Tathimini yangu juu tuzo za kimataifa za filamu za sinema zetu l-SZIFF2018

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
Na Sangu Joseph
.
Kwanza nianze kuwapongeza kampuni ya Azam Media kupitia mkurugenzi wake TIDO MUHANDO kwa kuamua kuirejesha tena kwenye Ramani Tasnia ya filamu nchini kiukweli kwa upande wangu sikuona changamoto au jambo lolote lililopelekea tuzo kutokwenda vizuri kimsingi zilikua poa sana kuanzia tuzo ya kwanza mpaka ya mwisho HONGERENI SANA mmejaribu mumeweza we are proudly of them aisee ndio maana mpaka SASA hivi hakuna malalamiko.
.
Lakini Kama ilivyokawaida inapotokea KITU kikubwa kama vile wadau lazima tuangalie kwa jicho la tatu namna nzima ya tuzo na utoaji kwa jicho langu kuna baadhi ya vitu nimefanikiwa kuviona sio kwa waandaji Bali wasanii wetu wa Bongo filamu nchini.

MASTAA WENGI HAWAKUWEPO KWENYE TUZO. Licha ya kuamini kuwa jana NDO ilikua kama kuzaliwa upya kwa Tasnia ya filamu bongo lakini nilishangazwa kuona idadi kubwa ya Wasanii ambao tunaamini wanatamba kama kina JB, RICHIE, RAY, WOLPER, UWOYA, na NK Kutokuwepo kwenye vipengele vyovyote nilijiuliza kwanini hawapo badhani kwa Kuwa mchakato (Majaji) uliendeshwa na wasomi itakua wasanii hawa kuna baadhi ya vigezo hawakufikia so nahisi kwa mwaka ujao watajipanga zaidi.
.
TUZO KUBEBWA NJE TZ BARA. Ukitoa vipengele vya Msanii mmoja mmoja, lakini kuna baadhi ya Tuzo ambazo ziliashiria BONGOFILM inahitaji kujiboresha sababu ya umuhimu wa vipengele hivyo mfano kipengele cha Mhariri bora wa Picha filamu ndefu, Mpiga picha bora Filamu ndefu, Tuzo zilienda KENYA kwa filamu ya Watatu, tuzo nyingine Mwandishi bora Filamu fupi, tuzo ya Muziki wa asili, Chaguo la Majaji Tuzo ilienda Visiwani Zanzibar kwa filamu ya BINTI ZANZIBAR. changamoto Pia kwa wasanii wetu kwenye tuzo zijazo lazima waweze kuzingatia maudhui na uhalisia ili waweze kufanya vizuri kwenye tuzo hizi.
.
TUZO ZA WEMA SEPETU. Licha kuibuka na tuzo mbili kama Msanii bora wa kike Na Chaguo la Watazamaji ni kweli imedhirisha Wema sepetu ndio msanii wa kike mwenye zaidi kuliko wote TZ ukizingatia ndie Msanii pekee Maarufu wa kike aliyeingia kwenye vipengele vingi kwenye Tuzo japo alishinda tuzo mbili tu but anapaswa kuongeza juhudi maana vipengele alivyoshinda ni ambacho kinahitaji ushawishi wa watu kupiga kura na lakini sio maudhui so itamuwia vigumu ikitokea msanii mwenzio mwenye ushawishi kama yeye akiingia kwenye kipengele hicho mfano WOLPER, JOKATE.
.
BONGO MUVI BADO INAVIPAJI. Aisee ni kweli ili ilihitaji mashindano kama haya ili kujua vipaji vipya vya bongo muvi Licha ya filamu za chipukizi kushirik kwenye vipengele mbalimbali lakini nimefurahishwa na baadhi ya Tuzo kuchukuliwa na filamu ambayo nilikua sihifahamu hii imeonesha umuhimu wa waandaji maana bila wao tusimgewajua wasanii wapya badala yake tungeendelea kuwapuuza wasanii wachanga wa Filamu mfano wa Tuzo mbili zilibebwa na watu wapya ambao simjui hata mmoja ni tuzo ya mhariri bora wa Filamu fupi na tuzo ya mpiga picha bora filamu fupi iliendwa kwa Filamu ya USINITENGE.
.
FInnaly imedhihirika Kuwa Gambo Zigamba ndie msanii bora wa kiume kwa sasa Bongo kunyakua tuzo NNE si mchezo kupitia filamu tu aliyocheza yeye wakati kulikuA na wasanii wakubwa kama Kina Ray, Jb ambao nao hata mmoja hawakuwepo kwenye vipengele chochote.

HONGERENI azamtv NYI MFANO WA KUIGWA.
.
[HASHTAG]#kijanamzalendo[/HASHTAG] [HASHTAG]#ilovetz[/HASHTAG] [HASHTAG]#maoniyangu[/HASHTAG]
 
kazi nzuri ila kwa upande wangu nahisi wake wanaoigiza siri za familia ndio watakaokuja kuirudisha bongo muvi niliwaangalia siku mbili tu sio siri wanajua
 
Nitachangia kidogo tu. Bongo wasanii wa filamu wenye vipaji wapo, tatizo wanakosa utaalamu. Hakuna watu wenye weledi wa kuweza kuiongoza tasnia ya filamu na kuirudisha kwenye hadhi. Utaalamu namaanisha, script writers wazuri, directors wa kweli sio hawa wababaishaji waliokosa ubunifu. Tatizo lingine kubwa ni suala la maadili, nidhamu ya kazi na kujitambua kwa wasanii.

Hayo yatosha.
 
Jamaaa wako VZr ukiamgalia zile tuzo hazina ubabaishaji kuna majaji wasomi kutoka nje..! Kwa hiyoo hakuna muvi ambayo haina vigezo pale ingepata tuzo tuzo zikosafi sana
 
Bongo muvi wanazingua tu. Tena baada ya kujihusisha na bashite ndio sina hata hamu ya kuangalia madudu yao.
 
Bongo muvi wanazingua tu. Tena baada ya kujihusisha na bashite ndio sina hata hamu ya kuangalia madudu yao.

Masikini usamehewe sijui tuna Vijana wa aina gani wewe yaaani watu wamejitokeza kuunga we unaleta masuala yako ya vyama..! MUNGU awasaidie..!
 
Makonda na sasamambo walipata tuzo ya nini?
Kichwa chako kina matatizo ndugu, tunajadili namna ya kuboresha na kukuza filam zetu wewe unaibuka na mambo ya Makonda, sasa hapa yanahusiana vipi na tuzo za jana, kweli sisi watanzania tuna safari ndefu sana
 
Kwani makonda na sasamambo sio waigizaji?

Wewe jamaa huna nia njema na vipaji vya ndugu zetu.
 
Kwani makonda na sasamambo sio waigizaji?

Wewe jamaa huna nia njema na vipaji vya ndugu zetu.
Sasa makonda na Mambosasa tangu lini wakawa waigizaji? Watu tuwe serious na mambo mhimu mda mwingine kutwa tunalalamika wanatupiga na kutuumiza mtu anaibuka kusema walipewa jana tuzo gani! Hii shida nayo
 
Kama hujawah kuona movie zao sema uelekezwe zilipo sio kuleta leta ubishi hapa jf.
 
Nani katamka chama? Bongo movie sucks. It always has.

SASA MTU anakuuliza kuhusu Sirro sijui makonda wanahusikaje na Bongo muvi yaani kiukweli mnatuaibishA sisi vijana..! Mnatufanya tuonekane MAZUZU..! sababu ya Ujinga km huo
 
Back
Top Bottom