TASWIRA; Viongozi mbalimbali Washiriki Mazishi ya Baba Mzazi wa Tundu Lissu!

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765

Wakili wa kujitegemea mkoani Arusha, akisoma taarifa ya wasifu wa baba yake mzee Augustino Lissu Mughwai (86) wakati wa misa ya mazishi wa mzee huyo ambaye pia ni mzazi wa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu.Mzee Augustino alifariki dunia septemba 16 mwaka huu.

Waziri wa nchi, sera, uratibu na bunge Mh. William Lukuvi akitoa salamu kwenye msiba wa baba yake na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kijijini Mahambe.
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe (wa kwanza kulia) akifuatilia misa ya mazishi ya baba mzazi wa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu MzeeAugustino Lissu Mughwai aliyefariki dunia Septemba 16 mwaka huu.
Waziri wa nchi,sera,taratibu na bunge William Lukuvi (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye msiba wa mzee Augustino Lissu Mughwai baba mzazi wa mbunge wa jimbo la Singida mashariki Tundu Lissu.Wa kwanza kushoto ni naibu waziri wa maliasili na utalii,Lazaro Nyalandu na wa pili kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone.Wa kwanza kulia ni mbunge wa Karatu CHADEMA,Israel Natse.
Wakili wa kujitegema mkoani Arusha, Allute Mughwai (wa kwanza kulia) akifuatilia kwa makini misa ya mazishi ya baba yake mzee Augustino Lissu Mughwai. Wa nne kutoka kulia ni mbunge wa jimbo la Singida mashariki,Tundu Lissu.

Mbunge wa jimbo la Kigoma kaskazini Kabwe Zitto (kulia) akizungumza na mkuu wa wilaya ya Ikungi Manju Msambya wakiwa kwenye mazishi ya baba wa mbunge wa jimbo la Singida mashariki,Tundu Lissu.(Picha zote na Nathaniel Limu).
 
mmmh! Kumbe Alutte na Tundu ni Ndugu? hafu wote ni Mawakili? Hafu wote wanavaa miwani!!Hafu wote wako kwenye kesi moja, ya GODBLESS Lema? lakini pia wako pande tofauti kwenye hiyo kesi!!
 
may his soul rest in peace, asante kwa picha kamanda, tupo pamoja.
 
Inatia moyo kuona watu wameitikia kuungana na wanafamilia kwenda kummpumzisha baba wa Lissu. Upumzike kwa amani Baba
 
Siasa sio chuki wala visasi, kwenye matukio ya namna hii lazima tuoneshe kuwa sisi ni Watanzania, watoto wa baba mmoja, nimeona baadhai ya Wabunge wa Singida, bila kujali vyama vyao na walikuwepo, sina hakika kama walikuja kumwakilisha yule wakili wa Arusha (maanake yeye yupo magamba while his Brother yupo Opposition) anyway, hiyo sio issue, lakini je Mchemba nae alikuwepo jamani? ni swali tu, na kama hakuwepo, alikuwa na issue yoyote iliyo mzuia? Ni swali tu wakuu.
 
inatia moyo sana na faraja kwa ndugu wafiwa,kweli msiba siasa huwekwa pembeni,nashukuru serikali inaona umuhimu wa mh.Tundu Lissu,ndo maana viongozi wa pande zote za serikali na chadema walikuwepo naskitika ndugu zetu cuf sijaona mwakilishi wa ngazi za juu,
Tunashukuru kwa kutuwekea picha za tukio muhimu la kumpumzisha baba wa Mh.Tundu Lissu,Kamanda wa ukweli
 
angekuwa amefiwa mtu wa chama kingine mfano ccm ungeona matusi na kejeli
 
inatia moyo sana na faraja kwa ndugu wafiwa,kweli msiba siasa huwekwa pembeni,nashukuru serikali inaona umuhimu wa mh.Tundu Lissu,ndo maana viongozi wa pande zote za serikali na chadema walikuwepo naskitika ndugu zetu cuf sijaona mwakilishi wa ngazi za juu,
Tunashukuru kwa kutuwekea picha za tukio muhimu la kumpumzisha baba wa Mh.Tundu Lissu,Kamanda wa ukweli

ngoja usikie amefiwa au amefariki wa chama kingine uone comment za wana jf/cdm tulivyo
 
Back
Top Bottom