Tathimini yako utendaji wa mawaziri wa JK:nani anafaa na nani apumzishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tathimini yako utendaji wa mawaziri wa JK:nani anafaa na nani apumzishwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Aug 23, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,015
  Likes Received: 37,746
  Trophy Points: 280
  Utendaji wa mawaziri ni kichoche kikubwa cha uwajibikaji kwa watumishi wa umma.Wizara inapopata waziri muwajibikaji ufanisi ktk wizara hiyo si jambo la kuuliza.Nani asie kumbuka uwajibikaji ktk wizara ya mambo ya ndani wakati wa enzi za mh.Augustino Lyatonga Mrema?Nimetumia mfano wa mh.Mrema kwasababu naamini rekodi yake mpaka leo hakuna alieifikia.

  Kwa mtazamo wangu,nchi hii bila mawaziri kuwajibika maendeleo ya kweli na ya haraka ni ndoto ya mchana.Watendaji wengi ktk wizara,taasisi na mashirika mengi ya umma utendaji wao umejikita ktk wizi,ufisadi,uzembe na kutokuwajibika.Uzoefu unaonyesha akipatikana waziri mchapakazi atawasimamia vizuri na wao kuwasimamia walio chini yao.

  Sasa watanzania wenzangu hebu tujiulize hivi huu uzembe,wizi,ufisadi n.k kwa watumishi wa umma hasa walioko ktk nafasi za utawala kama vile wakurugenzi,makamishina n.k uko ktk wizara mbili tu za mh.Mwakyembe na mh.Kagasheki?Hawa mawaziri wengine mbona hatuoni hatua za kuridhisha za kusimamia uwajibikaji katika wizara zao?Au wizara zao ziko safi?

  Mmi naona mh.Raisi anatakiwa achukue mfano wa mh.Mwakyembe na mh.Kagasheki wa kuwatimua wale mawaziri ambao utendaji wao si wa kuridhisha.Kuna baadhi ya mawaziri kuwasikia ktk vyombo vya habari ni labda kafungua semina mahali fulani,kaalikwa mahali kama mgeni rasmi na mambo kama hayo.

  Tatizo lingine mimi naona ni wao kukaa ofisini tu.Hivi mh.Mwakyembe na hata mh.Mulogo wangekuwa hawatembelei maeneo yao wangegundua madudu waliyoyabaini ktk ziara zao?Mawazi wengine wanajifunza nini kutoka kwa hawa wenzao?Kuna ubaya gani kuiga jambo zuri?

  Mimi nafikiri vyombo vya habari viwamulike na sisi watanzania tutoe maoni yetu kwa njia mbalimbali.

  Mwisho nasema mh.Mwakyembe kaza buti na usafishe wizara hiyo uliokabidhiwa.
   
Loading...