoteza hadhi yake. Mambo ni Mengi muda NI MCHACHE.

Lengine linalozungumzwa ni kukosekana Sauti ya UPINZANI Zanzibar kuwa nalo linazidisha HOFU ya Zanzibar kumezwa kwenye Muungano. Hapa kila mmoja anamlaumu Mwenzake. Mwandishi alibaini baadhi ya Wananchi kuwalaumu viongozi wa Upinzani kwa kususia na kuwaacha CCM peke yao jambo ambalo wanabainisha kuwa hawana nguvu za kuitetea Zanziubar. Wengine wanawalaumu CCM kwa kushindwa kuisimamia Zanzibar kwenye Muungano.

Kwa ufupi Zanzibar kuna Hofu kubwa ya Kumezwa na kupotea kwenye Muungano na Mwandishi amebaini tiketi muhimu kuelekea chaguzi za 2020 ni Kuhusu ; Uzalendo wa Zanzibar" hili liko ndani ya CCM na upinzani vile vile.

Hio ndio tathmini ndogo ya hali ya Zanzibar kuhusu Muungano kwa sasa na wanavyoichukulia awamu ya Tano.

Kishada.
 
Wazanzibar walitaka "nchi yao" wenye kujiamulia mambo yao wenyewe "wasibanwe"!...niki ndio kilikuwa kilio chao.

Awamu huu wamepewa uhuru huo. Zanzibar na habari zake inafifia Tanganganyika huku Wazanzibar Zanzibar wakiimarika kimya kimya!

Hakuna habari za Zanzibar katika media nyingi za bara achilia mbali za habari za riots wa ITV Faruku Karimu na Za Azam TV!

Hii inamaana kwamba wazanzibar hasa viongozi walafi wa madaraka na wanaharakati kina Jussa walibip wamepigiwa mazima!

Wasipokuwa makini Umaarufu wa Zanzibar ndio unakufa hivyo na kurudi kuwa Mkoa au moja ya Wilaya ya Tanzania.
 
Ukifuatilia utapata habari nyingi sana. Utajiuliza masuali mengi.
 
Zanzibar inastahili kuwa mkoa tu kupunguza matumizi makubwa ya muungano
Ukweli ni kwamba wazanzibari kwa ujumla wao wanataka wawe huru kuongoza Zanzibar. Mifumo iliyopo inakuwa vigumu kwa Wazalendo hata waliomo kwenye CCM kufurukuta. Upande wa Muungano unachezesha kete zake Vizuri Zanzibar. Unaambiwa ikionekana Maslahi ya Muungano kwa Upande wa Bara yanayumba wako tayari hata kufuta Uchaguzi na kupitisha Gari za Deraya mitaani ilimradi mambo yaende. Halafu Zanzibar wanaachiwa sokomoko lao.
 
Vile vile hofu ipo hata katika ulingo wa siasa za CCM yenyewe kama chama tawala. Mwandishi aliweza kubaini kuibuka kwa kambi za CCM Zanzibar. Kilichopo ni Urais baada ya Dr Shein. Ndani ya Serikali na kwenye Chama kuna kuwindana kwa kambi hizo.
Mwandishi amebaini kuwepo Kambi kuu mbili moja ikijinasibisha na Uungwaji mkono kutoka Bara na Moja ikijibainisha na Uzanzibari. Kwa maana kwamba CCM Zanzibar wana kilio cha muda mrefu cha kutaka mgombea atokane na maamuzi ya Zanzibar yenyewe na sio maamuzi kutoka upande wa Bara.
Nafikiri na ninaweza nikawa siko sawa-Zanzibar ina matatizo makubwa mawili. La kwanza ni hizi kambi ndani ya CCM ambazo muda wote hupelekea kiongozi wa zanzibar kuchaguliwa dodoma. Tunaweza kujikumbusha ya Jumbe na ya Bilali. Apitae CCM zanziar hana uhakika wa kupita Dodoma hasa kama anaonekana ana U-Zanzibari mkali. Muulize Bilali atakuambia, wenyewe walimpa umakamo wa JMT na kumnyamazisha. Wakati wa Karume walimuambia Bilali atoe jina.
Tatizo la pili ni kuingiliwa kwa chaguzi za Zanzibar na CHAMADOLA, Nyerere, Mkapa, Jakaya wamefanya hivyo na JPM kajifanya hayo kayakuta na kumuachia yule babu (JeCha) kufuta uchaguzi. Na kenye hili ukipinga ni kipigo tu.
Watatokaje hapa-mimi sijui na 2020 si mbali ngoja tuone.Nakumbuka Shein na ukimya wake alitoa moja kali walipomtishia kukata umeme. Alisema "Kateni tu, tutawasha vibatali" na serikali ya JMT(Soma Tanganyika ikaufyata). Wakisimama kwa umoja wanaweza wakapata wakitakacho lakini umoja na mshikamano n kitu kigumu sana. Nyerere aliwahi kusema "walidai, sitawapiga mabomu" sijui kama ni kweli alimaanisha hivyo au ilikuwa geresha. BWM yeye alitwanga. JPM nina hakika atampa kazi Murotoooo.
 
Zanzibar haitakuwa mkoa abadan ila itaendelea kutawaliwa na Tanganyika kwa mgongo wa Muungano mpka pale wazanzibar watakapokuwa wamoja. Hakuna chengine chochote kitakachoipa Zanzibar uhuru wake zaidi ya Umoja. Lakini kuna kazi kubwa sana ya kupatikana umoja wa Zanzibar maana Watanganyika wanatumia mbinu ya divide and rule. Wazanzibar wanagaiwa kwa siasa, ukabila na dini. Kwenye nyanja ya siasa CCM wa Zanzibar wanaaminishwa kuwa Zanzibar ni milki yao maana wao ndio waliopindua hivyo hakuna chama chengine chochote chenye hali yakushika dola, hata hivyo pamoja na kuaminishwa hivyo bado hali inakuwa ngumu sana siku za uchaguzi na wanashindwa kwa kura lakini Mtanganyika anatumia nguvu kukibakisha chama cha Mapinduzi (Rejea uchaguzi wa 2015). Pia Watanganyika wanatumia ukabila wa kuwagawa wazanzibar kwa kutumia upemba na Uunguja. Wanaleta propaganda ya kuwa wapemba ni hizbu na kukinasibishwa CUF ambayo sasa ni ACT wazalendo kuwa ni chama cha mahizbu hivyo hawana haki ya kutawala. Pia wanajaribu kujenga hoja ya kuwa CUF now ACT kuwa una wafuasi wake pemba tu ili waweze kuhalisha wizi wa kura katika majimbo ya Unguja kitu ambacho sikweli kwani 2015 CUF na CCM walipata majimbo sawa ya uchaguzi. Mwisho kabisa wanaendelea kuitawala Zanzibar kwa kigezo eti Zanzibar ikiwa huru inaweza kuwa kituo cha kigaidi kwa sababu tu 99% ya watu kule ni muslims fikra ambayo ni dhaifu sana. So siku wazanzibar wakiungana pamoja wanaweza kujikomboa katika dimbwi la ukoloni na kuwa huru.
 
wenzenu Catalunya wanasotea uhuru miaka zaidi ya 1000 nyie hata 100 bado haijafika mnaanza kulia lia!
Zanzibar kujiondoa kwenye makucha ya ukoloni wa Tanganyika bado sana
 
Kwa takribani wiki moja na ushei hivi, tulipiga kambi Zanzibar na kubahatika kupata udadisi wa kinachoendelea. Zanzibar kunaonekana kuko shwari kwa nje nje lakini kwa ndani utapata kujuwa hasa nini kinaendelea.

Maelezo yafuatayo yatasaidia kutoa picha halisi kwa tahmini ya Mwandishi na kile alichokiona.

Tathmini hii ibaki kuwa ni ya Mwandishi mwenyewe na haihusiani na taasisi au mamlaka yoyote.

HOFU YA ZANZIBAR KUMEZWA KWENYE MUUNGANO KWENYE AWAMU HII.
Hio hofu ipo juu sana. Mwandishi alipata ufafanuzi mbali mbali kutoka vyanzo tofauti na kubaini kuwa kuna hofu kuu. Hofu hii iko ndani ya SMZ yenyewe na hata kwa wananchi wa kawaida.

Kupitia vyanzo hivyo kuna malalamiko kwa baadhi ya Viongozi ndani ya SMZ na watendaji kulalamikia kuhusu Zanzibar kupoteza nguvu zake ndani ya Muungano na kukosa baadhi ya mashirikiano licha ya mapambio yaliyopo. Mifano ya wazi iliyotolewa kwa siku za karibuni ni SMT kushindwa kusaini mkopo ambao ungeisadia Zanzibar kujenga Bandari yake eneo maarufu la MPIGA DURI. Bandari hii imeahidiwa kwenye ilani ya CCM ya 2015 - 2020.

SMZ kukosa mashirikiano ya JMT kuhusu uimarishwaji wa ujenzi wa uwanja wa Ndege eneo la kukaa Abiria ambapo mradi huo hadi sasa haujakamilika.

Kuna malalamiko mengine mengi kuhusu ushirikishwaji wa Zanzibar kwenye mambo kadhaa ambayo maamuzi yake huathiri moja kwa moja mamlaka za Zanzibar. Kwa Mfano Mwandishi alibaini mvutano uliopo baina ya TFF na ZFF. Licha ya kuwa Michezo si suala la Muungano, TFF inalalamikiwa kwa kuhodhi Utambulisho wa Tanzania na kufaidi misaada ya maendeleo na kuiacha Zanzibar pweke.

Mwandishi alibaini kuwepo mgogoro unaofukuta kati ya TFF na ZFF. Aidha aliweza kubaini kufanyika hatua za makusudi kutoka pande mbili ili kutuliza hali.

Vile vile hofu ipo hata katika ulingo wa siasa za CCM yenyewe kama chama tawala. Mwandishi aliweza kubaini kuibuka kwa kambi za CCM Zanzibar. Kilichopo ni Urais baada ya Dr Shein. Ndani ya Serikali na kwenye Chama kuna kuwindana kwa kambi hizo.
Mwandishi amebaini kuwepo Kambi kuu mbili moja ikijinasibisha na Uungwaji mkono kutoka Bara na Moja ikijibainisha na Uzanzibari. Kwa maana kwamba CCM Zanzibar wana kilio cha muda mrefu cha kutaka mgombea atokane na maamuzi ya Zanzibar yenyewe na sio maamuzi kutoka upande wa Bara.

Kilichobainika CCM Zanzibar inaona hatari iliyopo ya kupatiwa mgombea kutoka Bara na hivyo kutokuwa na Uzalendo wa Maslahi ya Zanzibar kwenye Muungano. Pamoja na kwamba wote wana itikadi moja na ilani moja liunapokuja suali la utashi ndipo hofu ilipo.

Lengine ni hofu ya Utawala uliopo kwenye Muungano na maamuzi yasiyotabirika. Hili nalo lipo. Kuna hofu ndani ya watendaji SMZ na kwenye CCM kwamba Zanzibar kunahitajika Kiongozi Imara na shupavu ambaye atakuwa na uthubutu wa kuipigania Zanzibar. Taarifa zinabainisha kwamba kwa miaka ya hivi karibuni kumekosekana haiba hio na kila kitu kuhusu Zanzibar kukosa nguvu. Jambo hili linaleta lawama hata kwa Uongozi wa SMZ uliopo sasa. Hali hio inazidisha uvumi kwamba sasa Zanzibar inakwenda kuwa Mkoa moja kwa moja.

Utawala wa Rais Magufuli wa Kufanya Maamuzi ya Haraka nao unatia hofu wanasiasa wa Zanzibar kwa baadhi ndani ya CCM na nje ya CCM.

Kwa upande wa WANANCHI WA KAWAIDA, nako kuna hofu za aina hio. Wananchi wengi wengi wanakutajia moja kwa moja mtazamo wao. Ukigusa suali tu nafasi ya Zanzibar kwenye Muungano ni ipi ? unakutana na majibu yaliyofanana. HAIPO. na hicho kidogo kilichokuwepo kinakwenda kupotea . Hayo ndio majibu. Wananchi wengi mwandishi aliokutana nao wanatoa mifano ya Kutotambuliwa Kitambulisho cha Mzanzuibar Mkaazi kwenye mambo ya kitaifa kama Passpoprt na Usajili wa Laini za Simu na hivyo kuhitimisha kudhoofu kwa utambulisho wa Zanzibar kwenye Muungano na kupoteza hadhi yake. Mambo ni Mengi muda NI MCHACHE.

Lengine linalozungumzwa ni kukosekana Sauti ya UPINZANI Zanzibar kuwa nalo linazidisha HOFU ya Zanzibar kumezwa kwenye Muungano. Hapa kila mmoja anamlaumu Mwenzake. Mwandishi alibaini baadhi ya Wananchi kuwalaumu viongozi wa Upinzani kwa kususia na kuwaacha CCM peke yao jambo ambalo wanabainisha kuwa hawana nguvu za kuitetea Zanziubar. Wengine wanawalaumu CCM kwa kushindwa kuisimamia Zanzibar kwenye Muungano.

Kwa ufupi Zanzibar kuna Hofu kubwa ya Kumezwa na kupotea kwenye Muungano na Mwandishi amebaini tiketi muhimu kuelekea chaguzi za 2020 ni Kuhusu ; Uzalendo wa Zanzibar" hili liko ndani ya CCM na upinzani vile vile.

Hio ndio tathmini ndogo ya hali ya Zanzibar kuhusu Muungano kwa sasa na wanavyoichukulia awamu ya Tano.

Kishada.

Hizo kambi za CCM wote ni wanafiki tu, (Wasaka Tonge) Zanzibar haitaweza kamwe kupata maendeleo ya aina yoyote kwa kupitia CCM.
 
Nafikiri na ninaweza nikawa siko sawa-Zanzibar ina matatizo makubwa mawili. La kwanza ni hizi kambi ndani ya CCM ambazo muda wote hupelekea kiongozi wa zanzibar kuchaguliwa dodoma. Tunaweza kujikumbusha ya Jumbe na ya Bilali. Apitae CCM zanziar hana uhakika wa kupita Dodoma hasa kama anaonekana ana U-Zanzibari mkali. Muulize Bilali atakuambia, wenyewe walimpa umakamo wa JMT na kumnyamazisha. Wakati wa Karume walimuambia Bilali atoe jina.
Tatizo la pili ni kuingiliwa kwa chaguzi za Zanzibar na CHAMADOLA, Nyerere, Mkapa, Jakaya wamefanya hivyo na JPM kajifanya hayo kayakuta na kumuachia yule babu (JeCha) kufuta uchaguzi. Na kenye hili ukipinga ni kipigo tu.
Watatokaje hapa-mimi sijui na 2020 si mbali ngoja tuone.Nakumbuka Shein na ukimya wake alitoa moja kali walipomtishia kukata umeme. Alisema "Kateni tu, tutawasha vibatali" na serikali ya JMT(Soma Tanganyika ikaufyata). Wakisimama kwa umoja wanaweza wakapata wakitakacho lakini umoja na mshikamano n kitu kigumu sana. Nyerere aliwahi kusema "walidai, sitawapiga mabomu" sijui kama ni kweli alimaanisha hivyo au ilikuwa geresha. BWM yeye alitwanga. JPM nina hakika atampa kazi Murotoooo.
Ngoja kwanza tukae sawa. Sisi Wazanzibari tutakapojua maana ya umoja mambo yatakwend sawa, la sivyo, wacha tujifunze kuishi kwanza.
 
Back
Top Bottom