Tathimini: Ujio wa treni ya kisasa na athari zake kwa biashara ya usafiri wa anga na barabara

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Ukweli ni kwamba wakati dunua inaachana na treni za kizamani,hata sisi kama Taifa katika huu ulimwengu hatuwezi kubaki nyuma ni lazima na sisi tuende sambamba na wenzetu ingawa sisi tunaweza kuwa na mapungufu katika kutekeleza miradi mikubwa kama hii.

Mfano,katika nchi nyingine mikataba kama hii sijui huwa haipitia Bungeni na kujadiliwa kabla kusainiwa kama ilivyo hapa kwetu mimi sielewi.

Nchi zingine nazo sijui huwa hazifanyi projection kujua faida na hasara za miradi mikubwa kama hii na kuchukua tahadhari mapema katika mipango yake ya baadae mimi sijui?

Anyaway,tuachane na hayo sasa turudi kwenye mada juu ya kile kinachoweza kutokea hapo baadae baada ya mradi huu mkubwa kukamilika kulingana na mtazamo wangu.

Kabla sijatao tathimi ya athari za mradi huu kwa sekta nilizozitaja,ni lazima nisema wazi tu kuwa faida zipo kama vile watu na mizigo kusafiri kwa haraka na kwa muda mfupi na hivyo kuokoa muda unapotea kwa watu kukaa njiani/safarini kwa muda mrefu na hii pia itasaidi katika kusafirisha wagonjwa kwa haraka na kuokoa maisha ya watu.


Pia reli hii ya kisasa itayoanzia Dar-es-Salaam mpaka Mwanza na kupita mikoa ya Morogoro, Dodoma na Tabora then kuingia Isaka kutuunganisha na nchi za jirani kabla ya kufika Mwanza, itakuza na kuimarisha biashara baina ya nchi yetu na nchi za jirani zinazitumia bandari yetu.

Tutaokoa bara bara zetu maana tutapunguza idadi ya malori yanayotumia barabara zetu kusafirisha shehena kubwa ya mizigo kwenda mikoani na nchi za jirani,n.k.

Hizo ni baaadhi tu ya faida za mradi huu.Hata hivyo,pamoja na faidi hizi; hasara za mradi huu lazima zitakuwepo ambazo baadhi zinaweza kuwa kama ifuatavyo:

Kabla sijaendelea zaidi ni vizuri tukajua main line hii kilomia zake zitakuwaje baada ya ujenzi kukamilika.

Dar mpaka Moro ni reli hii itakuwa na urefu wa kilomita 205.Moro mpaka Dom itakuwa ni urefu wa kilomita 336.Dom mpaka Tabora itakuwa na urefu wa kilomita 294.Tabora mpaka Isaka kilomita 133 na Isaka mpaka mwanza ni wastani wa kilomita 253 ambapo ni jumla ya wastani wa kilomita 1222 kutoka Dar mpaka mwanza kwa kutumia treni hii.


Usafiri wa Anga


Treni hii itakayokuwa na speed ya 160km/hr,ni wazi itachukua masaa kama 3 tu kutoka Dar mpaka Dodoma ambapo ni wastani wa km 541 kwa njia hii ya reli.

Sasa kama mtu atatumia masaa takribani 3 kwa njia ya reli na akaweza kubeba mizigo mingi na kwa bei nafuu ni kwanini mtu huyu apande ndege kutoka Dar mpaka Dodoma?

Je,si kweli hata wabunge wengi na wenza wao na vigogo wengi watapanda treni badala ya ndege kuja Dodoma ambayo kwa sasa nauli ya one way ni shilingi 220,00 kwa mtu mmoja kwa route ya Dom to Dar?

Wafanyabiashara wengi nao hawatatumia treni hii kwa safari za Dodoma to Dar na Dar to Dodoma?

Route ya ndege ya Dar to Dom/Dom to Dar kweli itaweza kuendelea kuwepo na ikawa na faifa kibiashara?

Kama kwenda Tabora kutoka Dar itakuwa ni mwendo wa takribani masaa 5 kwa treni hii, wafanyabiashara na watu wengine wenye safari za kifamilia wataacha kutumia reli hii ili kepuka gharama kubwa za kupanda ndege?

Je,hali ikitokea,shirika letu la ndege halitaweza kuyumba kutokana na safari zake za ndani kuathirika?

Muda utaongea.

Usafiri wa barabara


Kwa speed ya hii treni ni wazi Dar mpaka Moro ni wastani wa lisaa limoja na dakika chache tu.

Je,si kweli abiria wengi watakuwa watakuwa wanatumua treni hii badala ya mabasi ya Dar to Moro kulingana na ratiba ya treni hii?

Kwakuwa treni hubeba abiria wengi,hakuna uwezekano wa mabasi ya Dar to Moro kukosa abiria hasa katika ile mida treni hii itakapokuwa inafanya route zake?

Kama treni hii itatumia masaa takribani matano au chini ya hapo kutoka Dar mpaka Tabora,nani atakuwa tayari kupanda basi linalotumia masaa takribani 12 au 13 kutoka Tabora kwenda Dar huku akikabiliwa na risk nyingi za barabarani?

Hata kama treni hii haitokuwa inasafiri kila siku kama mabasi,je hakuna uwezekano wa watu wengi kupanga safari zao kulingana na ratiba hii ili kuwkwepa adha ya kusafiri na mabasi yenye risk nyingi za barabarani?

Treni hii ikiwa na nauli za chini huku ikutmia muda mfupi na ikawa na route za karibu kila siku,mabasi ya Dar to Tabora/Tabora to Dar,yata-survive kibiashara?

Mabasi yote yanayofanya safari za Dar to Dodoma /Dodoma to Dar yatamudu yote kuwepo barabarani hasa endapo treni hii itakuwa ina-operate almost daily?

Baadhi ya mabasi hayatalazimika kujiondoa au kubadili route?

Yakibadili route maana yake si yanakwenda kuongeza ushindani katika hizo route mpya na hivyo kufanya biashara iwe ngumu zaidi katika hizo route?

Ukiacha mabasi,malori yaliyokuwa yanasafirisha mizigo kutoka Dar kwenda nchi za jirani yatakuwa na kazi gani?

Si kweli kuwa malori haya baadhi itabidi yapaki tu kwa kukosa kazi?

Je,hakuna wamiliki wa mabasi na malori haya ambao baadhi waliochukua mikopo bank ili kununulia mabasi/malori haya ya kufanyia biashara?

Biashara zao zikiyumba kutokana na ujio wa hii treni ya kisasa,wataweza kurudisha mikopo ya kwa wakati?

Hata ukitaka kuuza au kupiga mnada basi hili au lori hili,nani atakuwa tayari kulinunua kama biashara imekuwa sio nzuri?

Tusisahau pia malori haya na mabasi haya ya masafa marefu mbali na kusafiri kila siku,lakini pia yanatumia lita nyingi sana za mafuta kwa safari moja tu hivyo yakipaki au kupunguza safari ni wazi kutakuwa na impact katika ile kodi ya road license iliyohamishiwa kwenye mafuta


Ni kweli kabisa ujio wa treni hii ni jambo jema lakini je, tumejiandaa na ahari zake?

Sifa yetu kuu wabongo ni kuwa "reactive" na si "proactive" na ndio maana mara nyingi huwa tunakumbuka shuka wakati kumekucha.

Time will tell.

Nyongeza:

Watu wanalinganisha nchi yetu na mataifa mengine ambayo yameendelea kiviwanda, yanashughuli nyingi za kiuchumi,biashara, yenye majiji na miji mikubwa mingi ya kutosha kuwezesha aviation industry kufanya vizuri.

Kwa mfano, Mpanda tuna kiwanja cha ndege kilijengwa enzi za Kikwete wakati Pinda akiwa waziri mkuu.Leo hii niambieni ni shrika gani lina route ya kibiashara ya kwenda Mpanda hata kwa ndege ndogo tu?

ATCL iliyofufuliwa juzi tu ilikuwa na route ya Dar to Kigoma via Dodoma kwa baadhi ya siku na Dar to Kigoma via Tabora kwa baadhi ya siku zingine.

Leo hii ulizeni kama unaweza panda ndege ya ATCL kutoka Dodoma kwenda Kigoma alafu uliza au jiulize ni nini kimetokea.

Tena kumbukeni uwepo wa wakimbizi kunapelekea uwepo wa mashirika na taassi mbalimbali zinazohusika na maswala ya wakimbizi hivyo kunachangia uwepo wa abiria wanaofanya kazi katika haya mashirika.

Pia jiulizeni leo hii Precission nao waamue wawe na route ya Dar to Dodoma nini kitatokea au jiulizeni ni kwanini hawana route hiyo mpaka leo hii.Hata route ya Dar to Tabora hawana ingawa ilikuwapo zamani wakaifuta labda kama weirudisha siku hizi ingawa sidhani.

Pia msisahau kuna ndege nyingine tumeongeza na wakati huo huo hii treni ya kisasa nayo inabisha hodi.

Mtabisha sana ila ni swala la muda tu kabla ukweli haujdhihirika.
 
hoja nzuri je kenya Nairobi -mombasa usafiri wa magari umeyumba?
Unajua wenzetu walijipangaje?

Na je,tumeenda walau kujifunza kujua nini zilikuwa athari za treni hiyo na walikabililiana zao vipi in case zilitokeza?
 
Vyovyote iwavyo, suala la reli ya kisasa sio la kusubiri tena.

Concern yangu kubwa ni wapi matawi ya reli husika yanatakiwa kuanzia! Hapa cha kuangalia ni potential ya kiuchumi na biashara ya kule reli inakoenda! Kwa mfano, Mbeya ni moja ya sehemu ambayo ilipaswa kuwa kwenye awamu ya kwanza!!!

Kutokana na umbali mrefu, usafiri wa mabasi to Mbeya ni boring unless kama mtu umeamua kufanya tour. Usafiri wa anga nao ni wachache wanaoweza kumudu!

kutokana na hilo, Mbeya ni very potential kibiashara na kiuchumi kwavile pia ni mkoa unaozalisha sana mazao ya kilimo.

Kwahiyo watakuwa wamefanya jambo la maana sana ikiwa ujenzi wa reli ya kisasa utaenda sambamba na kui-update TAZARA.
 
Labda mtoa maada ulikuwa unataka serikali itangaze kuwa wamejipanga????... pia itangaze athari za treni ni.......

Serikali ipo sahihi, lazma tuhame na technolojia chief

Haya mabasi inabidi yapige route za kwenda sehemu ambazo treni haiendi, pia ktk Jiji la Dar es salaam & Mwanza & Arusha tunaitaji mabasi makubwa ndo yapige route town, daladal na hiace ziende porini zaidi


Kuhusu malori inabidi yawe yanapokea mizigo kutika stesheni kupeleka wilayani, hiyi ndo itakuwa kazi ya malori

Acha treni ije tu
 
Vyovyote iwavyo, suala la reli ya kisasa sio la kusubiri tena.

Concern yangu kubwa ni wapi matawi ya reli husika yanatakiwa kuanzia! Hapa cha kuangalia ni potential ya kiuchumi na biashara ya kule reli inakoenda! Kwa mfano, Mbeya ni moja ya sehemu ambayo ilipaswa kuwa kwenye awamu ya kwanza!!!

Kutokana na umbali mrefu, usafiri wa mabasi to Mbeya ni boring unless kama mtu umeamua kufanya tour. Usafiri wa anga nao ni wachache wanaoweza kumudu!

kutokana na hilo, Mbeya ni very potential kibiashara na kiuchumi kwavile pia ni mkoa unaozalisha sana mazao ya kilimo.

Kwahiyo watakuwa wamefanya jambo la maana sana ikiwa ujenzi wa reli ya kisasa utaenda sambamba na kui-update TAZARA.
Mkuu, kuna awmu tano na Mbeya haipo kabisa.

Navyofahamu mimi awamu ni hizi:

Awamu ya kwanza ni Dar mpaka Moro.

Awamu ya pili ni Moro mpaka Dom.

Awamu ya tatu ni Dom mpaka Tabora.

Awamu ya nne ni Tabora mpaka Isaka

Awamu ya tano na ya mwisho ni Isaka to Mwanza hivyo Mbeya wala Kigoma haipo.
 
Hudumieni wananchi , maisha magumutaani nyie mnaonhelea tren?
 
Navyojua Mimi treni haiwezi kubeba mizigo yote au abiria wote,bado ma Lori yatafanya KAZI tuu .
Sema Kwa abiria route ndefu kama mwanza ,kigoma,tabora wenye mabac itakuwa ishu kwao.
 
Mbona haukuongelea swala la uharibifu wa barabara zetu,

Mbona haujawazia kuwa je huoni huo ndio tunaita ushindani wa soko huria......

Je haujui kuwa hata hawa wamiliki wa mabasi wanaweza kuingia mkataba na serikali wakanunua mabehewa na kuyafanya kiwa ya luxury.

Je haujui kuwa Tanzania inamikoa mingi na hivyo haya mabasi yanaweza kuhama route.

Je haujui kuwa hiyo tija uliyoisema kama swala la muda mfupi wa kusafiri, kubeba mizigo mingi kwa gharama nafuu, na vinginevyo ndio vitu tunataka ili kuweza kupata maendeleo ya haraka....maana hiyo mikoa tajwa itachangamka na fursa mpya zitafunguliwa.
 
Navyojua Mimi treni haiwezi kubeba mizigo yote au abiria wote,bado ma Lori yatafanya KAZI tuu .
Sema Kwa abiria route ndefu kama mwanza ,kigoma,tabora wenye mabac itakuwa ishu kwao.
Na ndio hao nawaongelea hapa
 
Mwendo kasi ilipoanza watu waliadhani biashara ya daladala itakufa lakini wala ndo kwanza inaendelea Kwa kasi. Hata hiyo reli haiwezi kuwa biashara zingine.
 
Iwepo mizigo na abiria wa kutosha kubeba kila chombo kuanzia biskeli,boda boda,taxi,dala dala mabasi,maroli , train na ndege watafanya biashara.
Lakini itategemea na ukuaji wa uchumi na kipato cha wananchi walio wengi.
 
Treni ikianza kazi ndio muda tujenge barabara zetu kwa kiwango cha juu ili kutoa fulsa kwa watumiaji wa barabara.Hii itapunguza msongamano kwenye Treni na anga. Hata nchi zenye treni bado sio kila mtu anatumia Treni.
 
Mtoa mada unaonekana akili zako ni dormant kabisaa huku ukijifanya unajua unachokisema
Labda nikuulize swali je? Wazungu waliogundua aina hizi zote za usafiri waliachana na moja na kudeal tu na hyo mpya
Mbona aina hizi sote za usafiri zinatumika bado katika nchi zao bila athari yoyote ya kiuchumi
 
Back
Top Bottom