Tathimini ya soko la Muziki na Filamu Tanzania kama ambavyo Don Nalimison anachambua

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
TATHIMINI YA SOKO LA MUZIKI TANZANIA NA WASANII WA FILAMU

Naitwa Don Nalimison ni moja ya Wanamuziki nchini Tanzania ninayefanya mziki katika Lugha ya Kiingereza cha Kiafrika. Leo nataka tuangalie soko lilivyo.

ONLINE DISTRIBUTION MARKET
Tanzania bado hatujafikia soko la Online kwa kuwa 10% ya Watanzania ndio wanao tumia mitandao ya kijamii na hivyo kundi kubwa sio washabiki wa mitandao hiyo na pia wengi hawana uelewa wa mitandao hiyo hata Kama wamejiunga na mitandao hiyo. Na pia wengi hawana uwezo wa kifedha kuangalia na ku download mitandaoni kazi za Wasanii. Hivyo bado Wasanii na Wasambazaji wa kazi za Wasanii wana nafasi nzuri ya kuwafikishia Mashabiki wao kazi zao Kama hardcopy CD na DVD majumbani mwao kupitia mauzo ya madukani na machinga. Nchi za Magharibi wenzetu takribani 90% wanatumia mitandao ya kijamii na hii ni kuwa hali ya Kiuchumi kwa wenzetu iko vizuri Sana kununua vifurushi vya kutazama kazi za Wanamuziki na Wasanii kwa ujumla. Na hivyo kuwafanya Wanamuziki na Wasanii kupata kipato kikubwa Sana.Nampango wa kuwa na kampuni ya usambazaji kipindi kijacho ili kuokoa sanaa yetu.

MUUNDO WA MUZIKI NA FILAMU ZA KUKUBALIKA SOKONI
Mara nyingi tunafanya Muziki au kutengeneza FILAMU bila Kujua watu wengi wanapenda kazi gani? Na pia hatuangalii soko la Kimataifa zaidi tunaangalia kuuza kazi zetu Nchini mwetu tu. Mafanikio ya sanaa ni lazima tufanye Mambo kwa kulenga Mataifa mengine yanataka kazi za namna gani.

UBORA WA STUDIO ZETU
Tumekuwa tukiangushwa na studio za Kitanzania hasa unakuta mwimbaji ana nyimbo nzuri Ila mixing ya vocal inakuwa mbovu na kusababisha Mwanamziki kuonekana Hana uwezo ili Hali Yuko vizuri Sana. Kuna haja ya maprodyuza kushirikiana katika Kuboresha Muziki wa Tanzania kwanini tusijifunze kutoka Kongo, Nigeria na Afrika Kusini ambako maprodyuza wao hushirikiana pale wanapoona Mwanamziki au Msanii wa FILAMU ana kipaji kizuri ili kumuokoa.

VITUO VYA REDIO NA TELEVISHENI
Bado Kuna changamoto kwani bila kutoa pesa Nyimbo hazichezwi katika VITUO vya radio na TV, mfano Don Nalimison vituo vya radio na TV Zina shindwa kucheza nyimbo zangu kwa kuwa sijatoa chochote Cha kufanyiwa promotion ili Hali Nchi jirani napata sapoti kubwa bila kutoa fedha yoyote. Hii Hujuma lazima Wanamuziki wote kuungana ili kukomesha ukritimba huu.

MAGAZETI NA BLOGU
Magazeti nayo siku hizi yamekuwa na watu wao wa kuwaandika magazetini kwa maslahi Yao tu. Ukikosa fedha au umaarufu imekuwa ngumu kupata promotion magazetini, ikumbukwe kuwa promotion magazetini ni ya muhimu sana maana si wote wanatumia mitandao ya kijamii. Ndio maana Wanamuziki na Wasanii wengi wamejikita mitandaoni kwa kuwa uchumi wao ni mdogo kulipia magazetini. Wanasiasa wao hununua kabisa FRONT Page za magazetini na ndio maana wengi wanaandikwa Sana kwa kuwa wameyanunua magazeti. Ni wakati ambao imefika Wasanii nao kuanzisha magazeti yao yatakayo wabeba na kuwainua kisanii wao na wenzao, Mimi binafsi natafuta mtaji kusajili gazet maalum kwa ajili ya Wanamuziki na Wasanii japo litaanza Kama Magazine.

Niishie hapa kwa leo.

DON NALISON
DON NALIMISON ADVISORY BOARD
+255 682 94 29 01.
24 SEPTEMBER 2020.

FB_IMG_1600491637077_1.jpg
 
Don kama Don.

Mkuu lini utatoa tathimini yako kuhusiana na maswala ya soka la bongo hususani mustakabali wa vilabu vya SIMBA na YANGA ili nichote madini yako nakapate ujiko kitaa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom