Tathimini: Baada ya bomoabomoa,nini kimefanyika katika maeneo husika?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,668
149,840
Hili zoezi lilifanywa kwa kasi na kwa dharura kanakwamba ni dharura ya kukabiliana na uvamizi wa kijeshi.

Sasa baada ya maamuzi haya kutekelezwa,ni nini kimefanyika katika maeneo husika kuthibitisha udharura uliojitokeza?Kuna chochote cha maendeleo kinafanyika huko?

Kwa waliokuwa maeneo ya mabondeni tunaweza sema angalau ilikuwa ni hatua za kuwanusuru wakazi hao na majanga ya mafuriko.Kwa hawa wengine je?

Najua hakuna kilichofanyika cha maana mpaka sasa kwasababu hata mipango hiyo ya dharura bila shaka haikuwepo.Ili kuondo visingizio mtakavyoleta,nawapa miezi mingine sita mje mtuthibitishie udharura uliojitokeza ingawa kwa muda huo hata logic ya udharura huo itakuwa haipo tena.Tutaanza na uendelezaji wa maeneo ya wazi kama vile viwanja vya michezo, n.k

Tukutane,panapo majaliwa, hapa JF tarehe 24/09/2016 kupeana majibu.
 
Yale ni maeneo wazi ya kupumulia mito inayomwaga maji yake baharini. Waliojenga katika maeneo hayo walikuwa wameziba njia hizo na hivyo kusababisha mafuriko.Maendeleo yaliyofanyika ni kurejesha maeneo hayo katika hali yake ya asili!
 
Wewe ukitaka wakishabomoa wajenge nini?
Siyo lazima kujengwe kitu, uendelezaji wa eneo la ardhi unahusisha mambo mengi. Badala maeneo hayo kugeuka mapori yatakayofuga wezi na vibaka na kugeuzwa sehemu hatari dhidi ya wakazi wa Dar ni lazima yaendelezwe badala ya kuachwa.

Na mtoa mada kaweka wazi kabisa kuwa kwa jinsi zoezi lilivyoendeshwa ilikuwa kama vile kuna udharura na ndiyo maana anahoji kama kweli kulikuwa na huo udharura au zilikuwa ni pupa tu za Kisiasa!!
 
Hawa watu vichwa vyao ni kama "hardware" na siasa ndio "software" inayotumika ku-operate vichwa vyao!
 
CCM ina-fit sana kwenye ule msemo "chizi kapewa rungu mbele ya duka la vioo" Yaani viongozi wa CCM ni kawaida yao kutumia ovyo ovyo madaraka wanayopewa na wananchi bila ya kujali hasara watakayoisababisha kwa jamii yetu!!
 
kama pale wilayani wamepavunja halafu hakuna chochote kinachoendelea si bora wangeacha watu waishi nowadays ni kijiwe cha wahuni
 
Alifikiri ni rahisi, akasahau msemo hata roma haikkujengwa kwa siku moja. Kukosa busra na hekima kwenye uongozi ni sawa na saratani mwilini mwa binadamu.
 
jangwani wameanza kurudi kama kawaida yao nimeona mabanda na nguo zimeanikwa hivi kwanini wanapapenda sana japo hapafaai kabisa kwa matumizi ya binadamu? jangwani pabaya kuliko sehemu yoyote mfyuuuuuuuuuuuu
 
Hili zoezi lilifanywa kwa kasi na kwa dharura kanakwamba ni dharura ya kukabiliana na uvamizi wa kijeshi.

Sasa baada ya maamuzi haya kutekelezwa,ni nini kimefanyika katika maeneo husika kuthibitisha udharura uliojitokeza?Kuna chochote cha maendeleo kinafanyika huko?

Kwa waliokuwa maeneo ya mabondeni tunaweza sema angalau ilikuwa ni hatua za kuwanusuru wakazi hao na majanga ya mafuriko.Kwa hawa wengine je?

Najua hakuna kilichofanyika cha maana mpaka sasa kwasababu hata mipango hiyo ya dharura bila shaka haikuwepo.Ili kuondo visingizio mtakavyoleta,nawapa miezi mingine sita mje mtuthibitishie udharura uliojitokeza ingawa kwa muda huo hata logic ya udharura huo itakuwa haipo tena.Tutaanza na uendelezaji wa maeneo ya wazi kama vile viwanja vya michezo, n.k

Tukutane,panapo majaliwa, hapa JF tarehe 24/09/2016 kupeana majibu.

Wahanga wapi unaowazungumzia? Waliojenga katika open spaces au kunakotakiwa kupita bomba la maji, be specific!
 
Wapuuzi hao wametesa sana watu. Niliwaambia watu huu uharaka unatoka wapi!? Kwani wangepewa muda kulikuwa na tatizo miezi mitatu mpaka sita. Wamekiuka sana haki za binadamu. Wanatakiwa washtakiwe tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom