Taswira:Mke wa Rais Mama Salma Kikwete Atembelea kituo cha kuwatunza wasichana na wanawake watukutu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


JUN .Written by haki



IMG_5786.jpg





Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa msichana anayetunzwa katika kituo cha watoto wa kike watukutu cha Pertapis kilichoko Singapore wakati alipokitembelea kituo hicho tarehe 6.6.2013. Mama Salma yupo nchini Singapore akiambatana na Rais Kikwete katika ziara ya kikazi ya siku mbili nchini humo. Kulia ni Mkuu wa kituo hicho Mama Sahnim Sokaimi.



IMG_5884.jpg

IMG_5892.jpg





Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa somo kwa wasichana watukutu wanaotunzwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia zao cha Pertapis kilichoko jijini Singapore wakati alipokitembelea tarehe 6.6.2013.




IMG_5796.jpg





Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika mazungumzo rasmi na uongozi wa kituo cha kuwatunza wasichana na wanawake watukutu cha Pertapis kilichoko nchini Singapore.



IMG_5840.jpg





Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja kati yake na uongozi wa kituo cha kuwarekebisha tabia wanawake na wasichana cha Pertapis kilichoko huko Singapore wakati alipokitembelea tarehe 6.6.2013. Kushoto kwa Mama Salma ni Mama Badriya Kiondo, Afisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini India.




IMG_5916.jpg





Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akizungumza na Mama Sahnim Sokaimi, Mkuu wa kituo cha kurekebisha tabia za wanawake na wasichana watukutu cha Pertapis kilichoko nchini Singapore mara baada ya kukitembelea tarehe 6.6.2013.

 
Tanzania kumejaa watoto wa kike wa mitaani wasiokuwa na mtetezi, wanabakwa kila kukicha na kuharibiwa maisha yao, leo wanakata mitaa kuwaangalia watukutu wa dunia nyingine, vichekesho havimaliziki Nchi hii.
 
Tanzania kumejaa watoto wa kike wa mitaani wasiokuwa na mtetezi, wanabakwa kila kukicha na kuharibiwa maisha yao, leo wanakata mitaa kuwaangalia watukutu wa dunia nyingine, vichekesho havimaliziki Nchi hii.

tupunguze jazba. Unajua kazi ya WAMA?
 
Mamaangu jamani yupo kazini, Akah! Ebu tumuache afanye finishing, .si Namibia anastaafu..
 
Kaenda kufanya nini huko, mbona first lady wa huko hayupo nae?

Hivi aliyempokea Rais wetu kule ni Rais au waziri fulani? Wenye habari watujuze na picha weka kabisa!!! First Lady wa kule yuko sijui kasafiri naye au? Maana inaweza kuta ratiba ziliingiliana!!!! Ha ha ha!!!
 
Kwa hiyo hata kama mwenye kaya hayupo unang'ang'ania tu uende maana hakuna cha maana unaenda kuzungumza na mwenye kaya ni suala la kufika tu huko ili ule posho, na mimi nagombea 2015 huo urahis.
 
Back
Top Bottom