Taswira ninayoiona ndani ya CCM baada ya uchaguzi hadi kufika 2025

Hoja yako ina mantiki kidogo ingawa ni lazima utambue kuwa wapinzani hawajawahi kuwa na impact yoyote kwa miaka mitano iliyopita. wao ilikuwa ni kupinga kila kitu, kutoka nje ya bunge, kutukana, kujijali wao wenyewe na matumbo yao.

Kazi zote zilifanywa na CCM na ndicho sasa wanakwenda kukifanya. Kipindi hiki tutarajie uchapa kazi uliotukuka na maendeleo chanya zaidi maana wapumbavu hawapo tena.
Politely.....naona kama umekosea vile.
 
E
Kwa mtu yeyote makini hawezi sema uchaguzi umefanyika bali atasema uchaguzi umevurugwa.
Mimi sina chama lakini napenda kusimamia haki.
Tangu mchakato wa kuandikisha wapiga kura hadi kuja kupiga kura na kutangaza matokeo ni vituko, utoto, ukatili, kukosa uzalendo , kufagilia matumbo na mambo ya hovyo mengi sana.
Exactly.
 
Ninachokiona ni kuwa na bunge Kali sana lakini wabunge wengi wa aina ya Nape na Serukamba na Bashe watadhibitiwa na Katibu mkuu wa Chama.

Watadhibiwa sababu siasa zitakua za Kikanda.
Miaka mitano iliyopita kiukweli miradi mingi mikubwa ilikua inaelekezwa kanda Fulani zaidi . Kila ukiwasha TV utasikia uzinduzi kanda ile,mradi mkubwa kanda ile , SGR inatumia mabilion ya Dola lakini inaelekea kanda ile.

Watu wakaamini Tanzania imekua kama Dubai kwa uzinduzi wa kila siku kwenye TV .
Ilikua ni Nadra kusikia uzinduzi kule mafia au Pemba, Kilwa, Liwale,Nkasi n.k. ambapo pia kuna Binadamu na watanzania wanaolipa kodi.

CCM wakaungana kwa sababu walikua na adui ambaye ni wapinzani.

Sasa hakuna adui Watasema ukweli kuwa Hiyo SGR haiwezi kumsaidia Mwananchi wa Kilindi kule Tanga wakati wa mvua kwani barabara haipitiki bila kuwekwa Lami.

Watasema ukweli kuwa Biashara zinakufa mana zilizobaki ni za kwao na itabidi ziguswe ili nchi ipate kodi mana za wasiowapenda zilishakufa.

Lakini pia Roho wa Mungu ananiambia kuwa pataibuka wabunge watakaotaka kuweka MTU wao mwaka 2025 hao watataka kuonyesha udhaifu wa Utawala wa awamu hii bila kupepesa ili kuondoa mawazo ya wale wanaotaka kumfanya JPM kuwa Rais wa maisha.

Kundi LA wanaufaika litazidiwa kwa hoja mana watakua hawana hoja za kuwagusa wananchi zaidi ya kusifia huku wananchi wakiwa wanaumia.

Hapo ndio Chama cha mapinzuzi kitakapojipindua chenyewe ili kimpate Rais wa 2025 atakayegusa mioyo ya watanzania wengi waliokata tamaa kwenye sanduku la kura.

Nafikiri Busara itumike iundwe tume ya watu hata kutoka nje ichunguze majimbo na kata zote walizotangaza watu walioshindwa uchaguzi urudiwe ili washindi halali wapatikane.
Na waliovuruga uchaguzi wachukuliwe hatua. Hata kama ni makada na wakurugenzi . Kuna Giza Nene kama wakubwa watapuuza.
 
Mimi naamini alichokifanya bwana yule ameitengenezea CCM matatizo makubwa sana tofauti na uhai wake kabla, bila kujua ameipaisha chadema kitaifa mpaka kimataifa, haina tofauti mfano na waliompiga Tundu lissu risasi kugeuka kuwa mtu maarufu
 
Lakini pia Roho wa Mungu ananiambia kuwa pataibuka wabunge watakaotaka kuweka MTU wao mwaka 2025 hao watataka kuonyesha udhaifu wa Utawala wa awamu hii bila kupepesa ili kuondoa mawazo ya wale wanaotaka kumfanya JPM kuwa Rais wa maisha.
Mpasuko mkubwa sana wautarajie, mifano ya wakina Nape na baadhi ya makayibi wakuu wachama wastafuu ndiyo watakao ongoza huo mchakato
 
Hoja yako ina mantiki kidogo ingawa ni lazima utambue kuwa wapinzani hawajawahi kuwa na impact yoyote kwa miaka mitano iliyopita. wao ilikuwa ni kupinga kila kitu, kutoka nje ya bunge, kutukana, kujijali wao wenyewe na matumbo yao.

Kazi zote zilifanywa na CCM na ndicho sasa wanakwenda kukifanya. Kipindi hiki tutarajie uchapa kazi uliotukuka na maendeleo chanya zaidi maana wapumbavu hawapo tena.
Uko sawa kabisa "wapumbavu" hawapo, sasa tutaona maendeleo.
 
Ukimfanyia mtu jambo baya ni rahisi kulisahau.
Lakini ukifanyiwa wewe mwenyewe jambo baya huwezi kulisahau hata kama umesamehe.
Sahihi kabisa. Mtenda husahau mapema lakini mtendwa hawezi kusahau hasa kama katendwa vilivyo.

Huu uchaguzi umewashangaza hata waliotenda, wanashindwa tu kusema lakini mioyo yao haina amani.
 
Back
Top Bottom